Watu wawili wamefariki dunia kwa ajali iliyohusisha basi la mwendokasi na pikipiki

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Kwa mujibu wa Kamanda wa polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema kuwa ajali hiyo imetokea jana Septemba 8, 2021 saa 3:20 usiku.

Amesema ajali hiyo imetokea katika barabara ya mwendokasi eneo la Lumumba kwenye taa za kuongozea magari.

Ameitaja pikipiki yenye namba za usajili MC 663 CDX aina ya Boxer ikiendeshwa na Sami Riyaz Khan (17), Mkazi wa Gerezani, akiwa na abiria wake Patrick Chohan(16) iligongana na basi la mwendokasi lenye namba za usaji T 880 DGV aina ya Golden Dragon lililokuwa likitokea Kimara kuelekea Kivukoni na kusababisha vifo vya dereva wa pikipiki na abiria.

“Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa chanzo cha ajali ni dereva wa pikipiki kujaribu kupita taa nyekundu kinyume cha sheria, ndipo walipogongwa na gari la Mwendokasi na kufariki dunia wote.

“Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linawataka madereva wa pikipiki kutii sheria za usalama barabarani hususani taa za kuongozea magari, kuvaa kofia ngumu na kutopita kwenye barabara za Mwendokasi,” amesema Muliro.

=====

TAARIFA YA AJALI YA BASI LA MWENDOKASI NA PIKIPIKI NA KUPELEKEA VIFO VYA WATU WAWILI

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam lianasikitika kutoa taarifa ya ajali iliyohusisha basi la Mwendokasi na Pikipiki iliyopelekea vifo vya watu wawili.

Ajali hiyo ilitokea tarehe 08/09/2021 majira ya saa 21:20 usiku katika barabara ya mwendokasi eneo la Lumumba kwenye taa za kuongozea magari,ambapo pikipiki yenye namba za usajili MC 663 CDX aina ya Boxer ikiendeshwa na Sami Riyaz Khan(17),Mkazi wa Gerezani, akiwa na abiria wake Patrick Chohan(16) iligongana na basi la mwendokasi lenye namba za usaji T 880 DGV aina ya Golden Dragon lililokuwa likitokea Kimara kuelekea Kivukoni na kusababisha vifo vya dereva wa pikipiki na abiria.

Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa chanzo cha ajali ni dereva wa pikipiki kujaribu kupita taa nyekundu kinyume cha sheria, ndipo walipogongwa na gari la Mwendokasi na kufariki dunia wote.
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linawataka madereva wa pikipiki kutii sheria za usalama barabarani husasani taa za kuongozea magari,kuvaa kofia ngumu na kutopita kwenye barabara za Mwendokasi.

Imetolewa na:-
MULIRO J. MULIRO- ACP KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM, DAR ES SALAAM.
09/09/2021
Screenshot_20210909-201741.png
 
Nimeona picha yao ya ajali duh,
Inasikitisha sana,
Halfuuuu hawa mwendokasi wapewe somo la kupunguza mwendo kila wanapopita mataa hata kama taa zinawaruhusu ili kuokoa vijana wetu,
Kwa kuwa wametengewa barabara yao basi ni amri moja tu hakuna kuangalia hata kama anapita kichaa, wazee, walemavu n. K.
Ilimradi taa zinawaruhusu?
Hili liangaliwe sana la sivyo hawa jamaa wataendelea kupasua vichwa vya bodaboda kila uchwao,
Ukitaka kujua mwendokasi ni wajeuri kaa kwenye taa halafu uone jinsi wanavyofanya fujo,
Hao wa jana wote walibasti vichwa
 
Leseni ya kuendesha pikipiki ni miaka 16 tu.
Kumbe ndio maana bodaboda walio wengi ni watoto waliokimbia shule na kupewa leseni za kubeba abiria?

Sasa nimejua hawa watoto hawana shida bali walezi wao (serikali) ndio tatizo
 
Nimeona picha yao ya ajali duh,
Inasikitisha sana,
Halfuuuu hawa mwendokasi wapewe somo la kupunguza mwendo kila wanapopita mataa hata kama taa zinawaruhusu ili kuokoa vijana wetu,
Kwa kuwa wametengewa barabara yao basi ni amri moja tu hakuna kuangalia hata kama anapita kichaa, wazee, walemavu n. K.
Ilimradi taa zinawaruhusu?
Hili liangaliwe sana la sivyo hawa jamaa wataendelea kupasua vichwa vya bodaboda kila uchwao,
Ukitaka kujua mwendokasi ni wajeuri kaa kwenye taa halafu uone jinsi wanavyofanya fujo,
Hao wa jana wote walibasti vichwa
Swali ni kwanini wavuke ilhali taa haziruhusu??
 
