Watu wengi wa Dar huwa wanajua huku Mwanza ukiwa na buku unapata ndoo ya samaki

Watu wengi wa Dar huwa wanajua huku Mwanza ukiwa na buku unapata ndoo ya samaki

MSAGA SUMU

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2015
Posts
6,661
Reaction score
21,656
Watu wengi hapo mjini Dar huwa wanadhani huku Mwanza samaki ni bei rahisi, yaani wanafikiri ukiwa na buku unabeba mzigo wa kutosha kumbe wapi. Mtu akisikia unaenda Dar ukitokea Mwanza kila mtu utasikia anasema niletee samaki.

Jitahidini kabla ya kuagiza kuletewa samaki mtume na hela ya kununulia, maisha yameshakuwa ghali hata sisi tunakula matembele.
 
Watu wengi hapo mjini Dar huwa wanadhani huku Mwanza samaki ni bei rahisi, yaani wanafikiri ukiwa na buku unabeba mzigo wa kutosha kumbe wapi. Mtu akisikia unaenda Dar ukitokea mwanza kila mtu utasikia anasema niletee samaki.
Jitahidini kabla ya kuagiza kuletewa samaki mtume na hela ya kununulia, maisha yameshakuwa ghali hata sisi tunakula matembele.
Mimi mwenyewe najua hivyo hivyo, debe la samaki kwa buku!!!
 
Hata wakiwafikia wakija huku mashambani wanatoa mimacho wanataka ndoo ya maharage kwa elfu 5. Yaani wakija likizo wanazunguka kuombaomba vyakula wanapakia IST mpaka inatembelea upande kama nyani.
Hee, Basi usiombe wajue unatoka Umasaini ndanindani huko. Utasikia bro; tunaomba utuandalie mbuzi wa krismasi hii.Tutakupitia hapo kumchukua. Hawajui mbuzi anayefaa kwa sasa huku Umasaini ni 120,000/= hadi 250,000/= au zaidi.(bei ya mnadani tar.02/10/2022).
 
Tukitoka huku wanasema tuwajie na ndizi, ili hali hata za kula nasi zatupiga chenga skuizi!!
Hali kadhalika sisi huku hakuna ng'ombe wa kuchinja kimasihara. Ng'ombe atachinjwa baada ya kufanyika kikao kujadili hoja ya kumchinja au labda ni mgonjwa. Labda sanasana mbuzi inawezekana kumfanya kitoweo endapo kuna tukio muhimu e.g. ugeni mzito au wanapokuja timu ya wataalam wa mifugo kutoa chanjo. Hali ni tete.
 
Na nyie watu wa kanda ya ziwa mnaowatumia ndoo za samaki satu na wao huwa wanawatumia ndoo za samaki wa vibua na makorokocho mengine ya ajabu yanayopatikana dar na kanda ya ziwa hayapo?
 
Watu wengi hapo mjini Dar huwa wanadhani huku Mwanza samaki ni bei rahisi, yaani wanafikiri ukiwa na buku unabeba mzigo wa kutosha kumbe wapi. Mtu akisikia unaenda Dar ukitokea Mwanza kila mtu utasikia anasema niletee samaki.

Jitahidini kabla ya kuagiza kuletewa samaki mtume na hela ya kununulia, maisha yameshakuwa ghali hata sisi tunakula matembele.
Umeishia kulalama tu pasipo kuweka bei elekezi ya ndoo ama vinginevyo.
 
Back
Top Bottom