Watu wengi hushangaa kwanini wanawake wengi hupendelea kugombania wanaume wachache, huku wanaume wengi wakibaki bila chaguo

Uzi mtamu sana huu
 
Acha Ubishi hili liko dunia nzima, wanawake wanaweka vigezo na wengi wanahakikisha vimetimia
 
Ajabu hawa walugaluga wa vijijini wameingia miji mikubwa na kukuta pisi kali hasa maeneo ya kishua, halafu unakuta mporipori anakaa kilingeni na walugaluga wenzako kuwaelezea kuwa anapanga kumtokea mtoto anaisho masaki geti kali, huku yeye hata mlo mmoja ni changamoto
Ule wimbo wa zali la mentali umewatapeli sana watu wa vijijini kwa matumaini hewa
 
Wanaishia kupigwa za uso
 
Tunapozungumza muda huu, wanawake wawili wamepigana wakinigombania. Katika wawili hao Moja amefariki.

Muda mfupi ujao nitawatangazia msiba utafanyikia wapi
Mkuu hili tangazo lako ungempa maimartha ungepata pisi nyingi sana
 
Mwanaume gentleman lazima uudhurie misiba sherehe za kijamii uwajibikaji kwenye jamii inayokuzunguka

Ww mtoto wa kiume unakaaje bila kushriki mambo ya kijamii ukifa nani akuzike, mwanamke huwa apendi Mwanaume dhaifu asie na maadili
Upi uhusiano kati ya uhimara na uadilifu
 
Je, kama wanaume wengi wangeanza kuwa na standard na umakini sawa katika kuchagua wenza, taswira ya mahusiano ingekuwa tofauti na ilivyo leo?
Ukiweza hilo wanawake watasema una insecurity au watakuita misogynist. Inawachukiza sana wanawake pale mwanaume anapokuwa na standards. Wanafikiri kuwa na standards ni haki yao peke yao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…