Ni ulimbukeni kumchukia mtu ambae kiuhalisia yupo kinadharia zaidi, maana kuna baadhi ya watu wanachangia kama mademu kumbe midume, kuna mafukara wanaojifanya matajiri. Kwa kifupi kumchukia mtu wa JF ni sawa na kumchukia actor anaeigiza kama adui kwenye movie, ni maigizo tu.
Katika point hiyo hiyo, kuna baadhi ya watu wanatafuta kuchukiwa kwa makusudi ili iwe ndio umaarufu wao. Maana unaweza kuta jitu linatukana tu pasi na sababu za msingi.
Kama vile baadhi tunavyofanya JF kuwa sehemu ya kupoteza muda, kuna wengine ndio sehemu pekee uwepo wao unatambulika hata ukiwa ni kwa jina la uongo. Ili kujipa thamani ya nafsi yake (validation and self-worth) ndio unakuta anaanzisha maugomvi yasiyo na tija. Ukichunguza walio wagomvi wengi humu utakuta maisha yao halisi yamejaa upweke na jitimai.