Watu wameendekeza tamaa kwa kisingizio cha usasa

Point yangu ni kwamba argument zenu hazipo historically accurate; unaongelea USASA na KUVAA mimi nakuuliza kati ya Kuvaa na Kutokuvaa nini kilianza ?

Pili hao ambao wapo uchi; unakutana nao sokoni na kwenye nyumba za ibada au unawatafuta kwenye mitandao au nightclubs ?
 
Zama hizi kujiuza kumeongezeka mkuu na kumechagizwa na kuporomoka kwa maadili hasa ya uvaaji kwa wanawake ambapo hadi watoto wadogo wanaona vyupi vya wakubwa hivyo kujiongeza kuwa wanunuaji

Haya mambo tunayoita old fashion na new fashion ndio yanatuharibia kizazi chetu na dunia kwa ujumla
 
Mavazi ni moja ya mifano inayowakilisha usasa, ila pia usasa unawakilishwa kwa namna nyingi kama vile tabia ya mtu kwa ujumla yaaani kuanzia kuvaa, kula, muonekano na anavyo fikiri

Mfano mwingine halisi ni huo wa kuamini watu kuishi bila kupangiana hizo ni fikra za kinachoitwa kizazi kipya kwa maana haiwezekani mtoto umzae halafu umuache afanye atakavyo bila kumpangia kipi ni sahihi na kipi si sahihi
 
Mkuu are you Serious ? Tena zama hizi mwanamke ana choice ya kukataa au kuomba dau analodhani linafaa..., Tamaduni nyingi enzi zile Baba akipata tu mtoto wa kike anaanza kuhesabu Pesa..., Na tajiri akiona Kabinti anakafanyia Booking Kabisa....

Kwahio Mkuu kila zama na vitabu vyake; ila usidhani hata kidogo kama kuna jipya hapa ni marudio tu....
 
kwenye nyumba za ibada tuliwazuia na kuwarudisha nyumbani na mini zao, na hivi sasa tumeweka vitenge vya kutosha pale nje mlangoni mwa kanisa, ukija na kipensi chako tunakuvisha kanga, ukija na kaoshi tunakuvika lubega na wanawake vivyo hivyo πŸ’

uvaaji wako na usasa wako tunashauri ubaki navyo kwenu πŸ’

Nasisitiza kwamba uovu usipokemewa hatua za mwanzo kabisa ngazi ya familia baadae unakua ni haki nje ya familia,

ndio sasa tunakutana na hoja kama hizi ambazo inaonekana hatuko na historical accuratesπŸ’

Tukizubaa feminists watawini hii vita ya maadili potofu kwa jamii kwa kisingizio cha usasa...

R.I.P Laigwanan comrade ENL
 
Na huku ndo kujiuza kwenyewe ambako nakusemea, tamaa za pesa zinawafanya wadada kupanga madau na kuvaa vichupi na kuongeza maumbo ili wawatamanishe wanunuzi

Ila ukilisemea hili mtu kama wewe unakuja na hoja kuwa "kila zama na kitabu chake" means kujianika ndio kitabu cha sasa
 
Upo sahihi mkuu wanajificha kwenye muda kujustify maovu yao cha kusikitisha kundi hili lenye fikra hizi ni kubwa na lina nguvu kama nguvu za shetani
 
Na mimi ndio nakwambia kwa maneno unayotumia usiweke neno usasa...; hapa hakuna jipya na kwa nyanja tofauti kuna sekta hali ni bora kwa sasa kuliko hapo nyuma....; Na ukiongelea watu kuvaa nusu uchi mimi nakwambia kuna kipindi watu walikuwa wanatembea uchi
 
Hoja zako zote ni kujaribu kuutetea uovu unaofanyika kwa kulinganisha na mila za jamii zinaoendana na unachokitetea japo kiuhalisia hata hizo mila hazikufanya kama wanavyofanya vijana wa sasa
 
Mkuu kwa unavyoona wewe, kuongeza matako,
Teknolojia ilikuwa haipo ila kuna watu walikuwa wanavaa nguo zinabada kiuno ili shape iwe kama nyigu..., Afrika walikuwa wanaweka vyuma ili kurefusha shingo
kuweka nyusi na kope, kujichubua kuwa mweupe kama karatasi,
Hio mbona ilikuwa kawaida kabisa bora sasa hivi wameacha baada ya kugundua madhara kiafya
wanaume kuvaa heleni na kusuka, ambavyo asaiv ni si kitu cha kushangaza mtaani zamani vilikuepo
Ushawaona wamasai ? Na unajua kipindi cha Afro unadhani bila kusuka hizo nywele zingekuwa vipi ndefu ? Na je Rastafarians ? au hio sio kusuka ?
 
Mkuu umewaganda wamasai ambao kwa ukweli kati ya makabila yanaoongoza kwa mila na desturi nzuri ni wamasai hawajawai kuyumba, umemuona wapi masai akidanga na kujiuza
 
Mkuu umewaganda wamasai ambao kwa ukweli kati ya makabila yanaoongoza kwa mila na desturi nzuri ni wamasai hawajawai kuyumba, umemuona wapi masai akidanga na kujiuza
Kwahio Mavazi Sio uzuri wala ubaya wa Desturi ya watu Husika.. Okay hilo tumemaliza ngoja turudi kwenye Kudanga / Kujiuza...

Kudanga na Kujiuza ni kufanya nini ? Je mtu kutumia appearance yake kujipatia kitu ambacho asingepata bila kutumia appearance ni kujiuza ? Kama ndio technically ni wangapi hawajiuzi ?

Wanasema tena bora malaya unajua kabisa unachonunua na unachompa ni kiasi gani yaani Quid pro Quo
 
Huko kote ni kuutetea uovu na kuutafutia sababu uonekane sio uovu ila ukweli unaujua kuwa kwa kuendekeza huo mnaouita usasa wa mavazi na malezi na tabia unasababisha jamii kuwa ya watu wa ajabu ambao hawashauiriki kama wewe
 
Huko kote ni kuutetea uovu na kuutafutia sababu uonekane sio uovu ila ukweli unaujua kuwa kwa kuendekeza huo mnaouita usasa wa mavazi na malezi na tabia unasababisha jamii kuwa ya watu wa ajabu ambao hawashauiriki kama wewe
Ongelea Point kwamba kitu fulani au mavazi fulani hayafai ila usiweke neno usasa mimi nakwambia hata sasa hivi bora watu wanavaa madela enzi za 70s mini ndio zilikuwa mpango mzima....
 
Ongelea Point kwamba kitu fulani au mavazi fulani hayafai ila usiweke neno usasa mimi nakwambia hata sasa hivi bora watu wanavaa madela enzi za 70s mini ndio zilikuwa mpango mzima....
Labda kwenye jamii yako lakini nijuavyo mm hiyo miaka wanawake walikuwa wakivaa khanga na wakijiheshimu wachache sana hasa sehemu za starehe ndo walivaa nguo za ajabu

Kwa upande wa tabia watu waliongozwa na mila na miiko pamoja na dini tabia za uzinzi na uasherati zilihukumiwa kidini na kimila mfano kwa jamii yangu ukifumwa na mwanamke ukoo wenu utatakiwa kutekeleza tambiko na huwa wanatumia mbuzi au kondoo pamoja na faini nyingine

Kwa upande wa malezi familia nyingi zilisimamia watoto wao ambapo tabia mbovu kama umalaya ambao kwa sasa unaonekanwa kawaida kipindi kile ulikuwa ni aibu kubwa kwa familia kuonekanwa mtoto wa fulani ni malaya au ni mvuta bangi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…