mkuu nakubaliana na wewe, lakini niamini mimi mtu anaekaa makazi ya kawaida dar akiwa mkoani kwa kodi ile ile anaweza ishi mahali standard sana, ni vile tu shughuli za utafutaji zinaamua tukae wapi. hebu fikiria mimi laki moja nilikua nakaa nyumba ya vyumba vitatu njombe huko, ila kwa dar, laki moja naweza pata chumba kimoja master, au chumba sebule pembeni ya mji.Ni Ukweli kwamba Dsm ina Wakaazi wengi sana ambao wanaishi kwenye makazi duni Sana. Hali hii lakini haipo Dsm tu peke yake Bali ipo kote nchini Tanzania ingawaje kuna tofaufi ndogo ndogo za hapa na pale.
Kiini au chanzo cha kuwepo kwa madhila yote haya ni kutokana na Serikali kutokuwajibika ipasavyo kwenye masuala muhimu zaidi ya kutekeleza Miradi ya Mipango-miji. Hakuna kabisa Mipango-miji ndani ya nchi hii ya Tanzania, miji yote kabisa ipo shaghala baghala na vururu vururu Kama mazizi ya ng'ombe. Nyumba nyingi sana zilizopo ndani ya Mkoa wa Dsm hazifikiki kwa barabara, bali zinafikika kwa njia za vichochoroni za watembea kwa miguu ambazo hazina uwezo hata wa kupitisha pikipiki, takribani 70% ya nyumba zote kabisa za Dsm zipo hivyo.
Uzuri au ubora wa kuweza kuwepo kwa Makazi Bora huanzia na hatua muhimu sana za kuwepo kwa Mipango-miji.
Hawana ustaarabu Wala nidhamu aibu ndio kabisa wameishiwa.hahaha kuingia kwenye mwendokasi unaweza kuvunjwa mkono usipokuwa makini. Mimi kati ya vitu vimenishinda ni kugombea usafiri, yani unaweza heshimu mtu mzima lakini yeye akakupiga kikumbo ubaya ubwela.
miaka kumi bado hujajenga nyumba yako tu?Watu wa mikoani, hivi ulishawahi kujiuliza kwanini ndugu yako wa Dar anapiga chenga kila ukitaka kumtembelea? Ukiachana na chakula na gharama za Maisha, watu wengi wanaishi makazi duni sana hapa jijini.
Kwanza salamu kwako mkuu, wale wana dalisalama watumishi wa umma na wengineo najua imekua wikendi kubwa sana baada ya kupewa siku mbili za mapumziko. Okay twende kwenye hoja.
Mimi ni mpenzi sana wa makazi mazuri, yani kitu kinachochukua sehemu kubwa ya matumizi yangu si mavazi wala starehe ni makazi. Sasa hivi juzi vyuma vilikaza sana, nikasema nitafute nyumba angalau ya Laki 2 mpaka 250k kwa mwezi, bhasi bhana nikaanza kuwacheki madalali.
Dalali wa kwanza tukakutana maeneo ya kimara stop over pale, tukaanza Kwenda kwenye nyumba, panda milima na mabonde, tumefika kwenye nyumba kwanza gari haifiki, nyuma ya nyumba kuna mto sijui mfereji mkubwa, maji ndani hayatoki eti ukilipa utatengenezewa. Vyumba ni vidogo sana, kachoo kamejibana kwa mtu mwenye afya huwezi geuka kwa amani.
Tukaenda nyumba nyingine, aisee nilichoka, wapangaji ni wengi kama hostel Fulani, hilo sio shida sana, tunaingia ndani, eti wanasema chumba sebule jiko, jiko lenyewe ni kwamba pale sebleni wamebandika kasinki ka kunawia mikono na vi tiles kidogo ndo jiko eti, Dar bhana. choo cha chumbani hakina mlango, kwaio kama unaishi na mwenza full kunusishana harufu za chooni.
Kwa wiki nzima nimezunguka na madalali nimejionea mengi, wenye nyumba za dar ni wajanja sana, yani nyumba zinaungwa ungwa tu, inaweza kua kibaraza, wao wakaziba kikatokea chumba. Nilishindwa mwenyewe, nikaona niongee vizuri na mama mwenye nyumba wangu nitulie ninapokaa, najichanga mapema ili nitapohama nihamie sehemu nzuri.
