MSAGA SUMU
JF-Expert Member
- May 25, 2015
- 6,661
- 21,656
Mimi mwenyewe najua hivyo hivyo, debe la samaki kwa buku!!!Watu wengi hapo mjini Dar huwa wanadhani huku Mwanza samaki ni bei rahisi, yaani wanafikiri ukiwa na buku unabeba mzigo wa kutosha kumbe wapi. Mtu akisikia unaenda Dar ukitokea mwanza kila mtu utasikia anasema niletee samaki.
Jitahidini kabla ya kuagiza kuletewa samaki mtume na hela ya kununulia, maisha yameshakuwa ghali hata sisi tunakula matembele.
Mimi nikajua hata ukiomba kwa kulialia hali mbaya nyumbani unachotewa za mboga buremimi mwenyewe najua hivyo hivyo, debe la samaki kwa buku!!!
Hee, Basi usiombe wajue unatoka Umasaini ndanindani huko. Utasikia bro; tunaomba utuandalie mbuzi wa krismasi hii.Tutakupitia hapo kumchukua. Hawajui mbuzi anayefaa kwa sasa huku Umasaini ni 120,000/= hadi 250,000/= au zaidi.(bei ya mnadani tar.02/10/2022).Hata wakiwafikia wakija huku mashambani wanatoa mimacho wanataka ndoo ya maharage kwa elfu 5. Yaani wakija likizo wanazunguka kuombaomba vyakula wanapakia IST mpaka inatembelea upande kama nyani.
Hali kadhalika sisi huku hakuna ng'ombe wa kuchinja kimasihara. Ng'ombe atachinjwa baada ya kufanyika kikao kujadili hoja ya kumchinja au labda ni mgonjwa. Labda sanasana mbuzi inawezekana kumfanya kitoweo endapo kuna tukio muhimu e.g. ugeni mzito au wanapokuja timu ya wataalam wa mifugo kutoa chanjo. Hali ni tete.Tukitoka huku wanasema tuwajie na ndizi, ili hali hata za kula nasi zatupiga chenga skuizi!!
Huku kwetu zamani ilikuwa Mmaasai kula samaki ni kituko au tuseme haiwezekani. Lakini kwa sasa tunakula hadi dagaanyama wa baharini kutoka Tanga kwa starehe kabisa.Tena sasa hivi wana bei kweli ππΌββοΈππΌββοΈ
Tunakula mchicha kwa kwenda mbele na hivi mara wanaleta kansa mara maji ya maiti
Kweli mfano mtu akiwa moshi akitaka kuja dar lazima ataambiwa aje na ndizi, Tabora ataambiwa aje na Asali, Mbeya ataambiwa Mchele, Singida kuku.Nahisi ni kasumba watu wamejiwekea kwamba kwakua mkoa flani kuna kitu flani basi utapata kwa bei rahisi nadhani ni Malaya tu ndio wabei hizo.
Umeishia kulalama tu pasipo kuweka bei elekezi ya ndoo ama vinginevyo.Watu wengi hapo mjini Dar huwa wanadhani huku Mwanza samaki ni bei rahisi, yaani wanafikiri ukiwa na buku unabeba mzigo wa kutosha kumbe wapi. Mtu akisikia unaenda Dar ukitokea Mwanza kila mtu utasikia anasema niletee samaki.
Jitahidini kabla ya kuagiza kuletewa samaki mtume na hela ya kununulia, maisha yameshakuwa ghali hata sisi tunakula matembele.
Kabsaaaa mkuuKweli mfano mtu akiwa moshi akitaka kuja dar lazima ataambiwa aje na ndizi, Tabora ataambiwa aje na Asali, Mbeya ataambiwa Mchele, Singida kuku.