Pre GE2025 Watu Wasiojulikana: Malisa aelezea tukio la kutekwa kwa Deus Soka na vijana wengine wawili wa CHADEMA

Pre GE2025 Watu Wasiojulikana: Malisa aelezea tukio la kutekwa kwa Deus Soka na vijana wengine wawili wa CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Labda walikuwa wanatembea na wake za watu, jamaa wameamua kulipiza. Vijana wanapenda sana mashangazi

Sasa kama walitekwa, hii story umesimuliwa na nani? Maana walio experience hili jambo hawapo.

Halafu suala la ajenda za nchi, usijiweke mbele, subiri mifumo yenyewe iji-set. Jamii yenyewe huwa inajiivisha, na inakuwa tayari kwa mabadiliko. Ndio maana kwa Tanzania, mnataka watu waandamane, kwanza watu wenyewe wanawashangaa. Mnasema sijui katiba mpya, jamii kwa ujumla haijafikia hatua ya kuihitaji as long as serikali haiiwekei makucha jamii hiyo kwa ujumla wake, ukiacha wake wenye akili zilizopiga shoti kama Mdude Nyagali. Hawa lazima wapate mikwaruzo, kwa kuwa wanatembea kwenye eneo lenye umeme mkubwa.
Comment yako imeshiba sana. Mwenye kuelewa na aelewe
 
Wanaharakati wa haki za binadamu na wanachama wa CHADEMA wamekuwa wakipaza sauti kupitia X kijana wao Deusdedith Soka kuchukuliwa na wanaosemekana na polisi na mpaka sasa hajulikani alipo.

Vijana wengine kutoka CHADEMA ambao ambao hawajulikani walipo baada ya sekeseke la maandamano ya BAVICHA ni Jacob Mlay na Frank Mbise.

Malisa ameandika haya;

Leo ni siku ya 5 vijana watatu wa Chadema wanaodaiwa kutekwa huko Temeke hawajulikani walipo. Deus Soka, Jacob Mlay na Frank Mbise.

Siku ya tukio Soka alipigiwa simu na mtu aliyejitambulisha ni Askari akimtaka afike polisi Chang'ombe kwa utambuzi wa pikipiki yake iliyoibiwa mwaka 2023.

Soka alikua anamiliki pikipiki, akampa mshkaji wake Frank Mbise aendeshe, lakini ikaibiwa. Wakatoa taarifa Polisi Chang'ombe ambapo lilifunguliwa jalada la uchunguzi.

Pia soma: Kuelekea 2025 - CHADEMA yadai Viongozi wake Wilayani Temeke wameshikiliwa, Polisi wakana

Kwahiyo alipopigiwa simu kwamba pikipiki imepatikana ilikua habari njema. Akamjulisha Frank waende pamoja maana ndiye aliyekua na pikipiki wakati inaibiwa. Akampigia pia Katibu wa Chadema Wilaya ya Temeke, Jacob Mlay kumjulisha kuhusu wito wa Polisi. Mlay akamshauri waende pamoja. Kwahiyo ikawa timu ya watu watatu; Deus Soka, Frank Mbise na Jacob Mlay.

Wakiwa wanaelekea kituoni kupanda gari ilitokea Noah nyuma yao. Ghafla wakatoka watu wenye silaha na kuwaamuru kuingia. Kabla hawajafanya lolote wakaporwa simu zao na kisha gari ikaondolewa kwa kasi.

Baadhi ya Mashuhuda wanasema waliona vijana watatu wanatembea na ghafla ikaja Noah wakatoka watu wenye makoti, kisha wale vijana wakaingia ndani. Hawakuelewa kama lilikua tukio la utekaji.

Taarifa imetolewa Polisi lakini wamekanusha kuwashikilia na wamekanusha kumpigia simu Soka akafuate pikipiki yake.

Lakini familia haina imani na Polisi kwa sababu, Polisi walikanusha kumshikilia Kombo Mbwana, lakini baada ya siku 29 wakakiri yupo mikononi mwao. Pia ni Polisi haohao waliokanusha kumshikilia Robert Mushi lakini baada ya siku 10 mwili wake ukakutwa hospitali ya Polisi Kilwa Road.

Familia ya Soka inadai ndugu yao amekua akipokea vitisho kutoka kwenye vyombo vya Dola. Tar 10 August vijana wa Chadema Temeke walikamatwa wakielekea Mbeya kwenye kongamano la Bavicha, wakapelekwa kituo cha Polisi Chang'ombe, lakini Soka alipelekwa Kilwa Road. Tar.12 Soka alitolewa Kilwa Road na kupelekwa Chang'ombe ili akapewe dhamana pamoja na wenzie.

