Watu wanapitia manyanyaso kwenye ajira

Watu wanapitia manyanyaso kwenye ajira

Katika maisha yangu kumuita mtu Boss siwezi , Vyeti vyangu vipo vinaliwa na panya 😃 .

kuajiriwa sio kubaya na sio kila mtu ana misuli ya kujiajiri lakini nafahamu waajiriwa wanapitia manyanyaso mengi maofisini na sikuhizi kupata promotion hata uwe na sifa haupati watu wanapeana kwa connection ina discourage sana. Kama unauwezo wa kujiajiri i recommend you to do that
Bora ajiraaaa

Uskgusee ñdoaa mkuu kama badooo

Ukipigwa na vyote viwili utakufa
 
Kuajiriwa kunataka uwe na roho ngumu ya kuvumilia madhila utakayokumbana na huko kazini kutoka kwa Boss wako au workmates wako.
 
Katika casual talks amuezi kumsema vizuri boss wenu sometime ile critique ina mfanya boss kua unsecured, kuna siku naenda kazini nakuta ofisi imefungwa hamna mtu, kumbe walienda field wote ila mimi sina taarifa na boss alifanya makusudi kuniumiza, nili kaa wiki mbili bila ratiba au kazi mwezi huo mshahara nili pokea nusu ila si ku-mind nili sema poa tu...... mimi siwezi kuishi kinafiki na watu kamwee siwezi kuajiriwa tena labda iwe political post kama mkuu wa mkoa au wilaya, au ni ajiliwe na UN, ila kwa hao waswahili wetu hapana, bora nifanye umachinga wangu,.... usipo kua na Imani ya Dini unajikuta umeanza ushirkina ili upendwe kazini loh.
Boss,nakubaliana na mchango wako, lakin kwenye hili la watu kwenda field wote ofisi nzima, afu huna taarifa yani ukiachilia mbali Boss wako kukupa taatifa, hata work mates wako wote hukua na mshakaji wako hata mmoja walau ambae atakua anakumegea mambo yanavyoenda??
au nawewe una ka ujuaji flani maana kwenye kundi la watu hata kama unajua usijifanye mjuaji saaana otherwise watu wanaanza kukupangusa
 
Heshima ni muhimu sanaa kwa vitendo na maneno kumièeèita mtu boss upungukiwi chochote,....kuna taasisi moja ni lienda boss wao alikua padri, ila akiingia kwenye staffroom wote mnasimama kwanza mnatoa salamu na kukaa badaye. Mimi binsfsi hilo sio tatizo, tatizo ni pale ukianza kunionea bila issue ya maana.
Mimi sifanyi hivyo na siwezi.
 
Ni lazima umwite aliyekuajiri boss? Nakumbuka hata walimu shule tuliwatungia majina kujiridhisha nafsi.
Kuna Madame mmoja tulikuwa tunamuita anopheles ili kujifurahisha mana alikuwa jau sana 😹😹😹
 
Kwangu sina ukweli kuhusu kazi za kuajiriwa, I mean sina kazi. Ila nahisi uvumilivu, hekima, busara, utii na nidhamu ni nguzo tosha za kulinda kazi yako haijalishi BOSS atakuwa na roho gani kuna siku mungu atatia ukuu wake lazima uonekane. Lazima ubembeleze kinachokupa riziki kwani kuna wengi wanahitaji hiyo nafasi uliyoipata wewe, Lasivyo usipoweza kuvifanya hivyo utaonekana una kiburi cha uvivu.🙏🏾🙏🏾🙏🏾
 
Back
Top Bottom