Watu wameendekeza tamaa kwa kisingizio cha usasa

Hilo ni kabila la wazigua wanaopatikana Tanga tz vp hapo kuna mwenye matiti yaliokuwa wazi?

Ukweli ni kwamba hatuwezi kuwapotosha jamii na kutetea uvaaji wa kikahaba na tabia nyingine mbovu kwa kigezo eti zamani hawakuvaa huo ni uwongo

Walivaa hadi majani ya migomba(masegere) wakajifunika na vifuani na maeneo ya maungo yao(baadhi ya makabila na sio kama unayotuma ukadhani makabila yote yalikuwa hivyo)

Watu walikuwa na haya(aibu) kwakuwa utamaduni uliwalinda, hawakuvaa ili kushawishiana kingono na kuongeza mashepu kama sasa.
Huo ni mwaka gani na ukienda miaka elfu moja kabla ya hapo ? Hao wamevaa nini hapo Cotton / Pamba ? hizo zao lilikuwa domesticated wakati gani duniani ?
Na kwa hoja yako eti technology ya kuongeza shepu haikuwepo pia ni uongo kwani hadi sasa kuna wanaotumia miti shamba kuongeza shepu(miti ilikuwepo enzi na enzi)

Kwaiyo tukubali kuwa jamii imeporomoka kimaadili kwa ujumla na chanzo ni kuiga mila za wazungu kwa kigezo cha utandawazi na usasa(civilization) View attachment 2903772
Kwamba una miti shamba ya kuongeza makalio inayofanya kazi better kuliko plastic suggery ?

Unaonaje ukinipa recipe ili niweze kuwauzia hukom Ughaibuni huenda kama nchi tukapata mapato kuliko hata tunavyouza Pamba
 
Nadhani wewe una dini fulani (Uislamu au Ukristo) sasa nikuulize hapo nani kamkana babu na bibi yake (sababu waliotuletea hizi dini ndio walisema imani za babu zetu ni za kipuuzi)..

Ila nikitoka huko Binadamu tunajifunza na ku-evolve tunajifunza mazuri na mabaya tunakuwa bora kwahio cha maana wewe kwa misingi yako na imani yako wafundishe watoto wako au kuwa na misimamo yako kulingana na nini ni kibaya na nini ni kizuri UZURI ni kwamba wewe katika nyumba yako una sheria zako na sababu wewe ndio mkuu wa familia na unawalisha na kuwatunza basi utawatungia sheria kadri unavyopenda na kuona inafaa mpaka pale wakitoka kwako na kwenda KWAO hivyo watafanya wanavyotaka.... (So long as hakuna Abuse)

Huo ndio ustaarabu na aina ya maisha inayoweza kutufanya watu tofauti tuweze kuishi sehemu moja kwa kuheshimiana na bila kuingiliana....

To each his/her own...
Mkuu kama umesoma nilichoandika nikuwa

Wengi wa vijana wa sasa(ikiwemo wewe kwa hoja zako) wanatumia kigezo cha usasa(civilization) ili kukana malezi ya wazazi wao na kufuata ya kizungu kwa mgongo wa democracy ( hii inamaanisha kuwa hata nikimfunza mtoto wangu bado ata athiriwa na mazingira ya huko nje na kuja kunika baadae)

Lakini pia wazazi wengi wa sasa(ikiwemo wewe kwa hoja zako) wanatumia kisingizio cha usasa(utandawazi) kukwepa majukum yao ya ulezi kwa kigezo kuwa kizazi cha sasa hakiambiliki, hii inaathiri hata wale wanaosimamia vizuri familia zao kupata changamoto ya ulezi kwa sababu ya muingiliano wa watu( mtu huwezi kumfunga ndani kama kuku)
 
Huo ni mwaka gani na ukienda miaka elfu moja kabla ya hapo ? Hao wamevaa nini hapo Cotton / Pamba ? hizo zao lilikuwa domesticated wakati gani duniani ?