Soka aliwaeleza ndugu zake kwamba akiwa kwenye gari la Polisi kutoka Kilwa Road kwenda Chang'ombe, askari mmoja mwenye marasta alimwambia "muda si mrefu tutamalizana na wewe mazima."
"Binadamu anaangalia maslahi yake, ukiitwa kupambana hakikisha una mgao wako unaolingana na viungo utakavyopoteza au kifo." Tsh

Sijui kama Deusdedith Soka alikwisha pata masilahi ya kutosha kabla ya kuingia kwenye hizi harakati. Otherwise ataacha machungu tu kwa ndugu zake.

Harakati awaachie akina Martin Maranja Masese, Boniface Jacob etc ambao wamejipanga. Wale hawatekwi kibwege
 
Hahaha, naona umeamua mpaka somo lieleweke.
 
Soka aliwaeleza ndugu zake kwamba akiwa kwenye gari la Polisi kutoka Kilwa Road kwenda Chang'ombe, askari mmoja mwenye marasta alimwambia "muda si mrefu tutamalizana na wewe mazima."
Duh,

'Failed states' huwa zinaanza hivihivi.

Wale waliotarajiwa kuwa walinzi wa umma na mali zao wanajigeuza kimya kimya kuwa wahalifu, majambazi, wauaji, nk dhidi ya umma.

Taratibu taratibu hii awamu ya 6 imekuwa ya ajabu na hovyo sana sana!!!
Lucas Mwashambwa
 
"Binadamu anaangalia maslahi yake, ukiitwa kupambana hakikisha una mgao wako unaolingana na viungo utakavyopoteza au kifo." Tsh

Sijui kama Deusdedith Soka alikwisha pata masilahi ya kutosha kabla ya kuingia kwenye hizi harakati. Otherwise ataacha machungu tu kwa ndugu zake.

Harakati awaachie akina Martin Maranja Masese, Boniface Jacob etc ambao wamejipanga. Wale hawatekwi kibwege
Stuxnet wakati wa Hayati Magufuli ulionekana wa maana sana ukipinga mambo kama haya.

Sasa ni wakati wenu unafurahia mambo yale yale uliyochukia kwa Hayati.
 
Mzee mmoja alipata kuniambia mambo matatu ya kuchunga maishani kuepuka matatizo yanayo epukika
1. Tii mamlaka (serikali)
2.Ishi VIZURI na watu/ jamii inayo kuzunguka ishi nao vyema.
3.Heshimu/ wapende wazazi,familia,ukoo na nduguzo

NB.
Maaskari Wengi ni watu wa kupokea maelekezo kutoka juu na hutakiwi kuhoji maana ITS AN ORDER AND NOT A REQUEST
Mzee wa nchi gani?
 
'Failed states' huwa zinaanza hivihivi.
Wale wanaotarajiwa kuwa walinzi wa umma na mali zao wanajigeuza kimya kimya kuwa wahalifu, majambazi, wauaji dhidi ya umma.

Taratibu taratibu hii awamu ya 6 imekuwa ya ajabu na hovyo sana sana!!!
Lucas Mwashambwa
Na mwisho wanakuwaga wanapindua nchi.....inaanza taratibu
 
Hao watakuwa Kituoni mbona wanahojiana nao kuhusu ile jinai ya Mbeya.
 
Stuxnet wakati wa Hayati Magufuli ulionekana wa maana sana ukipinga mambo kama haya.

Sasa ni wakati wenu unafurahia mambo yale yale uliyochukia kwa Hayati.
Magufuli ni tofauti na Samia. Magufuli alimiliki yeye mwenyewe binafsi kundi la WASIOJULIKANA. Hawa watekaji wa sasa hivi ni athari zitokanazo na ushenzi alioanzisha Mwendazake na jamii yenyewe ya Watanzania. Utekaji, mauaji ya albino, mauaji ya vikongwe, ubakaji watoto ni vitu vinavyotokana na uozo wa jamii yetu wenyewe wala siyo kazi ya Rais
 
Sasa mkuu mbona kama hujali athari hizo?
 
Wakati baba yake na Malisa akiwa Kamishna wa Magereza, wafungwa walitumika sana kumlimia mashamba yake binafsi
Wewe ni mpumbavu kabisa, Onel Malisa marehemu alikuwa kamishna mkuu wa magereza mtoto wake anaitwa Godlisten Onel Malisa ni diwani wa ccm kata ya minazi mirefu.

Unadandia dandia kwa kuungaunga vitu usivyovijuwa tutusa wahed.
 
Back
Top Bottom