Mkuu ntamaholo.
Kwanini kudhalilisha taaluma za wengine. Mbona hatujasikia wananchi wakiombwa kufanya kazi ya Daktari kipindupindu kikiibuka? Kwanini polisi ambao wana intelijensia inayofanya kazi wakati wa shughuli za siasa?
Mkuu wewe utakuwa mchanga wa masuala haya. Sisi wakongwe tunajua. Ngoja nijaribu kukupa hints kidogo, i hope utanielewa.
1. Kwa mujibu wa sensa, tunakaribia mil 50. Na kwa mujibu wa taarifa za Polisi wenyewe, wanadai hawazidi 40,000 na hapo ni kuanzia ijp hadi aliyeko mafunzoni leo. Hivyo kila askari anahudumia watu 1250 kuhakikisha ulinzi na usalama wao. Hapo inajumuisha viongozi, walioko likizo, masomoni, wagonjwa na waliopata ulemavu wakitekeleza majukum ya kiulinzi. Kazi ni pevu.
International standard inataka kila askari kuhudumia 1:400, ni nchi chache sana zimefikia kiwango hicho.
2. Katiba ya jamhuri ya muungano ya JMT, inatamka wazi kuwa, ulinzi na usalama wa taifa hili, ni wajibu wa kila mwanachi. Kila mtu anahitaji kuwa salama na usalama ni zao letu sisi sote. Kama mimi nahitaji usalama, wewe huhitaji usalama, ni wajibu wangu kuhakikisha nawe unakuwa mwana usalama.
3. Sheria inayounda jeshi la polisi cap 322, pamoja na mambo mengine, ni kuhakikisha ulinzi na usalama wa raia na mali zao.
4. Sheria ya usalama wa taifa, kila mtu kwenye eneo lake ana wajibu wa kuhakikisha ulinzi na usalama unashamiri.
5. Sheria ya tawala za mikoa/wilaya na serikali za mtaa, wajibu wa kila kiongozi kwenye Tamisemi, kazi yake ya kwanza ni kuhakikisha watu wako salama.
Kwa hiyo kutaka ulinzi na usalama kwa kutegemea Polisi, huku wanaohitaji usalama hawashiriki ni kujidanganya tu. Intelijensi ya polisi inahitaji wananchi ili ifanye kazi. Intelijensi ya tiss inahitaji wananchi ifanye kazi. Bila wananchi hakuna linalofanyika.
Wahalifu ni sehem ya jamii, na wanajamii wanawajua wahalifu. Polisi haiwezi kuota. Wananchi wawatumbue tu.
Kazi ya polisi ni profession lkn huwezi linganisha na udaktari. Hata hivyo, ili madaktari watekeleze wajibu wao ipasavyo, wanahitaji kusimamiwa na wananchi wenyewe au kupitia viongozi wao. La sivyo matatizo yaliyopo yangekuwa maradufu ya haya yaliyopo.
Sijui umenielewa? Uliza kama hujaelewa