Kwamba una miti shamba ya kuongeza makalio inayofanya kazi better kuliko plastic suggery ?

Unaonaje ukinipa recipe ili niweze kuwauzia hukom Ughaibuni huenda kama nchi tukapata mapato kuliko hata tunavyouza Pamba
Hoja ya kuvaa majani ya migomba(masegere) hapo umeitupilia mbali

Lakini pia unajinasibisha na kujitanabaisha kuwa uko ughaibuni automatically lazima upinge andiko langu kwakuwa hapo ulipo unahisi upo mbinguni(you are civilized) kwaiyo wenye hoja za kuwa na maadili wote ni uncivilized na wakale

Hiyo umeonesha kwa kujali shape hadi wataka nikupe hiyo miti shamba ili uweze kuendeleza sera yako ya civilization shame on you!
 
Mkuu kama umesoma nilichoandika nikuwa

Wengi wa vijana wa sasa(ikiwemo wewe kwa hoja zako) wanatumia kigezo cha usasa(civilization) ili kukana malezi ya wazazi wao na kufuata ya kizungu kwa mgongo wa democracy ( hii inamaanisha kuwa hata nikimfunza mtoto wangu bado ata athiriwa na mazingira ya huko nje na kuja kunika baadae)
Na wewe nakwambia hivi ungefuata mafunzo ya mababu zako sasa hivi usingefanya unachofanya au tabia nyingi zako hata Imani yako huenda isingekuwa hii unayoamini...

Ila nikakwambia ndani ya nyumba yako wewe ni dictator wala haipaswi watoto wako wakupangie nyumba yako sheria zako...; sasa kama unataka kubadilisha tabia / mienendo ya Taifa zima Good Luck....
Lakini pia wazazi wengi wa sasa(ikiwemo wewe kwa hoja zako) wanatumia kisingizio cha usasa(utandawazi) kukwepa majukum yao ya ulezi kwa kigezo kuwa kizazi cha sasa hakiambiliki,
Majukumu gani na malezi yapi ? sababu according to you unaweza kusema hata mwanamke kuvaa suruali haifai au kuangalia muziki au sinema ni dhambi kwahio hayo ndio malezi unayoongelea ? Wewe fanya kazi yako mueleweshe mtoto mema na mabaya kulingana na ufahamu wako kama akipinda na akivunja sheria baadae huko after 18 atafunzwa na ulimwengu...; Issue ni kumuonyesha mtu mema na mabaya na sio kumficha kwamba kuna mema na mabaya (huenda ndani mwako akawa anafanya unavyotaka lakini huku kitaa ndio anatusumbua kwa kutuibia kuku na bata wetu)
hii inaathiri hata wale wanaosimamia vizuri familia zao kupata changamoto ya ulezi kwa sababu ya muingiliano wa watu( mtu huwezi kumfunga ndani kama kuku)
Kwahio unadhani kwamba Binadamu unaweza kumfungia sehemu na kumficha mabaya yote ya dunia akiwa mtoto na mwisho wa siku akiwa mkubwa hawezi kubadilika sababu alivyokuwa mtoto hakupata kitu cha kumpa tamaa ?

Binadamu sio Simple ni viumbe complicated sana na mwisho wa siku mtu akijua mema na mabaya atafanya choices nzuri akiwa na Hekima (ila sio kwamba unamficha mabaya ) au kutaka kupangia jamii nzima iandane na Imani zako...; By the way kwenu nyote mkiwa wachawi na mnakula nyama za watu haimaanishi na wewe utakula sababu umezungukwa na watu waliokula (au kipindi cha Utumwa haimaanishi kila mtu alikuwa anatesa hawa watumwa sababu ilikuwa legal kuwatesa)
 
Na wewe nakwambia hivi ungefuata mafunzo ya mababu zako sasa hivi usingefanya unachofanya au tabia nyingi zako hata Imani yako huenda isingekuwa hii unayoamini...

