Watu wanasema mimi ni nani? Swali alilouliza Yesu linalofungua ubongo wa mwanadamu kujitambua

Wivu wq kila kitu unao

Ndio mafundisho ya kanisa hayo ??

Sasa tuambie huyu aliyesema maneno haya uliyoyaleta ni nani ??


Luka 9:18-21 "Yesu aliwauliza wanafunzi wake kua je makutano hao wanasema ya kua mimi ni nani? Wanafunzi wake wakajibu yohana mbatizaji wengine wanasema wewe ni Eliya lakini petro akamjibu kua Ndiwe Kristo wa Mungu"
 
Bila uvumbuzi wa Copy n Paste maisha yako yangekua vipi.?
 
Ila mi ni muovu hadi siwezi jiuliza swali la hivyo.
 
Luka 9:18-21 "Yesu aliwauliza wanafunzi wake kua je makutano hao wanasema ya kua mimi ni nani? Wanafunzi wake wakajibu yohana mbatizaji wengine wanasema wewe ni Eliya lakini petro akamjibu kua Ndiwe Kristo wa Mungu".

Kumbe yesu ni kristo wa mungu?

Kristo wa mungu vs mungu

Nani muumba hapa???

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wapendwa kwa muda huu wa kukaa nyumba ni baada ya kazi, soma ujumbe mzuri toka kwa Bwn Yesu.
Utapata nondo na madini aliyomwaga ili mtambue kuwa yeye ni mwana wa Mungu aliye hai.
Yohn: 7: 1~33
The whole chapter.
Yohn : 8:1-59
The whole chapter.
Tuliza akili muombe Mungu akupe ufunuo wa kweli nayo kweli itakuweka huru!!

Thanks Da Vinci.
Kiranga, Graph and CO. see the truth through Jesus the Lord.
 