Nilihamia dar rasmi mwaka 2015 niseme tu, dar ukitaka ufurahie kukaa pazuri na sehemu sio mbali na kati kati ya jiji andaa angalau Laki 4 kwa mwezi (kama una famili), ukitaka kitonga, tukutane makabe ndani ndani ambako kama una shughuli za mjini, utachakaa kwenye usafiri.
Napakumbuka sana mkoani, nilikua nakaa nyumba ya laki moja, ina vyumba vitatu vya kulala, sebule, jiko la ndani na la nje. Space kubwa full kujimwaga.
Wenyewe wanasema Karaha za Dar ndio utamu wake.
Vipi experience yako ya makazi hapa dar?
Ukiachana na makabe umewahi paskia msumi? Hio ndio dar.Watu wa mikoani, hivi ulishawahi kujiuliza kwanini ndugu yako wa Dar anapiga chenga kila ukitaka kumtembelea? Ukiachana na chakula na gharama za Maisha, watu wengi wanaishi makazi duni sana hapa jijini.
Kwanza salamu kwako mkuu, wale wana dalisalama watumishi wa umma na wengineo najua imekua wikendi kubwa sana baada ya kupewa siku mbili za mapumziko. Okay twende kwenye hoja.
Mimi ni mpenzi sana wa makazi mazuri, yani kitu kinachochukua sehemu kubwa ya matumizi yangu si mavazi wala starehe ni makazi. Sasa hivi juzi vyuma vilikaza sana, nikasema nitafute nyumba angalau ya Laki 2 mpaka 250k kwa mwezi, bhasi bhana nikaanza kuwacheki madalali.
Dalali wa kwanza tukakutana maeneo ya kimara stop over pale, tukaanza Kwenda kwenye nyumba, panda milima na mabonde, tumefika kwenye nyumba kwanza gari haifiki, nyuma ya nyumba kuna mto sijui mfereji mkubwa, maji ndani hayatoki eti ukilipa utatengenezewa. Vyumba ni vidogo sana, kachoo kamejibana kwa mtu mwenye afya huwezi geuka kwa amani.
Tukaenda nyumba nyingine, aisee nilichoka, wapangaji ni wengi kama hostel Fulani, hilo sio shida sana, tunaingia ndani, eti wanasema chumba sebule jiko, jiko lenyewe ni kwamba pale sebleni wamebandika kasinki ka kunawia mikono na vi tiles kidogo ndo jiko eti, Dar bhana. choo cha chumbani hakina mlango, kwaio kama unaishi na mwenza full kunusishana harufu za chooni.
Kwa wiki nzima nimezunguka na madalali nimejionea mengi, wenye nyumba za dar ni wajanja sana, yani nyumba zinaungwa ungwa tu, inaweza kua kibaraza, wao wakaziba kikatokea chumba. Nilishindwa mwenyewe, nikaona niongee vizuri na mama mwenye nyumba wangu nitulie ninapokaa, najichanga mapema ili nitapohama nihamie sehemu nzuri.
Nilihamia dar rasmi mwaka 2015 niseme tu, dar ukitaka ufurahie kukaa pazuri na sehemu sio mbali na kati kati ya jiji andaa angalau Laki 4 kwa mwezi (kama una famili), ukitaka kitonga, tukutane makabe ndani ndani ambako kama una shughuli za mjini, utachakaa kwenye usafiri.
Napakumbuka sana mkoani, nilikua nakaa nyumba ya laki moja, ina vyumba vitatu vya kulala, sebule, jiko la ndani na la nje. Space kubwa full kujimwaga.
Wenyewe wanasema Karaha za Dar ndio utamu wake.
Vipi experience yako ya makazi hapa dar?
Watu wengi wa Dar wanafosi maisha aise.Watu wa mikoani, hivi ulishawahi kujiuliza kwanini ndugu yako wa Dar anapiga chenga kila ukitaka kumtembelea? Ukiachana na chakula na gharama za Maisha, watu wengi wanaishi makazi duni sana hapa jijini.
