Watu wanasema mimi ni nani? Swali alilouliza Yesu linalofungua ubongo wa mwanadamu kujitambua

Watu wanasema mimi ni nani? Swali alilouliza Yesu linalofungua ubongo wa mwanadamu kujitambua

Mim ni Andunje bilionea kutoka Bunju mwenye kipara
Hadi leo sijui biblia ni gazeti au jarida gani....huu ni mwaka wa kumi sijagusa kanisa wala msikiti na sitegemei kwenda labda nikiwa mfu
Mimi ni mfupi,mwenye pesa na mpenda starehe
Mimi niko hapa bunju miaka yote na sikufahamu ingawa unapesa. Pole mr[emoji2] [emoji2] [emoji2]
 
Watu wengi ukiwauliza Hilo swali atakujibu Mimi ni Aisha John Mpambalyanga ,mjukuu wa Thabiti.
Kimsingi mtu SI JINA LAKE!!
ndio maana tuna Aisha wengi duniani,au tuna Aisha John wengi vile vile!!
Na bado wao SIO mtu mmoja!!

Miongoni mwa tafsiri ya jina namna TU ya kurahisisha uitaji na uitikaji!!
Kwenye nadharia za lugha, tunasema majina hurejelea tu kifaa fulani!!
Ndio maana kifaa cha kusafisha meno kinaitwa mswaki kwa kiswahili na kiingereza kinaitwa toothbrush,kichina wanakiita vingine
nadhariaa ,
Hii ni kusema kitu/mtu CHOCHOTE/YEYOTE kinaweza/anaweza kuitwa VYOVYOTE.
Umenikumbusha hadithi fulani ya zamani
Ndugu mmoja mswahili alienda china kwa mambo yake. Wakati mmoja alienda mgahawani na kuagiza chai
Kumbe ile chai haikukolea sukari. Sasa alishindwa namna ya kuomba aongezewe sukari akamwita mhudumu na kumwambia chai chungu kumbe chai chungu ndio jina la huyo mhudumu.
 
Hii chai nayo chungu
 
Naomba mnisaidie kumjua huyo mtu aliyetunga habari za Yesu mnazareti,kwani uwezo wake haukua wa kibinaadamu,hivi aliwezaje kutunga hadithi ya Mtu mkamilifu vile,ambae aliishi kwa uwezo wa ajabu,nisaidieni nimjue mtu huyo ili nimwabudu Mungu kupitia yeye,na hata kama Mungu hayupo nimwabudu huyo kwa hadithi yake ya ajabu ya kisa cha Yesu aliyemwita mwana wa Mungu aliye juu.
mugu yupo lakini sio yesu wa kwenye biblia
wazungu waligeuza maisha ya mtu aliyeitwa yeshua hamashiach na kuweka upuuzi wao
mungu hajawahi kuongea na mtu(at least super natural power ninayoamini ipo)
jiulize kabla hawa washenzi hawajaja kututawala hatukuwa na imani zetu!!!!
achana na upuuzi wa biblia na quran,kuna contradictions nyingi sana
wazungu walivumbua sayansi lakini kwenye spirituality walifeli
 
Kwanini yeye unapinga hakuwepo lakini socrate alikuwepo???
kuna vitabu vya wanahistoria na waandishi kipindi hicho waliandika kuhusu yeye ingawaje walidanganya kuhusu elimu yake
hawakusema kuwa walifundishwa na wamisri hizo wanazoita falsafa zao(lakini the fact is they existed)
jesus hakuna historia yake zaidi ya biblia
 
Naam ndio maana yesu atabaki kua mwanafalsafa namba moja ulimwenguni na hakuna atakaye vunja hio rekodi

Unao ushahidi yesu aliyasema hayo maneno au unafuata msafara Tu ??
 
Supper Human.
Ni nyanja ambayo watu wengi hawaijui au hawajaifikia.
Walioifikia ni lazima wanajiuliza maswali kama.
Mimi ni nani ?
Kwanini nipo ?
Natakiwa niishi vipi ?
Na kwanini ?
Hatima yangu ni nini ?
Nani kanifanya niwe ?
Anataka nini kwangu ?
Kwanini ?
Kwa sasa natakiwa kufanya nini ?
Kwanini ?

Herode alipo mwuliza Yesu Kristo swali la.
KWELI ni nini ?

Yesu alinyamaza na hakumjibu, na hilo ndilo jibu alilostahili Herode kwasababu kuu tatu.

1. KWELI ni dhana mtambuka, kila mtu ana kweli yake kwa mfano, kuna watu wanasema Muhammadi ni Mtume wa KWELI wengine wanakanusha huo ukweli.
2. KWELI huwa inabadilikabadilika kutokana na mazingira yanayokuwepo. Mfano dawa ya Quinine ilikuwa inatibu KWELI ugonjwa wa Maralia kipindi fulani lakini kwa sasa dawa hiyo haitibu tena ugonjwa huo kama hapo awali, hivyo sio dawa ya UKWELI ya Maralia kwa sasa, kama hapo zamani.

3. Herode hakuwa Supper Human,
alikuwa ni Simple Human, mtu wa kawaida ambaye ni kati ya watu ambao hawajawahi kujiuliza na kuyafanyia kazi maswali ya hapo juu.
Wao wapo wapo tu ilimradi kumekucha wanaenda kufanya kazi ili wapate chakula, mavazi na malazi na kuweka akiba benki basi siku imekwisha, wanasubira kesho kufanya mambo hayohayo tena.
Pamoja kuna usemi kwamba binadamu wote ni sawa, lakini usawa huo upo kwenye maumbile tu, ila sio katika kujitambua.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huu uzi ukisoma bila kutafakari unaweza ukauchukulia wa kawaida ila kiukweli una ujumbe mzito sana hongera kiongozi kwa hilo

Wewe ni nani .? ni swali rahisi ila ukiuliza watu hilo swali nina uhakika majibu ya walio wengi watasema kwa kujibu mimi ni mtu nilieumbwa na mungu ukiona mtu amejibu hivyo ujue amejibu asilmia 30 ya jibu yaan hata nusu hajafika

Somo lako zuri na nimelipenda sana japokuwa ktk reference zako mimi huko sipo siziitaji siamini uwepo wa mungu hakuna mungu hayo mafundisho nakuachia

"ufanyeni mti kuwa mzuri na matunda yake kuwa mazuri au ufanyeni mti kuwa mbaya na matunda yake kuwa mabaya kwa maana kwa matunda yake mti utatambulikana" mathayo 12:33
 
Mwanzo hilo swali niliulizwa nikashindwa kulijibu kabisa japo nililiona ni rahisi sana..
 
Mwanzo hilo swali niliulizwa nikashindwa kulijibu kabisa japo nililiona ni rahisi sana..

Mimi hilo swali niliulizwa kwa mara ya kwanza mwaka 2013 nikajibu kama watavyojibu wengi akaniambia ingekuwa mtihani ningekupa 30 ya mia

Ukiweza kujibu vzr na ukaelewa wewe ni nani katika dunia na nafasi yako ipi unakuwa upo katika ulimwengu mwingine wenye hekima na ustarabu ulumwengu wa fair

Wengi hatujui hilo ndio maana usijekutegemea siku moja dunia kuwe na amani kwakuwa walio wengi hawajitambui wapo wapo
 
Back
Top Bottom