Usaili wa kuandika katika kada ya afya umefanyika Septemba 3, 2024 nchi nzima ili kuwapta wataalam wa afya watakaojaza nafasi 9, 483 za ajira.
Wakati usaili huu ukiwa unaendelea ilisambaa video mtandaoni ikionesha binti akiwa anasukumwa na Mwanaume akiwa ameshika karatasi kati ya watu wengine walioshika karatasi ndani ya chumba, huku Watu wanaosambaza video hiyo wakidai ni tukio lililotukia kwenye moja ya vituo vya usaili, Tazama( hapa na hapa)
Ukweli ni Upi?
JamiiCheck imefuatilia video hiyo kupitia utafutaji wa kimtandao kwa kutumia Google Reverse Image ili kufahamu uhalisia wa video hiyo inayodaiwa kuwa ni ya tukio lililotokea kwenye moja ya maeneo yaliyofanyika usaili katika kada ya afya nchini.
Tumebaini kuwa video hiyo si ya Tanzania na haihusiani na usaili katika kada ya afya, video hiyo ni ya Congo na iliwekwa mtandaoni tarehe Agosti 26, 2024 (Tazama hapa) na kuendelea kusambaa, (tazamahapa) ikionesha tukio lililotokea Congo DRC.
Ufuatiliaji wa kimtandao unaonesha tukio hili lilimuhusisha binti wa chuo chaISTA Kolwezi lundi (l’Institut Supérieur des Techniques Appliquées (ISTA)) ambaye alishambuliwa na mwalimu akiwa kwenye mtihani Mwalimu anafahamika kwa jina la Tshipamba Kabwe.
Barua ikionesha kusimamishwa kazi kwa mwalimu aliyemshambulia mwanafunzi huyo
Lakini na nyie wanawake ifike wakati mjifanyie tafakari maneno mnayotamka kwa watu wengine aidha mpenzi, mume au swahiba kazini kuna muda mtu anashindwa kuhimili yale maneno mwisho yanatokea ya kutokea. Anakuja kulaumiwa na tutamlaumu kweli mtendaji wa tukio kama huyo jamaa hapo. Wote tujifunze kulinda midomo yetu sio kulopoka lopoka tu.
Mkuu unaweza kuta kazi yenyewe ni stress tosha kwa kuzingatia mazingira kama hayo unayoona. I believe in judgement everything should be put fairy not in favor to benefit the less
Hakuna mtu huwa anapewa ruhusa ya kupiga mtu au kutukana mtu ila lazima tukumbushane kwamba ukiwa kiongozi haimaanishi kwamba Hasira na hisia zako zinakufa Hapana,
Ndomaana ni vibaya kutukana mtu au kupiga mtu lakini kuna namna huwez kudhibiti hisia haswa pale tukio linapogusa Utu wako wa ndani,
Ndomaana hata Rais Samia juzi alisema "Kuna Mbwa mpumbavu anabwekea maendelea yetu" kauli hii si sahihi kutoa kiongozi lakini baada ya kupata Hisia za hasira alishindwa kujizuia na kuitoa.... Hivyo kuna namna huwezi kuzuia baadhi ya maneno au matukio haswa pale Utu wako wa ndani unapoguswa.
Tatizo wazazi tumesahau wajibu wetu kuwafundisha watoto nidhamu na adabu, hata wale waliofundishwa adabu bado wengi ni vichomi. Inasikitisha, hasa kama mzazi kuona binti yako anapitia udhalilishaji wa namna hiyo wakati akiwa na msongo wa kupata ajira.