Ila nikakwambia ndani ya nyumba yako wewe ni dictator wala haipaswi watoto wako wakupangie nyumba yako sheria zako...; sasa kama unataka kubadilisha tabia / mienendo ya Taifa zima Good Luck....

Majukumu gani na malezi yapi ? sababu according to you unaweza kusema hata mwanamke kuvaa suruali haifai au kuangalia muziki au sinema ni dhambi kwahio hayo ndio malezi unayoongelea ? Wewe fanya kazi yako mueleweshe mtoto mema na mabaya kulingana na ufahamu wako kama akipinda na akivunja sheria baadae huko after 18 atafunzwa na ulimwengu...; Issue ni kumuonyesha mtu mema na mabaya na sio kumficha kwamba kuna mema na mabaya (huenda ndani mwako akawa anafanya unavyotaka lakini huku kitaa ndio anatusumbua kwa kutuibia kuku na bata wetu)

Kwahio unadhani kwamba Binadamu unaweza kumfungia sehemu na kumficha mabaya yote ya dunia akiwa mtoto na mwisho wa siku akiwa mkubwa hawezi kubadilika sababu alivyokuwa mtoto hakupata kitu cha kumpa tamaa ?

Binadamu sio Simple ni viumbe complicated sana na mwisho wa siku mtu akijua mema na mabaya atafanya choices nzuri akiwa na Hekima (ila sio kwamba unamficha mabaya ) au kutaka kupangia jamii nzima iandane na Imani zako...; By the way kwenu nyote mkiwa wachawi na mnakula nyama za watu haimaanishi na wewe utakula sababu umezungukwa na watu waliokula (au kipindi cha Utumwa haimaanishi kila mtu alikuwa anatesa hawa watumwa sababu ilikuwa legal kuwatesa)
Kuna mipaka either ya kimila au kidini binadamu lazima awekewe ili kulinda maadili yake hivyo basi kama jamii kuna maadili mabovu ambayo yanaangamiza jamii yetu lazima tupangiane kama jamii tuyatokomeze na sio kuyaruhusu yaendelee kwa kigezo cha democracy na civilization za wazungu
 
Hoja ya kuvaa majani ya migomba(masegere) hapo umeitupilia mbali
Nope wewe umenionesha picha ya watu wamevaa nguo za pamba nikakuuliza hio ilikuwa karne / mwaka gani Na sababu kubwa upatikanaji wa pamba (Mass production) ni rahisi zaidi kuliko kuanza kushape hilo jani la mgomba ili liwe kama gauni na comfortability na muwasho unakuwaje kama ni kwenye joto....; Na kama ni chache watapewa wazazi pekee au mpaka watoto....

Ukiangalia haya mambo wala hayana maadili au nini bali ni necessity na urahisi wa wakati husika....
Lakini pia unajinasibisha na kujitanabaisha kuwa uko ughaibuni automatically lazima upinge andiko langu kwakuwa hapo ulipo unahisi upo mbinguni(you are civilized) kwaiyo wenye hoja za kuwa na maadili wote ni uncivilized na wakale
Mimi ndio nimekwambia wewe kwa imani zako wewe za sasa hivi unaweza ukajikuta wewe ndio unaona kwamba mababu zako ni wa kale na wewe ndio upo civilized sababu unachofanya wewe wao hawakufanya... na sio huku tu hata kule ughaibuni na wao kuna hatua zilizopita kinachofanyika leo huko nyuma hakikufanyika Hizi Old Stone, Middle Stone na New Stone Age sio huku tu hata kule zilipitia...., Binadamu tumepia nyakati tofauti na mambo kubadilika kutokana na nyakati...

