Watu wanaamini kuna Mungu na shetani kwa sababu kuamini ni rahisi kuliko kufikiri

Sio tu hayupo.

Mungu hajawahi kuwepo, hayupo na hata uwezekano wa kuwepo kwake Haupo.
Uwezo wako bado mdogo ila hatua kwa hatua utaelewa kuwa MUNGU yupo hapo hapataki haraka na mkurupuko na majibu ya jumla kama unayotoa,kaa na ufikiri utaona kitu kama hutaki kufikiri basi baki akili yako ndogo inayogoma kufikiri.
 
Sio tu hayupo.

Mungu hajawahi kuwepo, hayupo na hata uwezekano wa kuwepo kwake Haupo.
Uwezo wako bado mdogo ila hatua kwa hatua utaelewa kuwa MUNGU yupo hapo hapataki haraka na mkurupuko na majibu ya jumla kama uliyotoa
Mm naamini wewe una akili nyingi sasa ktk hizo akili nyingi ulizonazo umewah kufanya jambo gani kwa vitendo na likawashangaza watu wengi na linaloshikika.
 
Sio tu hayupo.

Mungu hajawahi kuwepo, hayupo na hata uwezekano wa kuwepo kwake Haupo.
Uwezo wako bado mdogo ila hatua kwa hatua utaelewa kuwa MUNGU yupo hapo hapataki haraka na mkurupuko na majibu ya jumla kama uliyotoa
 

Nimesema kwenye imani KILA KITU KINAWEZEKANA........Inakuingia akilini?
 
Inategeme Mungu wako ni yupi, maana watu qwana kila aina ya Miungu. Kuna wenye miungu watu, miungu ng'o,be, miungu vitu.

Sisi Waislam tunaamini hakuna mungu apasae kuabidiwa isipokuwa Allah.

Hazai wala hajazaliwa na hakuna anachofanana nacho.
Binadamu anaongozwa na ubongo, hivyo uwezo wako ndo umefikia hapo na upo sahihi kutokana na mawazo yako maana ubongo hauwezi kufikiri zaidi ya hapo.
 
Mungu ametengenezwa na Mawazo ya Binadamu ili kupata faraja tu , bila Binadamu hakuna Mungu
Kipi hicho chenye kumfanya binaadamu atafute faraja na ina maana wasioamini Mungu hawana faraja au kukana Mungu nao ni faraja kwao?
 
Mungu yupo na anatenda.

Matendo yake hayana mfano hata kidogo.

Kitu kinachotukwamisha ni upeo na uwezo mdogo kwa kukubali kuongozwa na wachungaji na ma sheikh
 
Tatizo umekula na umeshiba ndio maana unaongea utopolo ,ila ungekuwa na njaa hata hii jeuri usingekuwa nayo,na kiburi chako adabu yake ni siku ya kufa tu ndio utajua kuwa mungu yupo au hayupo
 
Tatizo umekula na umeshiba ndio maana unaongea utopolo ,ila ungekuwa na njaa
hata hii jeuri usingekuwa nayo,
Huyo Mungu anashindwa kuwapa chakula watoto wadogo wanaokufa kwa njaa maeneo mbalimbali duniani halafu aje anipe shibe mimi?

Huyo Mungu uwezo wa kunishibisha Hana.

Huyo Mungu hajawahi kushibisha mtu yeyote kwa vile Hayupo na hata uwezekano wa kuwepo kwake Haupo.
na kiburi chako adabu yake ni siku ya kufa tu ndio utajua kuwa mungu yupo au hayupo
Ulishawahi kufa ukajua huyo Mungu yupo?

Au unaleta vitisho na hofu ulivyo pumbazwa na dini yako?

Nakwambia hivi, huyo Mungu hajawahi kuwepo, hayupo na hata uwezekano wa kuwepo kwake Haupo.

Kama Mungu huyo yupo mwambie aje hapa ajidhihirishe.
 
Soon atafika apo kwako na atakudhihirishia kwamba yeye yupo tena kwa vitendo ili ujue kuwa mungu hadhihakiwi, utaleta mrejesho.
 
Soon atafika apo kwako na atakudhihirishia kwamba yeye yupo tena kwa vitendo ili ujue kuwa mungu hadhihakiwi, utaleta mrejesho.
Mpaka sasa Mungu huyo Kashindwa kufanya chochote, Kashindwa kuja hapa kujidhihirisha.

Unabaki kumtetea na kumpigania ilhali yeye mwenyewe hawezi kujitetea 😂

Nakwambia hivi, Huyo Mungu ni Mdhaifu sana.

Niko hapa namsubiri huyo Mungu aje!!
 
Nilikimbia seminary baada ya kunipatia bible verses, nitafakari na nisikilize sauti ya mungu na niwaambie Mungu kaniambia nini!
 
Nilikimbia seminary baada ya kunipatia bible verses, nitafakari na nisikilize sauti ya mungu na niwaambie Mungu kaniambia nini!
Hiki kilikuwa kituko Cha mwaka.
Hiki kilikuwa kipimo kikubwa Cha unafiki, uzandiki na uongo.

Walitaka ukisie kwa kutumia fikra na akili zako ili baadae utoke na jibu la kubumba halafu useme ndio sauti ya Mungu.

Dunia ni unafiki na unafiki ndio dunia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…