Mlango 7
1 Na baada ya hayo Yesu alikuwa akitembea katika Galilaya; maana hakutaka kutembea katika Uyahudi, kwa sababu Wayahudi walikuwa wakitafuta kumwua.
2 Na sikukuu ya Wayahudi, Sikukuu ya Vibanda, ilikuwa karibu.
3 Basi ndugu zake wakamwambia, Ondoka hapa, uende Uyahudi, wanafunzi wako nao wapate kuzitazama kazi zako unazozifanya.
4 Kwa maana hakuna mtu afanyaye neno kwa siri, naye mwenyewe ataka kujulikana. Ukifanya mambo haya, basi jidhihirishe kwa ulimwengu.
5 Maana hata nduguze hawakumwamini.
6 Basi Yesu akawaambia, Haujafika bado wakati wangu; ila wakati wenu sikuzote upo.
7 Ulimwengu hauwezi kuwachukia ninyi; bali hunichukia mimi, kwa sababu mimi naushuhudia ya kuwa kazi zake ni mbovu.
8 Kweeni ninyi kwenda kula sikukuu; mimi sikwei bado kwenda kula sikukuu hii, kwa kuwa haujatimia wakati wangu.
9 Naye alipokwisha kuwaambia hayo, alikaa vivi hivi huko Galilaya.Yesu katika Sikukuu ya Vibanda
10 Hata ndugu zake walipokwisha kukwea kuiendea sikukuu, ndipo yeye naye alipokwea, si kwa wazi bali kana kwamba kwa siri.
11 Basi Wayahudi wakamtafuta kwenye sikukuu, wakasema, Yuko wapi yule?
12 Kukawa na manung?uniko mengi katika makutano juu yake. Wengine wakasema, Ni mtu mwema. Na wengine wakasema, Sivyo; bali anawadanganya makutano.
13 Walakini hakuna mtu aliyemtaja waziwazi, kwa sababu ya kuwaogopa Wayahudi.
14 Hata ikawa katikati ya sikukuu Yesu alikwea kuingia hekaluni, akafundisha.
15 Wayahudi wakastaajabu wakisema, Amepataje huyu kujua elimu, ambaye hakusoma?
16 Basi Yesu akawajibu, akasema, Mafunzo yangu si yangu mimi, ila ni yake yeye aliyenipeleka.
17 Mtu akipenda kuyatenda mapenzi yake, atajua habari ya yale mafunzo, kwamba yatoka kwa Mungu, au kwamba mimi nanena kwa nafsi yangu tu.
18 Yeye anenaye kwa nafsi yake tu hutafuta utukufu wake mwenyewe; bali yeye anayetafuta utukufu wake aliyempeleka, huyo ni wa kweli, wala ndani yake hamna udhalimu.
19 Je! Musa hakuwapa torati? Wala hakuna mmoja wenu aitendaye torati. Mbona mnatafuta kuniua?
20 Mkutano wakajibu, Ama! Una pepo! Ni nani anayetafuta kukuua?
21 Yesu akajibu, akawaambia, Mimi nalitenda kazi moja, nanyi nyote mnaistaajabia.
22 Musa aliwapa tohara; lakini si kwamba yatoka kwa Musa, bali kwa mababa; nanyi siku ya sabato humtahiri mtu.
23 Basi ikiwa mtu hupashwa tohara siku ya sabato, ili torati ya Musa isije ikavunjika, mbona mnanikasirikia mimi kwa sababu nalimfanya mtu kuwa mzima kabisa siku ya sabato?
24 Basi msihukumu hukumu ya macho tu, bali ifanyeni hukumu iliyo ya haki.Huyu ndiye Kristo?
25 Basi baadhi ya watu wa Yerusalemu wakasema, Je! Huyu siye wanayemtafuta ili wamwue?
26 Na kumbe! Anena waziwazi, wala hawamwambii neno! Yamkini hao wakuu wanajua hakika ya kuwa huyu ndiye Kristo?
27 Lakini huyu twamjua atokako; bali Kristo atakapokuja hakuna ajuaye atokako.
28 Basi Yesu akapaza sauti yake hekaluni, akifundisha na kusema, Mimi mnanijua, na huko nitokako mnakujua; wala sikuja kwa nafsi yangu; ila yeye aliyenipeleka ni wa kweli, msiyemjua ninyi.
29 Mimi namjua, kwa kuwa nimetoka kwake, naye ndiye aliyenituma.
30 Basi wakatafuta kumkamata; lakini hakuna mtu aliyeunyosha mkono wake ili kumshika, kwa sababu saa yake ilikuwa haijaja bado.
31 Na watu wengi katika mkutano wakamwamini; wakasema, Atakapokuja Kristo, je! Atafanya ishara nyingi zaidi kuliko hizi alizozifanya huyu?Maofisa Watumwa Kumkamata Yesu
32 Mafarisayo wakawasikia mkutano wakinung?unika hivi juu yake; basi wakuu wa makuhani na Mafarisayo wakatuma watumishi ili wamkamate.
33 Basi Yesu akasema, Bado kitambo kidogo nipo pamoja nanyi; kisha naenda zangu kwake yeye aliyenipeleka.
34 Mtanitafuta wala hamtaniona; nami nilipo ninyi hamwezi kuja.
 