Na hayo maadili ndio nikakwambia sio vyote vipya ni vizuri au vyote vya zamani ni vibaya....; na suala la mavazi huenda uchi ulikuwepo zamani kuliko hata sasa....
Hiyo umeonesha kwa kujali shape hadi wataka nikupe hiyo miti shamba ili uweze kuendeleza sera yako ya civilization shame on you!
Nani hajali Shape ? Wewe umeleta story kwamba zamani watu walikuwa hawaongezi makalio nikakwambia technology hio ilikuwa haipo kama sasa hivi wewe ukasema kuna dawa nikakwambia hio dawa kama unayo lete ingredients kama taifa huenda tukawauzia mataifa huko ambao ni wahitaji (sababu its a big business) na mimi sipo hapa kuwapangia watu cha kufanya hata kama mimi sipendi kitu sio kwamba na wao wasipende....
 
Kuna mipaka either ya kimila au kidini binadamu lazima awekewe ili kulinda maadili yake hivyo basi kama jamii kuna maadili mabovu ambayo yanaangamiza jamii yetu lazima tupangiane kama jamii tuyatokomeze na sio kuyaruhusu yaendelee kwa kigezo cha democracy na civilization za wazungu
Mipaka hio anaipanga nani na unajua kwamba mipaka / sheria za Kidini na Kimila / Kitamaduni huenda isiendane au ikapingana ?

Dunia nzima kwa muda mrefu sana iliaminika kwamba mtoto wa kike asisomeshwe au hata akifundishwa afundishwe mambo ya domestic pekee (hio ndio ilikuwa hali halisi enzi na enzi kwa sehemu kubwa sana duniani. Sasa swali linakuja kuwapa elimu watoto wa kike na usasa na yenyewe haifai ?

By the way wazungu ni kina nani sababu hata tukiongelea civilisation sio kweli kwamba ilianzia western....
 
Mkuu maana ya mila na desturi ni nini?

Hata kama binadamu wote tulikuwa sawa lakini kuna tabia na mienendo ikaja kututofautisha na ndio maana leo tunaongea kuhusu African culture na European culture

Kwaiyo hata kama Afrika tulibadilika namna gani lakini hatukufanana na wazungu kwaiyo ni bora tukabaki na uafrika wetu kuliko kuiga ya wazungu

Na kwenye inshu ya uvaaji wa zamani picha nyingi zilipigwa maeneo ambayo wapelelezi wa kwanza wamepitia sio kwa jamii zote utapata picha jinsi walivyovaa, ila unaweza ukakaa na bibi na babu yako akakwambia kabila lenu walikuwa wanavaaje sio kila kabila lilikuwa linaacha maungo wazi kigezo cha joto ni kigezo dhaifu kwani binadamu toka kale aliweza kuyamudu mazingira yake sio hawa ambao wanavaa nusu uchi hata kama kuna baridi(hawa sio binadamu wa kawaida mkuu)

Ukiona wewe hutaki kuwapangia wengine na wewe pia hutaki kupangiwa na huo ndio msingi wa democracy iliyoleta mmomonyoko wa maadili barani kwetu kila mtu anafanya atakavyo kwa kivuli cha democracy mwisho wa siku watoto wetu wanakuwa mashoga na hatuna cha kufanya ni upuuzi na cha ajabu nawewe unaunga mkono
 
Mipaka hio anaipanga nani na unajua kwamba mipaka / sheria za Kidini na Kimila / Kitamaduni huenda isiendane au ikapingana ?

Dunia nzima kwa muda mrefu sana iliaminika kwamba mtoto wa kike asisomeshwe au hata akifundishwa afundishwe mambo ya domestic pekee (hio ndio ilikuwa hali halisi enzi na enzi kwa sehemu kubwa sana duniani. Sasa swali linakuja kuwapa elimu watoto wa kike na usasa na yenyewe haifai ?

By the way wazungu ni kina nani sababu hata tukiongelea civilisation sio kweli kwamba ilianzia western....
Na siku zote dunia nzima hatuwezi kuwa na order inayofanana kama watakavyo wazungu eti human rights watch na mashirika mengine

Order ambazo kiuhalisia wanazitunga wazungu ndio wote tuzifuate hiyo haiwezekani kwaiyo suala la mila na desturi haziwezi kufanana pia kila kabila na mila zao ukiona tumeziacha moja ya sababu ni haya mambo ya kutawaliwa na wazungu either kifikra au kimfumo.

