Mimi nilitegemea useme tuchukue yaliyo mazuri na mabaya tuwaachie wao.
Na uzuri au ubaya wa jambo hupimwa na mtu/jamii husika lakini pia ni kulingana na sheria za nchi husika.
Mfano, kuvaa vimini sio kosa kisheria lakini inaweza kua tabia mbaya kwako, basi pambania hilo kwenye familia yako lakini kaa ukijua sheria za nchi hailitambui.
Kuimba/kusikiliza nyimbo hasa hizi bongo fleva nk, inaweza kua mbaya kwako lakini sheria za nchi hazitambui hilo, kwako baya ila kwa wengine inawalipa vizuri. Pambana na jamii yako.
Kwahiyo kwenye hizo unazoita "mila za wazungu" kuna mbaya na nzuri, nzuri zibebwe na mbaya zitupwe na hayo ndio maendeleo kiutamaduni.
Mila na desturi sio static, huwa zinabadirika mkuu, 1800's hawakua wanavaa t shirt na jeans, suits, raba nk lakini kutokana na muingiliano wa watu leo hii wewe unaona jeans ni vazi zuri na linafaa, gauni au skirt ndefu kwa ke ni vazi zuri na linafaa.