Watu wanaamini kuna Mungu na shetani kwa sababu kuamini ni rahisi kuliko kufikiri

Watu wanaamini kuna Mungu na shetani kwa sababu kuamini ni rahisi kuliko kufikiri

Kuamini kungekuwa rahisi robo tatu ya dunia wangekua wacha Mungu.
 
UUpo
Pia kuna wale wapuuzi wanaosema kuwa dini zimeleta maadili mema, jambao ambalo si kweli, mtu mwenye akili timamu haitaji dini wala imani yoyote kufanya mambo mema bali kuheshimu haki za wengine na sheria za kiutu.

Hatumuhitaji Mungu ili tufanye mema, hatutakiwi kufanya mema kwa kumuogopa Mungu bali kwa kujari utu wa wenzetu
Upo sawa ndo maana majambazi waporaji wauaji wachawi woote Wanasali na kuswali na ukienda huko urusi Korea kusini japani china hakuna Yesu Wala Muhammad na ndiyo wanatulea misaada ya dawa za malaria na kipindupindu sisi wente Mungu.
 
Ulimwengu wa tatu kazi yao ni kukariri tu badala ya kufikiri. Mf. Kariri kuwa "Yesu alifufuka" bila kuhoji unakariri tu! Mf Mungu gani anaetoa kafara kama binadamu wanavyofanya?.
 
Unachanganya mambo mkuu.

Kilichozungumziwa ni makazi ya Rais ambayo ni ikulu na si nchi, Mungu ambaye inaaminiwa kuumba huu ulimwengu tuliyopo ndio tunazungumzia hayo makazi yake ambayo inaaminika ni mbinguni.

Sasa ukienda ikulu na usimkute rais hiyo haina maana hakuna huyo rais au kama hakuna ikulu pia hatuwezi kusema hiyo nchi haina rais.
Kama hakuna ikulu basi raisi hayupo, kwasababu, anakotakiwa kuwepo tu hakupo, na hapa issue sio kumkosa ikulu,issue ni ikulu yenyewe kutokuwepo, sasa tunauliza hiyo ikulu haipo, je yeye atakuwa wapi, kwamba mlikosea kusema kuwa raisi yupo ikulu na kumbe sio kweli? Okay yuko wapi sasa? Mbona hamtuombi radhi kama mnajua mlikosea? Tunaomba kujua raisi alipo.
 
Kama hakuna ikulu basi raisi hayupo, kwasababu, anakotakiwa kuwepo tu hakupo, na hapa issue sio kumkosa ikulu,issue ni ikulu yenyewe kutokuwepo, sasa tunauliza hiyo ikulu haipo, je yeye atakuwa wapi, kwamba mlikosea kusema kuwa raisi yupo ikulu na kumbe sio kweli? Okay yuko wapi sasa? Mbona hamtuombi radhi kama mnajua mlikosea? Tunaomba kujua raisi alipo.
Kwahiyo kuna watu waliwahi kwenda huko kuitafuta hiyo ikulu?
 
Huwa naona kama kutokuamini Mungu kuna husishwa moja kwa moja na kuwa na akili sana, hivi kwa nini inakuwa hivyo japo kwenye maisha ya kawaida hakuna huo utofauti kuonyesha kuwa wasioamini Mungu ndio wenye akili kuliko wenye kuamini Mungu?

Mkuu tatizo ni kwamba wanao amini katika Mungu kimsingi ni kwamba wamekataa kutumia AKILI zao timamu na kuamua KUAMINI tu linapokuja swala la MUNGU

Kuna mambo kwenye IMANI unatakiwa kujitoa ufahamu ili kuya amani
 
Mkuu tatizo ni kwamba wanao amini katika Mungu kimsingi ni kwamba wamekataa kutumia AKILI zao timamu na kuamua KUAMINI tu linapokuja swala la MUNGU

Kuna mambo kwenye IMANI unatakiwa kujitoa ufahamu ili kuya amani
Ukiwa na maana ipi hebu fafanua?
 
Katika suratul- baqrah Kuna aya inazungumzia malaika walivyokua wakibishana na mungu juu ya suala la mungu kumuumba mwanaadamu, malaika walimwambia mungu kuwa ukimuumba mwanaadamu atakwenda kufanya maasi na umwagaji wa damu duniani, mungu akawaambia malaika kuwa yeye anayajua wasioyajua wao, hata dunia ya leo Kuna watu bado wanajifanya kuwa na zile zile tabia za kimalaika ingawa wote walitubu kwa kumsujudia Adam pale alipoumbwa isipokua ibilisi, kwa hiyo ndugu muandishi nakushauri utubu kabla milango ya toba haijafungwa, vyenginevyo mwisho wa siku utakuwa mfuasi wa shetani,
Pia wakati wa mtume Muhammad alikuwa Ana somesha darsa Kuna watu walikuwa wanaenda barazani kwake kusoma, siku moja aliwaambia baadhi ya dalili za kiama na moja wapo ni kuwa siku hiyo jua litachomoza kutokea magharibi na sio mashariki Kama ilivyo zoeleka, katika darsa hiyo Kuna mtu mmoja alimuuliza mtume Muhammad je Kama jua halikuchomoza magharibi? mtume Muhammad alikuwa anamuheshimu sana yule mtu kutokana na muonekano wake na mavazi yake ya gharama aliyokuwa akiyavaa, mtume Muhammad alifikiri mtu Yule ni katika watu wenye busara na hekima sana, lakini kutokana na swali alilouliza mtume Muhammad alimuona kumbe Hana chochote kichwani mwake kutokana na swali alilouliza, unadhani kwa Nini mtume Muhammad alimshusha hadhi mtu Yule? Ndugu muandishi nakuomba ujibu suala hili kwa kutumia hiyo akili yako inayokufanya uone ufakhari kupinga uwepo wa Mungu, kwa sababu watu ambao hawana majibu ya uwepo wa Mungu na wanaendelea kuamini au kukaa kimya na kutozungumza wasichokijua huenda wakawa na busara na hekima kubwa kuliko wewe ambae ni debe tupu.
 
Muhammad (S.A.W)
IMG_20240121_004836.jpg
 
Ili twende sawa kidogo, kama hutajali naomba kujua unamuamini Mungu wa imani ipi ili nikupe mifano
Unajua imani ziko nyingi sana mkuu sasa sidhani kama unazijua imani zote duniani.
 
Okay,.Kifo pia kina faida zake nyingi Tu,......Wewe umeamua kufocus na hasara za kifo,.vipi kuhusu faida za kifo?



NB:- Uhai&kifo vyote hivyo vina faida na hasara. Both are scary & exciting!
Issue sio kufa, je unakufa kifo gani? Kufa Kwa njaa utapenda ww ufe Kwa njaa?
 
Unajua imani ziko nyingi sana mkuu sasa sidhani kama unazijua imani zote duniani.
Hii ndio changamoto ya kujadili na waamini Mungu mkuu

Hapo juu nimesema kuna mambo kwenye imani ya Mungu inabidi ujitoe ufahamu kukubaliana nayo
Ukataka kujua ni mambo hani?
Ndio nikakuuliza wewe uniambie unamuamini Mungu yupi ili nikupe mfano wa mambo hayo

Maana nikikwambia mambo ya Allah wakati wewe ni wa Jehova au kinyume chakke hatuta elewana
 
Back
Top Bottom