Lakini sababu ingine ni mentality pia mmemezeshwa europian civilization ndio world order kwaiyo anachofanya mzungu na nyie lazima muige kuanzia kula, kuvaa, na staili nzima ya maisha ni upuuzi wa kiwango cha lami
 
Aisee nadhani unachanganya medesa...; Moja nadhani wewe una imani ya hizi dini za sasa kwahio ukiangolea usasa lazima ujue kwamba hata hii Imani hii ya Kikristo na Kiislamu sio Asili yako wewe Muafrika...

Mbili kuna mambo mazuri wala sio kwamba yalitoka uzunguni hata mababu zetu walikuwa wanapigania haki za binadamu kila Nyerere walikuwa wanapigania haki za Muafrika n.k. kwahio Human Rights sio jambo la wazungu na popote ambapo mtu hatendewi haki ni jukumu la kila mmoja wetu kulipinga awe mzungu au chotara haijalishi...

Narudia tena kitu gani walitunga wazungu ? Mambo mengi unayodhani yalianzia western wala hayakuanzia western hizi mila na desturi hata kule zilikuwepo mfano mwanamke kutokupiga kura sio huku tu bali ulimwengu mzima..., unyonyaji bado uliendelea na ilikuwa ni wanaonyonywa mfano utumwa ku-struggle ili kuondokana na utumwa huo ingawa nadhani wewe unadhani ingekuwa bora labda tungeendelea kuwa na uongozi wa kifalme sababu naona demokrasia (Power to the People) unaona haifai...

Unaweza kuniambia hapo wewe umevaa nini na hilo vazi limetokea wapi ? Huenda sio la muafrika na wala halijatokea western kama nilivyokwambia civilisation haikuanzia western...

Unaonglea kula / chakula - hivi haya mazao ya mahindi; mihogo; mchele n.k. unadhani vilitokea Afrika ?

Mkuu angalia mambo kwa mazuri na mabaya yake sio kwa asili sababu I can argue asili ya dunia nzima ni Tanzania pale Olduvai Gorge hivyo wote chimbuko letu ni pale....
 
Kama sio kuiga vya wazungu tanzania na Afrika kwa ujumla tungekuwa mbali sana hasa katika maadili na malezi(kwakuwa maada yangu imejikita hapa)

Hayo unayosema ya uhuru na haki za binadamu ni uzezeta wetu tu kuyaamini na wakati mwingine hatuna namna kwa ajili ya nguvu za kidola lakini mifumo yetu ya utawala kwa kutumia machifu ilikuwa imara sana katika kusimamia mila na desturi zetu na hata kizazi kilichotokana na mifumo hiyo kiko imara sana kimaadili

Mimi na Afrocentric view hatuamini katika hayo mambo ya ulaya kwanza ulaya ndio walioturudisha nyuma kimaendeleo maana tulikuwa na maendeleo yetu tofauti na ushoga
 
Na kuhusu nguo niliyovaa na nilizotuma picha hapo zote zigundulika Afrika kwani technology ya kutengeneza nguo(lather) ilikuwepo Afrika hata kabla ya kuja kwa wazungu maeneo ya benin na Egypt kote uko walikuwa vinala

Hao wa ulaya wamekuja kuwafundisha kutembea uchi tu na kujamiana waume kwa waume ila kama ni inventions tulikuwa nazo kitambo
 
Mkuu aliyesema civilisation imeanzia ulaya ni nani hivi hata unanisoma au ninajirudia kama santuri mbovu ?

Kwahio wewe asili yako ni Egypt au Benin au unadhani hata Egypt walizaliwa wanavaa nguo au hizo za sasa zilikuja baadae kila mahali walijisitiri kulinga na kulichokuwepo kwahio duniani pote wengi ilikuwa either vitu vilivyotokona na mimea au ngozi lakini cotton ilikuja baadae na kabla ya hapo ilikuwa silk ambayo nayo ilitokana na worms...