Mlango 8
1 [Walikwenda kila mtu nyumbani kwake; naye Yesu akaenda mpaka mlima wa Mizeituni.
2 Hata asubuhi kulipokucha akaingia tena hekaluni, na watu wote wakamwendea; naye akaketi, akawa akiwafundisha.
3 Waandishi na Mafarisayo wakamletea mwanamke aliyefumaniwa katika uzinzi, wakamweka katikati.
4 Wakamwambia, Mwalimu, mwanamke huyu amefumaniwa alipokuwa akizini.
5 Basi katika torati, Musa alituamuru kuwapiga kwa mawe wanawake namna hii; nawe wasemaje?
6 Nao wakasema neno hilo wakimjaribu, ili wapate sababu ya kumshitaki. Lakini Yesu akainama, akaandika kwa kidole chake katika nchi.
7 Nao walipozidi kumhoji, alijiinua, akawaambia, Yeye asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza wa kumtupia jiwe.
8 Akainama tena, akaandika kwa kidole chake katika nchi.
9 Nao waliposikia, wakashitakiwa na dhamiri zao, wakatoka mmoja mmoja, wakianzia tangu wazee hata wa mwisho wao; akabaki Yesu peke yake, na yule mwanamke amesimama katikati.
10 Yesu akajiinua asimwone mtu ila yule mwanamke, akamwambia, Mwanamke, wako wapi wale washitaki wako? Je! Hakuna aliyekuhukumu kuwa na hatia?
11 Akamwambia, Hakuna, Bwana. Yesu akamwambia, Wala mimi sikuhukumu. Enenda zako; wala usitende dhambi tena.]Yesu Nuru ya Ulimwengu
12 Basi Yesu akawaambia tena akasema, Mimi ndimi nuru ya ulimwengu, yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima.
13 Basi Mafarisayo wakamwambia, Wewe unajishuhudia mwenyewe; ushuhuda wako si kweli.
14 Yesu akajibu, akawaambia, Mimi ningawa ninajishuhudia mwenyewe, ushuhuda wangu ndio kweli; kwa sababu najua nilikotoka na niendako; lakini ninyi hamjui nilikotoka wala niendako.
15 Ninyi mwahukumu kwa kufuata mambo ya mwili; mimi simhukumu mtu.
16 Nami nijapohukumu, hukumu yangu ni kweli; kwa kuwa mimi si peke yangu, bali ni mimi na yeye aliyenipeleka.
17 Tena katika torati yenu imeandikwa kwamba, Ushuhuda wa watu wawili ni kweli.
18 Mimi ndimi ninayejishuhudia mwenyewe, naye Baba aliyenipeleka ananishuhudia.
19 Basi wakamwambia, Yuko wapi Baba yako? Yesu akajibu, Mimi hamnijui, wala Baba yangu hammjui; kama mngalinijua mimi, mngalimjua na Baba yangu.
20 Maneno hayo aliyasema alipokuwa akifundisha hekaluni, katika chumba cha hazina; wala hakuna mtu aliyemkamata, kwa sababu saa yake ilikuwa haijaja bado.Yesu Atabiri kuhusu Kifo chake
21 Basi akawaambia tena, Mimi naondoka, nanyi mtanitafuta; nanyi mtakufa katika dhambi yenu; mimi niendako ninyi hamwezi kuja.
22 Basi Wayahudi wakasema, Je! Atajiua! Kwa kuwa asema, Mimi niendako ninyi hamwezi kuja?
23 Akawaambia, Ninyi ni wa chini, mimi ni wa juu; ninyi ni wa ulimwengu huu, mimi si wa ulimwengu huu.
24 Kwa hiyo naliwaambieni ya kwamba mtakufa katika dhambi zenu; kwa sababu msiposadiki ya kuwa mimi ndiye, mtakufa katika dhambi zenu.
25 Basi wakamwambia, U nani wewe? Yesu akawaambia, Hasa neno lilo hilo ninalowaambia.
26 Ninayo mengi ya kusema na kuhukumu juu yenu; lakini yeye aliyenipeleka ni kweli, nami niliyoyasikia kwake, ndiyo ninenayo katika ulimwengu.
27 Wala hawakutambua ya kuwa anawatajia Baba.
28 Basi Yesu akawaambia, Mtakapokuwa mmekwisha kumwinua Mwana wa Adamu, ndipo mtakapofahamu ya kuwa mimi ndiye; na ya kuwa sifanyi neno kwa nafsi yangu, ila kama Baba alivyonifundisha ndivyo ninenavyo.
29 Naye aliyenipeleka yu pamoja nami, hakuniacha peke yangu; kwa sababu nafanya sikuzote yale yampendezayo.
30 Naye alipokuwa akisema hayo, wengi walimwamini.Wanafunzi wa Kweli
