ANKO JEI
JF-Expert Member
- Jul 21, 2018
- 1,319
- 2,504
Watu wa mikoani, hivi ulishawahi kujiuliza kwanini ndugu yako wa Dar anapiga chenga kila ukitaka kumtembelea? Ukiachana na chakula na gharama za Maisha, watu wengi wanaishi makazi duni sana hapa jijini.
Kwanza salamu kwako mkuu, wale wana dalisalama watumishi wa umma na wengineo najua imekua wikendi kubwa sana baada ya kupewa siku mbili za mapumziko. Okay twende kwenye hoja.
Mimi ni mpenzi sana wa makazi mazuri, yani kitu kinachochukua sehemu kubwa ya matumizi yangu si mavazi wala starehe ni makazi. Sasa hivi juzi vyuma vilikaza sana, nikasema nitafute nyumba angalau ya Laki 2 mpaka 250k kwa mwezi, bhasi bhana nikaanza kuwacheki madalali.
Dalali wa kwanza tukakutana maeneo ya kimara stop over pale, tukaanza Kwenda kwenye nyumba, panda milima na mabonde, tumefika kwenye nyumba kwanza gari haifiki, nyuma ya nyumba kuna mto sijui mfereji mkubwa, maji ndani hayatoki eti ukilipa utatengenezewa. Vyumba ni vidogo sana, kachoo kamejibana kwa mtu mwenye afya huwezi geuka kwa amani.
Tukaenda nyumba nyingine, aisee nilichoka, wapangaji ni wengi kama hostel Fulani, hilo sio shida sana, tunaingia ndani, eti wanasema chumba sebule jiko, jiko lenyewe ni kwamba pale sebleni wamebandika kasinki ka kunawia mikono na vi tiles kidogo ndo jiko eti, Dar bhana. choo cha chumbani hakina mlango, kwaio kama unaishi na mwenza full kunusishana harufu za chooni.
Kwa wiki nzima nimezunguka na madalali nimejionea mengi, wenye nyumba za dar ni wajanja sana, yani nyumba zinaungwa ungwa tu, inaweza kua kibaraza, wao wakaziba kikatokea chumba. Nilishindwa mwenyewe, nikaona niongee vizuri na mama mwenye nyumba wangu nitulie ninapokaa, najichanga mapema ili nitapohama nihamie sehemu nzuri.
Nilihamia dar rasmi mwaka 2015 niseme tu, dar ukitaka ufurahie kukaa pazuri na sehemu sio mbali na kati kati ya jiji andaa angalau Laki 4 kwa mwezi (kama una famili), ukitaka kitonga, tukutane makabe ndani ndani ambako kama una shughuli za mjini, utachakaa kwenye usafiri.
Napakumbuka sana mkoani, nilikua nakaa nyumba ya laki moja, ina vyumba vitatu vya kulala, sebule, jiko la ndani na la nje. Space kubwa full kujimwaga.
Wenyewe wanasema Karaha za Dar ndio utamu wake.
Vipi experience yako ya makazi hapa dar?