Kwahiyo unavyoongelea mavazi na ukoloni ni kwamba wakoloni walikuja huku uchi wakawakuta waafrika wamevaa ?!!! Historia yako ni ya wapi ?!!!
 
Kama sio kuiga vya wazungu tanzania na Afrika kwa ujumla tungekuwa mbali sana hasa katika maadili na malezi(kwakuwa maada yangu imejikita hapa)
Mfano ? Kwamba Tanzania / Afrika ni Kisiwa ? Developing countries haziendelei sababu ya marginalization na kunyonywa pamoja na upuuzi wa watawala wa huku na tamaa za kuweza kuuza na kugawa rasilimali kwa mgongo wa vijizawadi...; Hakuna eneo ambalo ni kisiwa wala hakuna teknolojia ya ulaya per se bali teknolojia inachukuliwa sehemu moja na kuboreshwa..... (If I have seen further is by standing on the shoulders of the Giants) mambo ya industrial revolution na vitu kama internal combustion engine zimeitoa dunia katika hatua moja mpaka nyingine ni kwa thinkers kufikiria na kuboresha jambo ambalo linamtoa mwanadamu kama kiumbe katika hatua moja mpaka nyingine ya kupambana na mazingira....

Kuhusu maadili / fashions sio kwamba zinapingwa hapa tu hata kule / popote kuna watu conservative ambao wanaona kwamba vazi hili halifai..., kwahio kwa watu wanaokwenda ufukweni Bikini kwao inavaa sababu hawawezi kwenda kule na baibui (vyote ambavyo sio mavazi ya muafrika asilia) lakini hata hio bikini huwezi kusema aliigundua mtu wa kule sababu vazi la kufunika sehemu za siri na kwenye kifua lilikuwepo tangu enzi na enzi...
Hayo unayosema ya uhuru na haki za binadamu ni uzezeta wetu tu kuyaamini na wakati mwingine hatuna namna kwa ajili ya nguvu za kidola lakini mifumo yetu ya utawala kwa kutumia machifu ilikuwa imara sana katika kusimamia mila na desturi zetu na hata kizazi kilichotokana na mifumo hiyo kiko imara sana kimaadili
Uhuru na Haki ni nini ?

Kwamba vice versa ya uhuru na haki ndio asilia yetu na ni bora kuliko uhuru na haki ya mtu ? Kwamba enzi za utumwa zilikuwa bora kuliko sasa hivi ambapo mtu hauna haki ya kumiliki binadamu mwenzako ?

Machifu ni kwamba kuna sehemu ilikuwa mtu unakuwa kiongozi sababu ya uzao wako (na kwa taarifa yako hii haikuwa Afrika tu bali duniani kwa ujumla) sasa unaona hio ilikuwa bora ?!!!
Mimi na Afrocentric view hatuamini katika hayo mambo ya ulaya kwanza ulaya ndio walioturudisha nyuma kimaendeleo maana tulikuwa na maendeleo yetu tofauti na ushoga
Kwahio ulaya ni ushoga ? Na vilevile narudia tena mara nyingine sio kweli kwamba civilization ilianzia ulaya..., kwahio mkuu wewe amini unachoamini ila usipindishe facts kujaribu ku-paint picha unayotaka wewe wakati mambo hayapo hivyo yalivyo....

Hivi unaujua hata UK Allan Turing Mmoja wa Magwiji wa Hesabu na alieyesaidia sana katika mambo ya Artificial Intelligence alikufa vipi kutokana na kuwa Gay....

Turing was prosecuted in 1952 for Homosexual Acts. He accepted hormone treatment with DES, a procedure commonly referred to as Chemical Castration, as an alternative to prison.

