Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Wanaharakati wa haki za binadamu na wanachama wa CHADEMA wamekuwa wakipaza sauti kupitia X kijana wao Deusdedith Soka kuchukuliwa na wanaosemekana na polisi na mpaka sasa hajulikani alipo.
Vijana wengine kutoka CHADEMA ambao ambao hawajulikani walipo baada ya sekeseke la maandamano ya BAVICHA ni Jacob Mlay na Frank Mbise.
Malisa ameandika haya;
Leo ni siku ya 5 vijana watatu wa Chadema wanaodaiwa kutekwa huko Temeke hawajulikani walipo. Deus Soka, Jacob Mlay na Frank Mbise.
Siku ya tukio Soka alipigiwa simu na mtu aliyejitambulisha ni Askari akimtaka afike polisi Chang'ombe kwa utambuzi wa pikipiki yake iliyoibiwa mwaka 2023.
Soka alikua anamiliki pikipiki, akampa mshkaji wake Frank Mbise aendeshe, lakini ikaibiwa. Wakatoa taarifa Polisi Chang'ombe ambapo lilifunguliwa jalada la uchunguzi.
Pia soma: Kuelekea 2025 - CHADEMA yadai Viongozi wake Wilayani Temeke wameshikiliwa, Polisi wakana
Kwahiyo alipopigiwa simu kwamba pikipiki imepatikana ilikua habari njema. Akamjulisha Frank waende pamoja maana ndiye aliyekua na pikipiki wakati inaibiwa. Akampigia pia Katibu wa Chadema Wilaya ya Temeke, Jacob Mlay kumjulisha kuhusu wito wa Polisi. Mlay akamshauri waende pamoja. Kwahiyo ikawa timu ya watu watatu; Deus Soka, Frank Mbise na Jacob Mlay.
Wakiwa wanaelekea kituoni kupanda gari ilitokea Noah nyuma yao. Ghafla wakatoka watu wenye silaha na kuwaamuru kuingia. Kabla hawajafanya lolote wakaporwa simu zao na kisha gari ikaondolewa kwa kasi.
Baadhi ya Mashuhuda wanasema waliona vijana watatu wanatembea na ghafla ikaja Noah wakatoka watu wenye makoti, kisha wale vijana wakaingia ndani. Hawakuelewa kama lilikua tukio la utekaji.
Taarifa imetolewa Polisi lakini wamekanusha kuwashikilia na wamekanusha kumpigia simu Soka akafuate pikipiki yake.
Lakini familia haina imani na Polisi kwa sababu, Polisi walikanusha kumshikilia Kombo Mbwana, lakini baada ya siku 29 wakakiri yupo mikononi mwao. Pia ni Polisi haohao waliokanusha kumshikilia Robert Mushi lakini baada ya siku 10 mwili wake ukakutwa hospitali ya Polisi Kilwa Road.
Familia ya Soka inadai ndugu yao amekua akipokea vitisho kutoka kwenye vyombo vya Dola. Tar 10 August vijana wa Chadema Temeke walikamatwa wakielekea Mbeya kwenye kongamano la Bavicha, wakapelekwa kituo cha Polisi Chang'ombe, lakini Soka alipelekwa Kilwa Road. Tar.12 Soka alitolewa Kilwa Road na kupelekwa Chang'ombe ili akapewe dhamana pamoja na wenzie.
Soka aliwaeleza ndugu zake kwamba akiwa kwenye gari la Polisi kutoka Kilwa Road kwenda Chang'ombe, askari mmoja mwenye marasta alimwambia "muda si mrefu tutamalizana na wewe mazima."