Victor Mlaki
JF-Expert Member
- May 1, 2016
- 5,628
- 6,411
Katika kujifunza nimejaribu kubaini kuwa maombi yetu leo yana uelekeo wa aina moja "Baba nipe hiki au kile na siyo ya kusikiliza maelekezo"
Tunatumia muda mwingi kuomba na siyo kusikiliza ndiyo maana hata tunapopatiwa maelekezo ya namna ya kupata mahitaji yetu tutakuwa nje ya usikivu "we don't pay attention"
Kuomba ni kitu kingine na kusikiliza ni kitu kingine. Kwa mfano ukishamuomba mtu kitu chochote ni dhahiri hatua inayofuata ni kusubiri "kusikiliza" atakachokujibu.
Wakati mwingine unaweza ukawa unaendelea kuomba na kumbe kuna maelekezo alipaswa kusikiliza na kuyafanyia kazi ili kupata hitaji lako.
Watu wengi leo kulingana na masumbufu ya maisha ya kila siku na mahitaji yake hatutengi muda na maeneo tulivu ya kusikiliza na badala yake muda mwingi ni wa kuomba kuliko kusikiliza.
Asili inatuonesha umuhimu wa utulivu na kusikiliza kwa makini katika maisha na hili limedhihirisha uwezo mkubwa alionao binadamu katika tuwasiliane na mazingira yake na pia nguvu inayotawala mazingira hayo.
Katika kuruhusu usikivu kuna uwezekano wa kusikia mengi jambo ambalo linaweza kumsaidia binadamu kuishi mahitaji yake.
Mwili wa binadamu unaweza kutoa taarifa nyingi mno ikiwa tu upo katika hali nzuri kiafya inayoruhusu kujisikiliza.
Pamoja na kuwa na mahitaji mengi tunahitaji kutenga muda tutakaoutumia kusikiliza na kujisikiliza.