Prosecution hio ikapelekea mwisho wa siku kuondoa uhai wake....; Kwahio mkuu wewe unachosema kwamba utamaduni wa ulaya ni ushoga nashindwa kukuelewa issue ni kwamba hawawi prosecuted kama wewe unavyotaka labda wapigwe risasi au kuuliwa au kuchinjwa (jambo ambalo hata mimi binafsi sitaki kuishi kwenye eneo la watu kuchukua sheria mkononi) mfano mtu akiiba sijui akatwe mkono au mwingine apofushwe macho n.k. (sababu mataifa ya hivyo pia yapo)
 
Mfano ? Kwamba Tanzania / Afrika ni Kisiwa ? Developing countries haziendelei sababu ya marginalization na kunyonywa pamoja na upuuzi wa watawala wa huku na tamaa za kuweza kuuza na kugawa rasilimali kwa mgongo wa vijizawadi...; Hakuna eneo ambalo ni kisiwa wala hakuna teknolojia ya ulaya per se bali teknolojia inachukuliwa sehemu moja na kuboreshwa..... (If I have seen further is by standing on the shoulders of the Giants) mambo ya industrial revolution na vitu kama internal combustion engine zimeitoa dunia katika hatua moja mpaka nyingine ni kwa thinkers kufikiria na kuboresha jambo ambalo linamtoa mwanadamu kama kiumbe katika hatua moja mpaka nyingine ya kupambana na mazingira....

Kuhusu maadili / fashions sio kwamba zinapingwa hapa tu hata kule / popote kuna watu conservative ambao wanaona kwamba vazi hili halifai..., kwahio kwa watu wanaokwenda ufukweni Bikini kwao inavaa sababu hawawezi kwenda kule na baibui (vyote ambavyo sio mavazi ya muafrika asilia) lakini hata hio bikini huwezi kusema aliigundua mtu wa kule sababu vazi la kufunika sehemu za siri na kwenye kifua lilikuwepo tangu enzi na enzi...

Uhuru na Haki ni nini ?

Kwamba vice versa ya uhuru na haki ndio asilia yetu na ni bora kuliko uhuru na haki ya mtu ? Kwamba enzi za utumwa zilikuwa bora kuliko sasa hivi ambapo mtu hauna haki ya kumiliki binadamu mwenzako ?

Machifu ni kwamba kuna sehemu ilikuwa mtu unakuwa kiongozi sababu ya uzao wako (na kwa taarifa yako hii haikuwa Afrika tu bali duniani kwa ujumla) sasa unaona hio ilikuwa bora ?!!!

Kwahio ulaya ni ushoga ? Na vilevile narudia tena mara nyingine sio kweli kwamba civilization ilianzia ulaya..., kwahio mkuu wewe amini unachoamini ila usipindishe facts kujaribu ku-paint picha unayotaka wewe wakati mambo hayapo hivyo yalivyo....

Hivi unaujua hata UK Allan Turing Mmoja wa Magwiji wa Hesabu na alieyesaidia sana katika mambo ya Artificial Intelligence alikufa vipi kutokana na kuwa Gay....

Turing was prosecuted in 1952 for Homosexual Acts. He accepted hormone treatment with DES, a procedure commonly referred to as Chemical Castration, as an alternative to prison.

Prosecution hio ikapelekea mwisho wa siku kuondoa uhai wake....; Kwahio mkuu wewe unachosema kwamba utamaduni wa ulaya ni ushoga nashindwa kukuelewa issue ni kwamba hawawi prosecuted kama wewe unavyotaka labda wapigwe risasi au kuuliwa au kuchinjwa (jambo ambalo hata mimi binafsi sitaki kuishi kwenye eneo la watu kuchukua sheria mkononi) mfano mtu akiiba sijui akatwe mkono au mwingine apofushwe macho n.k. (sababu mataifa ya hivyo pia yapo)
Hivi mkuu machifu walipractice utumwa? Maana naona waliongelea sana hili
 
Kwenye uchifu kuna Matabaka - Kuna viongozi ambao ni machifu (na mara nyingi uongozi huo ni wa kurithi) kwahio kuna mabwana na watwana kuna watu ambao maisha yao ni kutumikia wengine; Wewe kama babu yako alikuwa mtumwa / mtwana ni vigumu kwa wewe mjukuu kuja kuwa chief... Na mfumo huu wa uongozi sio tu kwamba ulikuwepo Afrika pekee bali dunia nzima...

