Watu walioratibu na kutekeleza kumpiga Risasi Tundu Lissu, ni Waovu kuliko hata Shetani Mwenyewe


Huo ugonjwa sina mkuu wangu. Patience kama yote. Ila kama binadamu kujidanganya kwenye kitu kilichopo wazi haiingii akilini.

Mama SSH alianza vizuri na sifa tukammwagia. Anachofanya leo na picha hizo, vitu viwili tofauti:

Baada ya siku 100: Tunapoachana kwenye Mataa na Rais Samia

Picha hizo ndani ya siku zake 100 za kwanza, sawa. Lakini si leo!

"Machoni kama watu."
 
Hakika kuna waovu kuliko shetani, chukulia aliyetengeneza virusi covid 19 , hata shetani ana huruma kuliko yeye.
 

Tundu anatukwamisha na kutukwaza. Watu tunataka kujua sababu ya tukio lile lakini yeye binafsi halichukulii serious kabisa. Sijui kwanini haoni kama uhai wake ulikua mashakani na sijui kwanini haoni kupatikana kwa ukweli utasaidia raia wengine kama yeye kuwa salama kwa kile watakachokijua na kukielewa

Nguvu ambazo amekua akizunguka nazo kuongea angezitumia kuweka mambo bayana ingemsaidia yeye familia yake na watanzania kwa ujumla

Kuendelea kuongea maongezi anayojua wazi hayaleti suluhu ni kutufanya tuanze kuwaza mambo mengine.

Sipendi kuongelea kabisa hili swala la Tundu sababu liliniumiza sanaaa.... lakini kitendo cha yeye kuja kwa kampeni na kuondoka kwa haraka baada ya kushindwa uchaguzi huku akiacha mambo yake yakiwa yananing'inia kwenye vyombo vya usalama inafikirisha sana


Tuache ushabiki tuwaze sawasawa
 

Hata mamba hulia kwa huruma mno akimhurumia mvuka mto.
 
Alijipiga risasi mwenyewe maana askari wetu huwa awakosei shabaha
 
Hakika kuna waovu kuliko shetani, chukulia aliyetengeneza virusi covid 19 , hata shetani ana huruma kuliko yeye.
Yawezekana aliyetengeneza virusi vya corona viliondoka naye. Yawezekana hakujua itakuwa je. Yawezekana alikuwa na nia njema kabisa na labda hata Shetani na hata Mungu wanajua hilo.

Ila huyu aliyekuwa akiagiza, akitekeleza, akipanga na kuratibu mauaji ya akina Lissu, Ben, Azory, Mawazo, wale wa kwenye viroba, nk kwa hakika ni mwovu kweri kweri.

In short ni heri ya huyu mwamba hapa:



Ambaye angalau tunasikia kuna walio mkera na akasema nao hao hao.
 
Vicious people!

I wish they wewe just vicious people.

These are ruthless, merciless, savage, remorseless, bloodthirsty, cold-blooded murderous tyrants.

The devil himself cannot be any worse!
 
I wish they wewe just vicious people.

These are ruthless, merciless, savage, remorseless, bloodthirsty, cold-blooded murderous tyrants.

The devil himself cannot be any worse!
The devil himself cannot be any worse![emoji31][emoji31][emoji31]
 
UJUMBE wao ni huu
"DAMU ISIYO NA HATIA ISIPOKOMBOA HUANGAMIZA"
MUNGU ni FUNDI Wahusika wote Wataangamia Mmoja baada ya Mwingine

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
 
Ni waovu maana wangemmaliza kama Hamza
 
Unataka atoe majibu ya upelezi wa upande mmoja?

Hukuona Tundu alikuja kwa kampeni akaachwa afanye kampeni halafu akaondoka kabla ya siku ya kesi zake na hajarudi??
Kwa Hamza hakutoa ushahidi wa upande moja ?! Uzuri Mungu hachezewi
 
Kama alinyang'anywa ulinzi na simu za maonyo angekaa kukufurahisha ?!. Mbona Leo uchunguzi wa Hamza umefanyika mhusika akiwa hayupo !!
 
Na hata wahi atokee tena duniani bwege yule😂😂😂😂😂😂

Karma is real¡¡¡
Lakini mjue pia kwamba, bila kujali namna gani au wakati gani mtu anakufa, binadamu waliowengi watakufa ingawa najua si wote. Ila ukweli mmoja ni huu, binadamu wote watakaokuwa hai, na watakuwa walikufa, ipo siku tutasimama Mbele za Mungu, aliyetuumba na kutupa fursa ya kuishi duniani lakini tukiwa upande wake. Waliomkataa Mungu watahukumiwa adhabu na waliomkubali Mungu, watakirimiwa.
Kumkataa Mungu ni pamoja na kumpiga jirani yako kwa siri, uasherati, uzinzi, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, uwongo, kiburi, uuaji, uchawi, ushirikina, hila, wizi, chuki, usengenyaji, na yanayofanana na hayo.

Wafanyao mambo ya jinsi hii watahukumiwa. Lakini wakitubu dhambi hizi na kuacha kuzitenda, watasamehewe na Mungu hatazikumbuka tena.

Kama vile waliotaka kumuua Tundu Lisu wasipotubu watasimama hukumuni, vile vile na wanaofanya dhambi kutokana na tukio hilo, watasimama katika hukumu ya Mungu.

Ninyi nyote, MNAOMLAANI NA KUMPIGA MAWE RAIS MAGUFULI KWA KUAMINI KWAMBA NI YEYE ALIHUSIKA katika tukio la kupigwa kwa Tundu Lisu, MNAHAKIKA KWAMBA YEYE NDIYE ALIWATUMA WAUAJI, AU ALIRATIBU MPANGO WA MAUAJI YA TUNDU LISU, AU ALIFURAHIA MOYONI MWAKE TUKIO HILO? MNA HAKIKA KWAMBA ALISHIRIKISWA MPANGO HUO KABLA HAUJATEKELEZWA?
Angalieni ndugu zangu, ushabiki wa mambo msiyoyajua, usije ukawasababisha kufanya dhambi kwa Mungu kisha kuwaingiza hukumuni.
 
Itokee na kwetu
 
Mkuu tumalizane hapahapa duniani, mambo ya mbinguni tuachane nayo
 
Kama hajaratibu, alikataa asiende kutibiwa nje na wakati Nimrod Mkono ana miaka 5 huko, alinyima asiombewe, akaagiza afukuzwe na ubunge.
 
Kama hajaratibu, alikataa asiende kutibiwa nje na wakati Nimrod Mkono ana miaka 5 huko, alinyima asiombewe, akaagiza afukuzwe na ubunge.

Bado sijui kama una uhakika na haya. Ni hilo tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…