31 Basi Yesu akawaambia wale Wayahudi waliomwamini, Ninyi mkikaa katika neno langu, mmekuwa wanafunzi wangu kweli kweli;
32 tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru.
33 Wakamjibu, Sisi tu uzao wake Ibrahimu, wala hatujawa watumwa wa mtu wakati wo wote; nawe wasemaje, Mtawekwa huru?
34 Yesu akawajibu, Amin, amin, nawaambia, Kila atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi.
35 Wala mtumwa hakai nyumbani sikuzote; mwana hukaa sikuzote.
36 Basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli.
37 Najua ya kuwa ninyi ni uzao wa Ibrahimu lakini mnatafuta kuniua kwa sababu neno langu halimo ndani yenu.
38 Niliyoyaona kwa Baba ndiyo niyanenayo; nanyi vivyo hivyo mliyoyasikia kwa baba yenu ndiyo myatendayo.Yesu na Abrahamu
39 Wakajibu, wakamwambia, Baba yetu ndiye Ibrahimu! Yesu akawaambia, Kama mngekuwa watoto wa Ibrahimu, mngezitenda kazi zake Ibrahimu.
40 Lakini sasa mnatafuta kuniua mimi, mtu ambaye nimewaambia iliyo kweli, niliyoisikia kwa Mungu. Ibrahimu hakufanya hivyo.
41 Ninyi mnazitenda kazi za baba yenu. Ndipo walipomwambia, Sisi hatukuzaliwa kwa zinaa; sisi tunaye Baba mmoja, yaani, Mungu.
42 Yesu akawaambia, Kama Mungu angekuwa baba yenu, mngenipenda mimi; kwa maana nalitoka kwa Mungu, nami nimekuja; wala sikuja kwa nafsi yangu, bali yeye ndiye aliyenituma.
43 Mbona hamyafahamu hayo niyasemayo? Ni kwa sababu ninyi hamwezi kulisikia neno langu.
44 Ninyi ni wa baba yenu, Ibilisi, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzitenda. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo; wala hakusimama katika kweli, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake. Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe; kwa sababu yeye ni mwongo, na baba wa huo.
45 Nami, kwa sababu nasema iliyo kweli, hamnisadiki.
46 Ni nani miongoni mwenu anishuhudiaye ya kuwa nina dhambi? Nami nikisema kweli, mbona ninyi hamnisadiki?
47 Yeye aliye wa Mungu huyasikia maneno ya Mungu; hivyo ninyi hamsikii kwa sababu ninyi si wa Mungu.
48 Wayahudi wakajibu, wakamwambia, Je! Sisi hatusemi vema ya kwamba wewe u Msamaria, nawe una pepo?
49 Yesu akajibu, Mimi sina pepo; lakini mimi namheshimu Baba yangu, na ninyi mwanivunjia heshima yangu.
50 Wala mimi siutafuti utukufu wangu; yuko mwenye kutafuta na kuhukumu.
51 Amin, amin, nawaambia, Mtu akilishika neno langu, hataona mauti milele.
52 Basi Wayahudi wakamwambia, Sasa tumeng?amua ya kuwa una pepo. Ibrahimu amekufa, na manabii wamekufa; nawe wasema, Mtu akilishika neno langu, hataonja mauti milele.
53 Wewe u mkuu kuliko baba yetu Ibrahimu, ambaye amekufa? Nao manabii wamekufa. Wajifanya u nani?
54 Yesu akajibu, Nikijitukuza mwenyewe, utukufu wangu si kitu; anitukuzaye ni Baba yangu, ambaye ninyi mwanena kuwa ni Mungu wenu.
55 Wala ninyi hamkumjua; lakini mimi namjua. Nikisema ya kwamba simjui, nitakuwa mwongo kama ninyi; lakini namjua, na neno lake nalishika.
56 Ibrahimu, baba yenu, alishangilia kwa vile atakavyoiona siku yangu; naye akaiona, akafurahi.
57 Basi Wayahudi wakamwambia, Wewe hujapata bado miaka hamsini, nawe umemwona Ibrahimu?
58 Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Yeye Ibrahimu asijakuwako, mimi niko.
59 Basi wakaokota mawe ili wamtupie; lakini Yesu akajificha, akatoka hekaluni.
 
Meaning of great thinker

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante Kwa Somo Zuri Nimelipenda Mungu Anisaidie Kujitambua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…