Ila ilifika wakati watu (common people) wakiona sio sawa watu watutawale sababu tu ni wa ukoo fulani na uchifu ukafa kifo cha kawaida..... Na sehemu ulipobaki sanasana ni symbolically na hauna nguvu sana

Ukionglea utumwa achana na huu wa Taifa moja kuja kuchukua watumwa wa Taifa jingine; ilikuwa watu mkiwa masikini; mateka wa vita; mfalme , chifu akiamua / akiona nyie sio anaweza akawa-brand kama watumwa au kama mnafanya kazi kwa kabaila fulani yule ndio Bwana wenu nyie Watwana.....

Kwahio katika Uongozi wa Kifalme / Kichifu wakati uzalishaji ni duni na mahitaji ya luxury hayatoshi unajikuta kuna wachache wanaokula hio keki ya jamii kwa mgongo wa kwamba wao ni bora (ni tofauti ya sasa ambapo mtu anaweza akatoka kwenye Utwana kwenda kwenye Ubwana kirahisi) katika chiefdom huenda usifanikiwe sababu tu Babu yako hakuwa damu ya Machifu...
 
Dunia inavobadilika hakuna mtu yoyote wa kuizuia. USASA hauepukiki na kua limited na mawazo ya wazazi wako au mila na desturi ni kutojitendea haki mwenyewe. Nobody in this world knows what is right or wrong vitu vyote vya kibanaadamu vipo limited,so kijana kubadilika na kufatisha kila anachoona kinachofaa bila kujali wazazi au jamii yake ni matumizi mazuri ya free will yake na uhai wake anavootumia.

Wewe ni nani kujiona unajua kipi kizuri au kibaya kwenye dunia hii ya miaka billioni 4 ambapo binaadamu amekuja kwenye dunia hii kama miaka millioni kadhaa tu iliyopita.
 
Kwaiyo wewe unaamini kuwa democracy ya wazungu na capitalism kila mtu anakula national cake?
 
Ukisema dunia unakosea mkuu sema kwa jumuia ya wazungu

Kuna nchi za asia na uarabuni watu hawafati philosophy ya democracy ya kujiamulia tu hata ukiwa shoga wanakuangalia eti ni haki yako haipo hivyo

Afrika tu ndo tumeshikwa akili na wazungu
 
Kwaiyo wewe unaamini kuwa democracy ya wazungu na capitalism kila mtu anakula national cake?
Demokrasia sio ya Wazungu ni mfumo ambao ingawa mara nyingi ni theoretical na unadangaya watu kwamba kweli kinachofanyika wanaamua wenyewe ila inaleta uhuru na Amani...; sababu at least wanaona kwamba aliyepo walimchagua... sababu Demokrasia inatokana na maneno yanayomaanisha nguvu ya watu / umma (kwahio watu wenyewe ndio wanongoza) tofauti na kutawaliwa (atleast hii notion hata theoretically inaleta ahueni)

Ubepari huo ni mfumo tu wa kiuchumi ambapo na wenyewe angalau theoretically unaonyesha kwamba ukipigana unaweza ukawa tajiri (ni nguvu zako na jasho lako) ingawa practically kuna ugumu na kuna faulo na technology inavyoendelea huenda hata mfumo huu wa ubepari wa leo usiwepo kesho.... Sababu umeleta matabaka makubwa ambayo huenda yalikuwepo enzi za Ukabaila na Ubwanyeye.....

Kwahio hii mifumo be it an illusion or not atleast inakupa hope kwamba hata ukizaliwa masikini legally unaweza ukawa mtu yoyote (tofauti na mifumo ya kifalme legally huenda hautaruhusiwa kutoka kwenye tabaka lako)
 
Back
Top Bottom