DOKEZO Watu wanaodhaniwa Askari wa Polisi na Maafisa Msitu wawapiga Wananchi, kuchoma moto makazi na mazao Wilaya ya Chemba na Ikungi

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
wahame mara moja kwenye eneo la hifadhi
Hifadhi gani ile? Je, kuwaondoa watu kwenye hifadhi ni kuwapiga? Hifadhi za misitu zinajulikana. Hifadhi hutambulika baada ya kutangazwa kwenye gazeti la serikali. Kuna uthibitisho gani kwamba kile kijiji ni hifadhi? Je, umewahi kufika uweze kuelewa ninachozungumza?
 
Wale wananchi wanaonewa kwa sababu ni wanyonge. Ni maskini na wengi wao hawajaenda shule kabisa au elimu ni ndogo.
Kuna taarifa kwamba changamoto kubwa ni kutojulikana mpaka katika ya wilaya mbili za mkoa wa Singida na wilaya ya Chemba katika mkoa wa Dodoma. Hill litatuliwe kwanza. Wale wananchi hawakuvamia pori. Waligawiwa na kijiji chao. Kwanini kijiji hakikuamrishwa kuwaondoa wananchi ili kama bado ina maeneo, iwagawie tena ili kuendelea na shughuli zao.
Taarifa zinasema wale wananchi wamekuwa pale Toka mwaka 2013.
Kwanini hizi tafrani zipambe moto kuanzia mwaka Jana tu?
 
Ujue hilo eneo wameshalihusudu wanatafuta mwekezaji.

Sababu utasikia ni hifadhi ya serikali.
 
Ujue hilo eneo wameshalihusudu wanatafuta mwekezaji.

Sababu utasikia ni hifadhi ya serikali.
Nadhani hili ndo linafanyika. Productivity ya lile eneo ndio chanzo cha kuumizwa kwa wananchi wanyonge wale.
 
Hivi yule askari aliepotelea msituni akihofiwa kuuawa na wafugaji alipatikana?
 
Malengo makuu la Taifa lolote ni
1. Kuwa na mipaka inayotambuliwa na mataifa mengine.
2. Ustawi wa watu wake.
3. Kujitawala.
Watu wanaowaua wengine na kuwahukumu bila kufuata misingi ya kisheria iliyowekwa, wanapuuza na kuondosha lengo namba 2 la kuwa kama Taifa.
Tuna Taifa linaloeleweka. Siyo Taifa la kila mtu kujichukulia sheria mkononi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…