Watu watatu wafikishwa Mahakamani kwa kosa la mauaji yaliyotokea miaka 20 iliyopita

Watu watatu wafikishwa Mahakamani kwa kosa la mauaji yaliyotokea miaka 20 iliyopita

Watu watatu wamefikishwa Mahakamani kwa tuhuma za mauaji ya kuua mwanamke Mkoani Mtwara miaka 20 iliyopita.

Watuhumiwa hao ni wakazi wa Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Masasi kwa tuhuma za mauaji ya mwanamke aliyetambulika kwa majina ya Nora Hamisi.

Nora aliyekuwa Mkazi wa Kata ya Mkuti Wilayani Masasi, aliuawa na mwili wake kutupwa katika Mtaa wa Machinjioni katika Kata ya Mkuti.

Watuhumniwa hao walifikishwa kortini mwishoni mwa wiki mbele ya Hakimu wa Wilaya ya Masasi, Batista Kashusha na kusomewa mashtaka ya mauaji wanayodaiwa kuyafanya miaka 20 iliyopita.

Mwendesha Mashtaka wa Polisi Insepta Jovina alidai kuwa watuhumiwa hao wanakabiliwa na kesi hiyo namba 2 ya mwaka 2002 mbele ya Mahakama hiyo.

Aliwataja watuhumiwa hao ni Rajabu Songo (34), kazi wa mtaa wa Machinjioni, Kata ya Mkuti Wilayani Masasi, Stanley Mtweve (32), Mkazi wa Mtaa wa Makaburini Kata ya Mkuti Wilayani Masasi na Yusuph Pahala (30), mkazi wa Mtaa wa Maendeleo Kata ya Mkomaindo wilayani Masasi.

Inspekta Jovina alidai kuwa watuhumiwa hao walimuua Nora kisha kuuchukua mwili wake na kuutupa katika Mtaa wa Machinjioni kisha kutoweka.

Alidai waliutupa mwili eneo hilo kwa lengo la kupoteza ushahidi, lakini baada ya uchunguzi wa Jeshi la Polisi walikamatwa. Watuhumiwa hawakutakiwa kuzungumza lolote kwa kuwa Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji.

Kwa mujibu wa sheria, Mahakama yenye mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji ni Mahakama Kuu.

Wote walirejeshwa mahabusu na kesi hiyo itatajwa tena Aprili 24, 2022.


Source: Nipashe
Wakazi wa mitaa ya Machinjioni na Makaburini! Waathirika wa majina ya mitaa.
 
Kosa miaka 20 iliyopita, watumiwa miaka 30, 32 na 34; maana yake walikuwa miaka 10,12 na 14. Okay
Nimejiuliza swali ilo ilo. Kwamba tukirudisha nyuma 20 years, how was that possible? Kwamba watoto walimbeba marehemu na kwenda kumtupa, watoto waliweza kuitunza Siri?
 
Watoto wa miaka kumi na nne,kumi na tatu miaka 20 iliyopita walikuwa kidogo wana miili unaweza kusema ni sawa tu na watoto wa form 3 miaka hii hivyo akili ya kutenda jinai hiyo wanaweza kuwa nayo na hata akili ya kusema tufiche mwili wanaweza kuwa nayo vilevile,miaka ya 80 tukiwa bado wadogo kuna mtoto mwenzetu mtaani alimpiga teke la tumbo mwenzie na kumuua tukiwa tunacheza tu kiutaniutani hivyo labda tusikie mazingira ya kifo yalikuwaje kwa wenzetu hao
 
Aliwataja watuhumiwa hao na umri wao ulivyokuwa wakati wa tukio ni; Rajabu Songo (34), kazi wa mtaa wa Machinjioni, Kata ya Mkuti Wilayani Masasi, Stanley Mtweve (32), Mkazi wa Mtaa wa Makaburini Kata ya Mkuti Wilayani Masasi na Yusuph Pahala (30), mkazi wa Mtaa wa Maendeleo Kata ya Mkomaindo wilayani Masasi.
Watuhumiwa wakati wa tukio walikuwa na hiyo miaka 2002 ,kwa hiyo sasa wapo na miaka hamsini plus nilivyoelewa mimi.
 
mbona maelezo yanaeleza vizuri,mwandisha umri wa watuhimiwa wakati wa tukio
... huyo ni mtu aliyesoma hiyo habari mwenyewe yet hakuelewa; sijui akienda kumsimulia mwingine na huyo mwingine naye akaenda kusimulia; after 5 recipients haitakuwa hiyo habari tena; itakuwa habari "mpya" kabisa!
 
Back
Top Bottom