Entim
JF-Expert Member
- Jun 7, 2013
- 4,025
- 2,261
kweli inauma sana, baada ya kifo huwa wanasiasa hutumia hiyo fursa kutafuta umaarufu. Huyo diwani naye nina mashaka naye katika utendaji wake, haiwezekani awe mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa kata halafu vibaka wanavamia mtaa wake kama shamba la bibi. issue ya vibaka ni hatari kuliko SMG.Mkuu wa mkoa wa mwanza john mongella ameahidi kuwa waliofanya mauaji ya mwenyekiti Alphonse na Yale ya msikiti wa mkolani watapatikana wakiwa hai au wamekufa.
Amesema vyombo vya usalama havilali, ili kuhakiisha watu hao wabapatikana wakiwa hai au wamekufa.
Amesema vyombo husika vitang'oa mzizi wa matukio hayo kama njia ya kuhakikidha kuwa mkoa wa Mza unakuwa salama.
Diwani wa buhongwa kaomba polisi wa kata hiyo wapatiwe gari na pia mtaa huu kujengwe kituo cha polisi.
Utajiuliza Jana ilikuwa shida kupata gari LA kuokoa maisha lakini Leo kuna msururu wa nagari yanakuja kutoa pole huku wakuu sana wakiahidi kutoa gari ya kusafirisha mwili wa marehemu aluyekosa gari LA kuokoa maisha yake!
Note: kutoka buhongwa police hadi bulale ni km 1, hata askari angetembea kwa miguu anaweza kuwahi tukio.