Watu wema bado wapo na wanaishi

Watu wema bado wapo na wanaishi

Leejay49

JF-Expert Member
Joined
Feb 10, 2023
Posts
16,388
Reaction score
51,970
Sijui nisemaje lakini you people mmenishangaza sana,

Always humu huwa nahisigi kuna watu flani hivi sijui nisemaje lakini mnisamehe nilivyokuwa nawawazia sivyo,.

First of all mie ni mtu ambaye siwezagi kukaa na kitu rohoni kwakweli,. Ila sio muongeaji kwa watu wangu wanaonizunguka, so JamiiForums ndio eneo ambalo naweza kutema nyongo zangu zooote,. Na huwa sijali hata kama watu wakisema najiexpose, ( As long as ni mimi na sivunji sheria yeyote ile huwa najionaga niko tu normal. )

Jana nlipost ule uzi wangu wa kutapeliwa just nipate tu faraja maana huku nje hata kumsimulia mtu nlikua naona aibu na kujiona mjinga, ila nyie watu mmenishangaza sanaaa, Mmeenda Beyond na zile faraja nlizopewa, Beyond kabisa na yale maneno mliyoandika "pole Leejay, pole mammy, pole cute and everything,.. masai dada nadhani alisema niweke Account number nikawaza nikasema em ngoja nijaribu nione,. Ila haikukaa sana nikaifuta ile Comment nikaona kama najichoresha ( Ila sijui kuna watu waliicopy😊). Kuna wawili watatu nliona wametuma chochote kitu akiwemo Manyanza,,. Na wengine hata siwajui I'd zao ni ilikuwa tu kimyakimya na hawakusema ni kina nani,..

Kisimu changu kuna mda kilizima chaji jana sikuwa nimeshughulika nacho tena, mpaka ile asubuhi nimechaji nimekiwasha Naona notofications za CRDB Bank ni nyingi mpaka kinaandika Sms Full, Nachungulia nione kiukweli hadi nikatamani nipige makelele 😥🤭,. Nyie watu Mungu awabariki sana aisee.

Nimeshindwa namna nzuri ya kuwashukuru wote ni ipi maana sina hata namba zenu za simu na Pm nilifunga lakini, sidhani kama humu kuna watu wanafaham majina yenu halisi ila tu nyie watu mpo kwenye maombi yangu kuanzia sasa.

Manyanza nimekutag kwasabu ni wewe pekeyako ulinithibitishia na niliona jina lako,..
Ila kuna hawa watu siwajui ni kina nani, japo mmefanya sirini mie kuwashukuru sirini pekeyake nimeshindwa, i Just want you to know that " Mko na kiti chenu peponi aisee "

"NILITAMANI SANA NIZIFAHAMU ID ZENU NIMFATE MMOJA MMOJA KUWASHUKURU LAKINI NDIO HIVYO TENA NIMESHINDWA KUBAINI" ..

Nimeshindwa kuweka screenshoots kwasabu notifications zimeingia kwenye kisimu kidogo, kupiga picha muamala mojamoja nisingeweza,,. ( Nimefanya hivyo nikiamini kuwa humu hakuna anayefahamu majina yenu halisi, na nitafuta baada ya mda ).

Niseme tu Imepitiliza ile nliyotapeliwa🙌🙌🙏, Mbarikiwe sana aisee And my Pm will be open, You just hit and say ni Mimi au vyovyote vile ili siku ikitokea watu wanakusumbua hapa nideal nao wasikuchoshe Tajiri wangu😂😂

Ni hayo tu,. Thanks
 
Back
Top Bottom