Pre GE2025 Watu Wasiojulikana: Malisa aelezea tukio la kutekwa kwa Deus Soka na vijana wengine wawili wa CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Laanakum
 
🚮
 
akina @Martin Maranja Masese, Boniface Jacob etc ambao wamejipanga. Wale hawatekwi kibwege
Hizo mbinu za kusababisha kutotekwa kibwege zinafaa kujulikana kwa wengi ili watu wajue kujihami. Nchi imepoteza mwelekeo
 
Malisa ndio mwanzilishi wa mama anaupiga mwingi.
Tunafutwa machozi
😂 😂 😂
 
Sasa mkuu mbona kama hujali athari hizo?
Ninajali sana. Ndiyo maana nasema kama vijana wanaweza kuepuka "harakati za kushindana na Dola" bora wafanye hivyo.

Nimemfuatilia sana huyu kijana Deusdedith Soka. Amewahi kushikwa na Polisi zaidi ya mara 3. Kila akishikwa ni familia yake ndiyo ina suffer. Lakini wale mashabiki wa harakati wanamuona kama bingwa wao au shujaa.

Mtu kma huyu dogo anajidanganya tu kudhani anaweza kubadili mfumo wa dola. Hata hawa akina Mbowe ambao ni viongozi wa CHADEMA leo hii waliamza taratibu siyo kwa jeuri na kiburi kama cha huyu dogo.
 

Ukiwa kwenye siasa haitakiwi uamini mtu yeyote.....Mimi hata mtu nayemjua anipigie njoo na bla bla kibao siendi mpaka anieambie motive behind otherwise namwambia aongee tumalizane kwenye simu.

Mwamba alikuwa Zakaria alivyotaka kuwamwaga Ubongo wasiojulikana , watu wakija kukuchukua hakikisha hautoki kizembe othewise piga nduru umevamiwa na wezi(Unapiga yowe tu weziiii ,majirani weziiiiiii) raia watoke ,raia wakishajaa hata wakiwa na mitutu watasalenda.

Ukipigiwa simu na mtu akianza kukuuliza sijui upo wapi mara kuna issue inabidi tuongee tuiweke sawa mwambie direct aongee kwenye simu ukiona anang'ang'ania uko wapi mara tukutane jua hapo jamaa anapewa malekezo na manjagu stuka ,yeyusha tu kwamba upo bukoba kikazi na hauwezi kukutana nao kwa leo mpaka muda mwingine kama urgent waongee kwenye simuj.
 
Okay kumbe unamjua? Tuache huyo mwanaharakati na hao wengine vipi?

Na je huyo mwanaharakati yeye amevunja sheria gani?
 
Nchi hii watu wanataka kuwafanya vijana waanzishe makundi kama ya Mungiki kule Kenya wakati ule. Yalikuwa makundi ya kulipa visasi kwa wenye mamlaka wanaoyatumia vibaya kwa kutesa jamii.
Mfano huyo OCCID Mohamed Mirabo si anafahamika? Na pengine ana mke na watoto! Kwa akili zile za Mungiki alikuwa tayari kesha weka familia yake matatani. Mmenielewa.
Jee ndiko tunataka kuwapeleka vijana wetu waone hiyo ni njia sahihi kulipa visasi? Maana wamefikishwa point of NO RETURN
 
Hii mbinu yako itafanya kazi kama kweli ni vibaka wanaotaka kukuibia lakini sio Watekaji ambao wanakuja na Baraka zote kutoka juu.
 
Huwezi kuzuia 'mfumo asili' (nature) kwa mtutu wa bunduki.

Kama aina ya uongozi wa ccm haukubaliki tena na jamii hata watumie maguvu ya kila aina, lakini wataanguka tu...ni suala la muda.
 
Huwezi kuzuia 'mfumo asili' (nature) kwa mtutu wa bunduki.

Kama aina ya uongozi wa ccm haukubaliki tena na jamii hata watumie maguvu ya kila aina, lakini wataanguka tu...ni suala la muda.
Hatua ambayo ccm wamefikia ni Sawa na Kicks of Dying Horse
 
kwa mtiririko wa habari hii, Kwa 100% wahusika ni hawa 'wajomba'
Ila wajomba mmepoteza credibility yenu kabisa kwa UMMA wa wa Tanzania kwani mnatumika kwa maslahi ya wachache badala ya wananchi wote! siku zaja haya yatakuwa na mwisho!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…