BARA BARA YA 5
JF-Expert Member
- Sep 11, 2009
- 1,174
- 835
Miaka yao kwa wakati huo..sio.kwa sasa....Kosa miaka 20 iliyopita, watumiwa miaka 30, 32 na 34; maana yake walikuwa miaka 10,12 na 14. Okay
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Miaka yao kwa wakati huo..sio.kwa sasa....Kosa miaka 20 iliyopita, watumiwa miaka 30, 32 na 34; maana yake walikuwa miaka 10,12 na 14. Okay
Walikuwa na miaka hiyo wakati wanafanya hilo tukio,sasa hapo hiyo miaka ongeza na 20 ndo upate umri wao wa saizi.Kosa miaka 20 iliyopita, watumiwa miaka 30, 32 na 34; maana yake walikuwa miaka 10,12 na 14. Okay
Mbona kasema ni umri wao ulivyokuwa miaka hiyoKwahiyo hao watoto wa miaka 10, 12 na 14 waliweza kumuua mwanamke na kuutupa mwili kuficha ushahidi? Mnatuona sisi mazezeta sio?
Labda kama wameedit... haikuwa hivyo mwanzoniHuu umri ni WA wakati wanatenda jinai
Isome Tena taarifa! Mbona imeeleza wazi kwamba wametajwa na Umri WALIOKUWA NAO WAKATI WA TUKIO!Kosa miaka 20 iliyopita, watumiwa miaka 30, 32 na 34; maana yake walikuwa miaka 10,12 na 14. Okay
Miaka yao kwa wakati huo..sio.kwa sasa....
Aliwataja watuhumiwa hao na umri wao ulivyokuwa wakati wa tukio ni; Rajabu Songo (34), kazi wa mtaa wa Machinjioni, Kata ya Mkuti Wilayani Masasi, Stanley Mtweve (32), Mkazi wa Mtaa wa Makaburini Kata ya Mkuti Wilayani Masasi na Yusuph Pahala (30), mkazi wa Mtaa wa Maendeleo Kata ya Mkomaindo wilayani Masasi.
Mna haraka sana au hamjasoma mada?
Nimekusoma mkuu. Kumbe mada alikuwa edited.
Ndio mkuu.... halafu tunaonekana vilaza wakurupukaji bure 😂😂😂😂Nimekusoma mkuu. Kumbe mada alikuwa edited.
Ni umri wao ulivyokuwa wakati wa tukio. Kwa sasa wote ni 50+Hapa tumedanganywa kwenye suala zima la umri. Bora hata ingekuwa 40 kasoro, au 40+
Izo chuki binafsi sasa..Tushetani tudogo tukikua huwa yanakuwa mashetani makubwa sana.Sijahusianisha na shauri tajwa.Kama UVCCM tu.Unategemea watakuwaje mbeleni?
Soma vizuri yaliyoandikwa. Mwandishi amesema kabisa umri wa watuhumiwa wakati wa tukio ulikuwa kadha wa kadha.Kosa miaka 20 iliyopita, watumiwa miaka 30, 32 na 34; maana yake walikuwa miaka 10,12 na 14. Okay
Kesi haiozi aisee.Watu watatu wamefikishwa Mahakamani kwa tuhuma za mauaji ya kuua mwanamke Mkoani Mtwara miaka 20 iliyopita.
Watuhumiwa hao ni wakazi wa Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Masasi kwa tuhuma za mauaji ya mwanamke aliyetambulika kwa majina ya Nora Hamisi.
Nora aliyekuwa Mkazi wa Kata ya Mkuti Wilayani Masasi, aliuawa na mwili wake kutupwa katika Mtaa wa Machinjioni katika Kata ya Mkuti.
Watuhumniwa hao walifikishwa kortini mwishoni mwa wiki mbele ya Hakimu wa Wilaya ya Masasi, Batista Kashusha na kusomewa mashtaka ya mauaji wanayodaiwa kuyafanya miaka 20 iliyopita.
Mwendesha Mashtaka wa Polisi Insepta Jovina alidai kuwa watuhumiwa hao wanakabiliwa na kesi hiyo namba 2 ya mwaka 2002 mbele ya Mahakama hiyo.
Aliwataja watuhumiwa hao na umri wao ulivyokuwa wakati wa tukio ni; Rajabu Songo (34), kazi wa mtaa wa Machinjioni, Kata ya Mkuti Wilayani Masasi, Stanley Mtweve (32), Mkazi wa Mtaa wa Makaburini Kata ya Mkuti Wilayani Masasi na Yusuph Pahala (30), mkazi wa Mtaa wa Maendeleo Kata ya Mkomaindo wilayani Masasi.
Inspekta Jovina alidai kuwa watuhumiwa hao walimuua Nora kisha kuuchukua mwili wake na kuutupa katika Mtaa wa Machinjioni kisha kutoweka.
Alidai waliutupa mwili eneo hilo kwa lengo la kupoteza ushahidi, lakini baada ya uchunguzi wa Jeshi la Polisi walikamatwa. Watuhumiwa hawakutakiwa kuzungumza lolote kwa kuwa Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji.
Kwa mujibu wa sheria, Mahakama yenye mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji ni Mahakama Kuu.
Wote walirejeshwa mahabusu na kesi hiyo itatajwa tena Aprili 24, 2022.
Source: Nipashe
Wabongo kwa kudandia story juu juu hawajambo.Mbona kwenye habari wamesema kabisa umri wao ulivyokuwa wakati wa tukio.................
Someni vizuri na muelewe hapa mbona wamebainisha kabisa....Kosa miaka 20 iliyopita, watumiwa miaka 30, 32 na 34; maana yake walikuwa miaka 10,12 na 14. Okay
Aliwataja watuhumiwa hao na umri wao ulivyokuwa wakati wa tukio ni; Rajabu Songo (34), kazi wa mtaa wa Machinjioni, Kata ya Mkuti Wilayani Masasi, Stanley Mtweve (32), Mkazi wa Mtaa wa Makaburini Kata ya Mkuti Wilayani Masasi na Yusuph Pahala (30), mkazi wa Mtaa wa Maendeleo Kata ya Mkomaindo wilayani Masasi.Kosa miaka 20 iliyopita, watumiwa miaka 30, 32 na 34; maana yake walikuwa miaka 10,12 na 14. Okay
Ila watakaa mahabusu ya wakubwa sio ya watoto.Inapaswa shauri Lao lisikilizwe kwanza na mambo ya umri wao yataangaliwa kisheria kulingana na wakati wa tukio.