Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 89,019
- 156,726
1.Mungu yupo kwa sababu akili ya binadamu licha ya kufikiri inaongoza bado nayo inaongozwa.
Katika kutambua masuala mbalimbali akili ina uwanda na mawanda finye sana kwenye chanzo kwa sababu haina uwezo wa kuelezea chanzo cha vyanzo.
This is a logical non sequitur. Kwamba akili ya mtu inaongozwa, haioneshi kwamba inaongozwa na Mungu. Hapa umelazimisha.
Ufinyu wa akili ya mtu hauoneshi Mungu yupo. Umelazimisha hoja.
2.Akili haina uwezo wa kutambua kabisa kitu ambacho hakipo "human mind can not deny nothing".Hii ina inamaanisha ukiona kimetajwa tu maana yake kipo.Ingawa inawezekana kuwa na ugumu katika kuelezea uwepo.
Hizo ni baadhi tu ya sababu za kuafiki uwepo wa Mungu.
Quote me this "God has no personality"
Umesema nikiona kimetajwa, nijue kipo.
Nikitaja kwamba "wewe ni baba mzazi wa baba yako mzazi", kwa kuwa nimeweza kutaja hilo, kutaja kwangu kunakufanya wewe uwe baba mzazi wa baba yako mzazi?