Watu wanaoongoza kwa kuchukiwa humu JF

Watu wanaoongoza kwa kuchukiwa humu JF

Ni ulimbukeni kumchukia mtu ambae kiuhalisi yupo kinadharia zaidi, maana kuna baadhi ya watu wanachangia kama mademu kumbe midume, kuna mafukara wanaojifanya matajiri. Kwa kifupi kumchukia mtu wa JF ni sawa na kumchukia actor anaeigiza kama adui kwenye movie, ni maigizo tu.

Katika point hiyo hiyo, kuna baadhi ya watu wanatafuta kuchukiwa kwa makusudi ili iwe ndio umaarufu wao. Maana unaweza kuta jitu linatukana tu pasi na sababu za msingi.

Kama vile baadhi tunavyofanya JF kuwa sehemu ya kupoteza muda, kuna wengine ndio sehemu pekee uwepo wao unatambulika hata ukiwa ni kwa jina la uongo. Ili kujipa thamani ya nafsi yake ndio unakuta anaanzisha maugomvi yasiyo na tija. Ukichunguza walio wagomvi wengi humu maisha yao halisi yamejaa upweke na jitimai.
We mbwah umesema kweli kabisa...🤣🤣🤣🤣 Falah sana wewe yaani nimecheka ile mbaya. Nikasema huyu mbwah yupo sahihi......
 
Hahahaa! Jina la ID yako linavaa uhusika wa akili yako inaelekea unamaarifa mengi 🤣🤣🤣

Hakujua wapi apeleke lawama zake, Sema amekupatia pamoja na maarifa yako yote, Kwa huyo dada ndio mwisho wa mbwembwe zako..
Aaargh wapi. Nlimchezea mchezo alikuja gundua too late. Nlitumia hii ID alikuwa hafahamu kuwa nayo ni yangu akaja gundua kusudi langu too late. Wanawake tukae nao kwa akili bob
 
We mbwah umesema kweli kabisa...🤣🤣🤣🤣 Falah sana wewe yaani nimecheka ile mbaya. Nikasema huyu mbwah yupo sahihi......
Daah! Mbona hivi tena jamaa amekosa nini sasa hadi kuwa mbwah!!
Katika point hiyo hiyo, kuna baadhi ya watu wanatafuta kuchukiwa kwa makusudi ili iwe ndio umaarufu wao. Maana unaweza kuta jitu linatukana tu pasi na sababu za msingi.
au hichi kipengele kina kuhusu Chizi Maarifa
 
Daah! Mbona hivi tena jamaa amekosa nini sasa hadi kuwa mbwah!!
Nadhani umeelewa point yangu. Kinachotafutwa hasa ni ule ubishani ambao kwa mwenye kutoa matusi kihalisia anatafuta njia ya kupata amani ya nafsi yake kwa kujibiwa ili ajihisi na yeye yupo ulimwenguni.

Hili namithilisha na kitendo cha kuibiwa nguo zako na mwendawazimu ukiwa unakoga na kuanza kumfukuza. Kwa halaiki wasiojua kilichotokea wewe ulie uchi ndie utaonekana mwendawazimu, halkadhalika kumjibu mtu anaekutukana pasi sababu atakaekutia matusi kati anaweza hisi wewe ulietukanwa ndie mkorofi.
 
Huyo namba 1. Mtoe hafai kuwepo hapo toka aanzishe Uzi wa kumroga mfanyakazi mwenzao, hastahili kuwepo hapo kwanza Hana mchango wowote wa hoja zenye mashiko.
 
3. Huyu demu jina lake limenitoka ila naye nimesoma mara kadhaa wakisema ana msongo wa mawazo kutokana na nyuzi anazoanzisha akiamini anarogwa, hapendeki,malaya,anatengwa, anaonewa wivu,anaonekana kachoka n.k so ikamfanya kila jambo katika hayo alifungulie uzi. Mpaka alipopelekwa hospital (watu wanasema hivyo) na kugundulika ana msongo wa mawazo na kulazwa ndo kumetulia. Huyu atakuwa binti mwembamba sana amekauka mwili

Itakuwa umeogopa kichambo cha Yuniki Fulawa...
 
Nadhani umeelewa point yangu. Kinachotafutwa hasa ni ule ubishani ambao kwa mwenye kutoa matusi kihalisia anatafuta njia ya kupata amani ya nafsi yake kwa kujibiwa ili ajihisi na yeye yupo ulimwenguni.

Hili namithilisha na kitendo cha kuibiwa nguo zako na mwendawazimu ukiwa unakoga na kuanza kumfukuza. Kwa halaiki wasiojua kilichotokea wewe ulie uchi ndie utaonekana mwendawazimu, halkadhalika kumjibu mtu anaekutukana pasi sababu atakaekutia matusi kati anaweza hisi wewe ulietukanwa ndie mkorofi.
True saying budhaa! Ila watambue kwamba matusi ni mwanzo wa kujidharaulisha wenyewe na si kwamba wanaonekana ni werevu hapana tunawaona ni watu dhaifu kwenye jamii na si wenye maadili sawa sawa!
 
True saying budhaa! Ila watambue kwamba matusi ni mwanzo wa kujidharaulisha wenyewe na si kwamba wanaonekana ni werevu hapana tunawaona ni watu dhaifu kwenye jamii na si wenye maadili sawa sawa!
malezi ya utotoni huakisi moja kwa moja tabia za ukubwani. Ukiona mtu anaendekeza matusi na lugha mbovu ujue hivyo ndivyo alivyolelewa na chances are hivyo ndivyo atakavyolea kizazi chake.
 
Back
Top Bottom