Nusura siku moja nivunje simu ya Pisi kali moja, Baba yake alituliza ghasia
Ilikuwa hivi, nipo zangu kiwanja nimekula kilaji nikaanza kuruka majoka
nikaona bint mmoja akinirekodi, nikamfuata na kumnyang’anya ile simu!
Washikaji niliokuwa nao wakaungana namimi kuzisaka zile picha wakazikuta snapchat wakafuta, tukamwambia tunavunja kumbe alikuwa na baba yake, na ndugu zake wengine akajitetea alikuwa akimrekodi huyo mzee wake lakini ndani tulipata amerekodi video zetu!
Basi tukataka kuivunja, mzee akatusihi tusivunje tukarestore na kufuta kila kitu ikawa ndio adhabu yake!
Yule mzee nikabadilishana nae namba baada ya lile tukio akutuachia na kilaji kaunta akasepa!
Sasa hivi yule mzee ni rafiki yangu, mara nyingi weekend ilifika kama muda upo hunipigia simu tunaenda kula kilaji!
Ile pisi kali mtoto wa mzee ushamba ushamtoka, na mara kadhaa mimi na yeye tunatoka tunaenda kuruka majoka!