Kwa mujibu wa Kamanda wa polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema kuwa ajali hiyo imetokea jana Septemba 8, 2021 saa 3:20 usiku.

Amesema ajali hiyo imetokea katika barabara ya mwendokasi eneo la Lumumba kwenye taa za kuongozea magari.

Ameitaja pikipiki yenye namba za usajili MC 663 CDX aina ya Boxer ikiendeshwa na Sami Riyaz Khan (17), Mkazi wa Gerezani, akiwa na abiria wake Patrick Chohan(16) iligongana na basi la mwendokasi lenye namba za usaji T 880 DGV aina ya Golden Dragon lililokuwa likitokea Kimara kuelekea Kivukoni na kusababisha vifo vya dereva wa pikipiki na abiria.

“Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa chanzo cha ajali ni dereva wa pikipiki kujaribu kupita taa nyekundu kinyume cha sheria, ndipo walipogongwa na gari la Mwendokasi na kufariki dunia wote.

“Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linawataka madereva wa pikipiki kutii sheria za usalama barabarani hususani taa za kuongozea magari, kuvaa kofia ngumu na kutopita kwenye barabara za Mwendokasi,” amesema Muliro.

=====

TAARIFA YA AJALI YA BASI LA MWENDOKASI NA PIKIPIKI NA KUPELEKEA VIFO VYA WATU WAWILI

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam lianasikitika kutoa taarifa ya ajali iliyohusisha basi la Mwendokasi na Pikipiki iliyopelekea vifo vya watu wawili.

Ajali hiyo ilitokea tarehe 08/09/2021 majira ya saa 21:20 usiku katika barabara ya mwendokasi eneo la Lumumba kwenye taa za kuongozea magari,ambapo pikipiki yenye namba za usajili MC 663 CDX aina ya Boxer ikiendeshwa na Sami Riyaz Khan(17),Mkazi wa Gerezani, akiwa na abiria wake Patrick Chohan(16) iligongana na basi la mwendokasi lenye namba za usaji T 880 DGV aina ya Golden Dragon lililokuwa likitokea Kimara kuelekea Kivukoni na kusababisha vifo vya dereva wa pikipiki na abiria.

Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa chanzo cha ajali ni dereva wa pikipiki kujaribu kupita taa nyekundu kinyume cha sheria, ndipo walipogongwa na gari la Mwendokasi na kufariki dunia wote.
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linawataka madereva wa pikipiki kutii sheria za usalama barabarani husasani taa za kuongozea magari,kuvaa kofia ngumu na kutopita kwenye barabara za Mwendokasi.

Imetolewa na:-
MULIRO J. MULIRO- ACP KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM, DAR ES SALAAM.
09/09/2021
View attachment 1930929
Gone too young...before 18 na si ajabu dereva alikuwa na leseni
 
Nimeona picha yao ya ajali duh,
Inasikitisha sana,
Halfuuuu hawa mwendokasi wapewe somo la kupunguza mwendo kila wanapopita mataa hata kama taa zinawaruhusu ili kuokoa vijana wetu,
Kwa kuwa wametengewa barabara yao basi ni amri moja tu hakuna kuangalia hata kama anapita kichaa, wazee, walemavu n. K.
Ilimradi taa zinawaruhusu?
Hili liangaliwe sana la sivyo hawa jamaa wataendelea kupasua vichwa vya bodaboda kila uchwao,
Ukitaka kujua mwendokasi ni wajeuri kaa kwenye taa halafu uone jinsi wanavyofanya fujo,
Hao wa jana wote walibasti vichwa

Ulisha wahi kuendesha gari hapa mjini? Asee kuna wakati unaweza sema maneno mabaya sana kwa ajili ya waendesha pikipiki. Yaana anaweza pita mbele yako shaaa unapambana kumukoa ila wala hajali. Jana mataa ya hapa Tangibovu yana ruhusu gari zinazotika goba zipite jamaa ww boda ana force apite usawq wa Tegeta kama vile taa ndio za upande wake, Kusema ukweli inatakiwa semina za lazima kila mwezi mara 1 kuwakumbusha la sivyo watakufa wengi saana.
 
Back
Top Bottom