JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Watu watatu wamefikishwa Mahakamani kwa tuhuma za mauaji ya kuua mwanamke Mkoani Mtwara miaka 20 iliyopita.
Watuhumiwa hao ni wakazi wa Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Masasi kwa tuhuma za mauaji ya mwanamke aliyetambulika kwa majina ya Nora Hamisi.
Nora aliyekuwa Mkazi wa Kata ya Mkuti Wilayani Masasi, aliuawa na mwili wake kutupwa katika Mtaa wa Machinjioni katika Kata ya Mkuti.
Watuhumniwa hao walifikishwa kortini mwishoni mwa wiki mbele ya Hakimu wa Wilaya ya Masasi, Batista Kashusha na kusomewa mashtaka ya mauaji wanayodaiwa kuyafanya miaka 20 iliyopita.
Mwendesha Mashtaka wa Polisi Insepta Jovina alidai kuwa watuhumiwa hao wanakabiliwa na kesi hiyo namba 2 ya mwaka 2002 mbele ya Mahakama hiyo.
Aliwataja watuhumiwa hao na umri wao wa sasa kuwa ni; Rajabu Songo (34), kazi wa mtaa wa Machinjioni, Kata ya Mkuti Wilayani Masasi, Stanley Mtweve (32), Mkazi wa Mtaa wa Makaburini Kata ya Mkuti Wilayani Masasi na Yusuph Pahala (30), mkazi wa Mtaa wa Maendeleo Kata ya Mkomaindo wilayani Masasi.
Inspekta Jovina alidai kuwa watuhumiwa hao walimuua Nora kisha kuuchukua mwili wake na kuutupa katika Mtaa wa Machinjioni kisha kutoweka.
Alidai waliutupa mwili eneo hilo kwa lengo la kupoteza ushahidi, lakini baada ya uchunguzi wa Jeshi la Polisi walikamatwa. Watuhumiwa hawakutakiwa kuzungumza lolote kwa kuwa Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji.
Kwa mujibu wa sheria, Mahakama yenye mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji ni Mahakama Kuu.
Wote walirejeshwa mahabusu na kesi hiyo itatajwa tena Aprili 24, 2022.
============
Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara ni kuwa watuhumiwa hao wanatuhumiwa kutenda kosa hilo walipokuwa na umri mdogo na siyo kwamba ripoti ya umri wao imekosewa. Hivyo, umri uliotajwa mwenye habari yao ni umri walionao kwa sasa mwaka 2022.
Source: Nipashe