Watu watatu wafikishwa Mahakamani kwa kosa la mauaji yaliyotokea miaka 20 iliyopita

Kosa miaka 20 iliyopita, watumiwa miaka 30, 32 na 34; maana yake walikuwa miaka 10,12 na 14. Okay
Walikuwa na miaka hiyo wakati wanafanya hilo tukio,sasa hapo hiyo miaka ongeza na 20 ndo upate umri wao wa saizi.
 
Kosa miaka 20 iliyopita, watumiwa miaka 30, 32 na 34; maana yake walikuwa miaka 10,12 na 14. Okay
Isome Tena taarifa! Mbona imeeleza wazi kwamba wametajwa na Umri WALIOKUWA NAO WAKATI WA TUKIO!
Kwa maana nyingine huo Umri Hapo ni WA Wakati wa Tukio... Sasa ili kupata Umri Kamili wa Wahukumiwa, Ongeza Miaka Ishirini!
Watuhumiwa Sasa Wana Miaka Hamsini naa...!
 
Woooote mnaosema tulikurupuka someni hapa kwanza

1650362168499.png

Mwandishi alijichanganya.
 
Some I Tena hiyo Taarifa Kwa Umakini! Imesema wazii Majina ya Watuhumiwa NA UMRI WALIOKUWA NAO WAKATI WA TUKIO!
Tatizo Kila kitu tunataka kusoma haraha haraka bila kutafakari!!
 
Aliwataja watuhumiwa hao na umri wao ulivyokuwa wakati wa tukio ni; Rajabu Songo (34), kazi wa mtaa wa Machinjioni, Kata ya Mkuti Wilayani Masasi, Stanley Mtweve (32), Mkazi wa Mtaa wa Makaburini Kata ya Mkuti Wilayani Masasi na Yusuph Pahala (30), mkazi wa Mtaa wa Maendeleo Kata ya Mkomaindo wilayani Masasi.

Mna haraka sana au hamjasoma mada?
1650362220322.png

Kuna umuhimu wa kuwa na edit history ya post kwenye forum Maxence Melo
 
Watu watatu wamefikishwa Mahakamani kwa tuhuma za mauaji ya kuua mwanamke Mkoani Mtwara miaka 20 iliyopita.

Watuhumiwa hao ni wakazi wa Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Masasi kwa tuhuma za mauaji ya mwanamke aliyetambulika kwa majina ya Nora Hamisi.

Nora aliyekuwa Mkazi wa Kata ya Mkuti Wilayani Masasi, aliuawa na mwili wake kutupwa katika Mtaa wa Machinjioni katika Kata ya Mkuti.

Watuhumniwa hao walifikishwa kortini mwishoni mwa wiki mbele ya Hakimu wa Wilaya ya Masasi, Batista Kashusha na kusomewa mashtaka ya mauaji wanayodaiwa kuyafanya miaka 20 iliyopita.

Mwendesha Mashtaka wa Polisi Insepta Jovina alidai kuwa watuhumiwa hao wanakabiliwa na kesi hiyo namba 2 ya mwaka 2002 mbele ya Mahakama hiyo.

Aliwataja watuhumiwa hao na umri wao ulivyokuwa wakati wa tukio ni; Rajabu Songo (34), kazi wa mtaa wa Machinjioni, Kata ya Mkuti Wilayani Masasi, Stanley Mtweve (32), Mkazi wa Mtaa wa Makaburini Kata ya Mkuti Wilayani Masasi na Yusuph Pahala (30), mkazi wa Mtaa wa Maendeleo Kata ya Mkomaindo wilayani Masasi.

Inspekta Jovina alidai kuwa watuhumiwa hao walimuua Nora kisha kuuchukua mwili wake na kuutupa katika Mtaa wa Machinjioni kisha kutoweka.

Alidai waliutupa mwili eneo hilo kwa lengo la kupoteza ushahidi, lakini baada ya uchunguzi wa Jeshi la Polisi walikamatwa. Watuhumiwa hawakutakiwa kuzungumza lolote kwa kuwa Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji.

Kwa mujibu wa sheria, Mahakama yenye mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji ni Mahakama Kuu.

Wote walirejeshwa mahabusu na kesi hiyo itatajwa tena Aprili 24, 2022.

Source: Nipashe
Kesi haiozi aisee.
 
Kosa miaka 20 iliyopita, watumiwa miaka 30, 32 na 34; maana yake walikuwa miaka 10,12 na 14. Okay
Someni vizuri na muelewe hapa mbona wamebainisha kabisa....

Aliwataja watuhumiwa hao na umri wao ulivyokuwa wakati wa tukio ni; Rajabu Songo (34), kazi wa mtaa wa Machinjioni, Kata ya Mkuti Wilayani Masasi, Stanley Mtweve (32), Mkazi wa Mtaa wa Makaburini Kata ya Mkuti Wilayani Masasi na Yusuph Pahala (30), mkazi wa Mtaa wa Maendeleo Kata ya Mkomaindo wilayani Masasi.
Kwa maana hiyo kwa sasa watuhumiwa wanamika 54,52na 50 kwa sasa

Quote
 
Kosa miaka 20 iliyopita, watumiwa miaka 30, 32 na 34; maana yake walikuwa miaka 10,12 na 14. Okay
Aliwataja watuhumiwa hao na umri wao ulivyokuwa wakati wa tukio ni; Rajabu Songo (34), kazi wa mtaa wa Machinjioni, Kata ya Mkuti Wilayani Masasi, Stanley Mtweve (32), Mkazi wa Mtaa wa Makaburini Kata ya Mkuti Wilayani Masasi na Yusuph Pahala (30), mkazi wa Mtaa wa Maendeleo Kata ya Mkomaindo wilayani Masasi.

Jitahidi kusoma between the line kiongozi wangu. Nadhani hakuna utata wa aina yoyote katika hili. Maana yake ni kwamba, chukua umri wa kila mtugumiwa kwa wakati huu, kisha jumlisha miaka 20 ili upate umri halisi wa sasa wa kila mtuhumiwa.
 
Back
Top Bottom