Kwanza salamu kwako mkuu, wale wana dalisalama watumishi wa umma na wengineo najua imekua wikendi kubwa sana baada ya kupewa siku mbili za mapumziko. Okay twende kwenye hoja.
Mimi ni mpenzi sana wa makazi mazuri, yani kitu kinachochukua sehemu kubwa ya matumizi yangu si mavazi wala starehe ni makazi. Sasa hivi juzi vyuma vilikaza sana, nikasema nitafute nyumba angalau ya Laki 2 mpaka 250k kwa mwezi, bhasi bhana nikaanza kuwacheki madalali.
Dalali wa kwanza tukakutana maeneo ya kimara stop over pale, tukaanza Kwenda kwenye nyumba, panda milima na mabonde, tumefika kwenye nyumba kwanza gari haifiki, nyuma ya nyumba kuna mto sijui mfereji mkubwa, maji ndani hayatoki eti ukilipa utatengenezewa. Vyumba ni vidogo sana, kachoo kamejibana kwa mtu mwenye afya huwezi geuka kwa amani.
Tukaenda nyumba nyingine, aisee nilichoka, wapangaji ni wengi kama hostel Fulani, hilo sio shida sana, tunaingia ndani, eti wanasema chumba sebule jiko, jiko lenyewe ni kwamba pale sebleni wamebandika kasinki ka kunawia mikono na vi tiles kidogo ndo jiko eti, Dar bhana. choo cha chumbani hakina mlango, kwaio kama unaishi na mwenza full kunusishana harufu za chooni.
Kwa wiki nzima nimezunguka na madalali nimejionea mengi, wenye nyumba za dar ni wajanja sana, yani nyumba zinaungwa ungwa tu, inaweza kua kibaraza, wao wakaziba kikatokea chumba. Nilishindwa mwenyewe, nikaona niongee vizuri na mama mwenye nyumba wangu nitulie ninapokaa, najichanga mapema ili nitapohama nihamie sehemu nzuri.
Nilihamia dar rasmi mwaka 2015 niseme tu, dar ukitaka ufurahie kukaa pazuri na sehemu sio mbali na kati kati ya jiji andaa angalau Laki 4 kwa mwezi (kama una famili), ukitaka kitonga, tukutane makabe ndani ndani ambako kama una shughuli za mjini, utachakaa kwenye usafiri.
Napakumbuka sana mkoani, nilikua nakaa nyumba ya laki moja, ina vyumba vitatu vya kulala, sebule, jiko la ndani na la nje. Space kubwa full kujimwaga.
Wenyewe wanasema Karaha za Dar ndio utamu wake.
Vipi experience yako ya makazi hapa dar?
Ukienda Dodoma utatengua kauli yako.Dar nyumba zipo overrated sana.
Kuelezea si kubeza mkuu, mafanikio ya mtu hayapimwi kwenye muda wala kujenga nyumba. mtu yeyote anaeongea bila bias atakueleza hiki nilichokueleza hapa.miaka kumi bado hujajenga nyumba yako tu?
halafu unaleta ujuaji kwenye nyumba zawatu? na unazibeza kabisa😁😁😁😁😁😁😁😁
akili huna wewe
Upo sahihi kabisa, kuna nyumba nzuri sana ukiwa na bajeti nzuri.Nyumba standard ya kijana Dar anayejitafuta atleast uwe na budget ya 400-800k (siongelei chumba)
700k-1.2M kwa mtu mwenye familia, anayetaka kuishi vizuri-middle class ya kati.
Kuanzia 1.5M na kuendelea kwa maeneo kama Mbezi beach-middle class iliyochangamka.
Mikocheni ni hizo bei za 2M na kuendelea, of which very few can afford.
Kwa kipato kidogo Dar utaishi maisha ya mateso sana. Ndo maana Dar ALMOST kila mtu ni mwizi kwa namna anayoijua yeye.
Hahaha kuna brother mmoja ana nyumba yake kali sana pale njombe, kila akiambiwa bei wanyotaka wapangaji anasema bora iote majani tu.A moment of silence for some of us tuliopangisha mkoani nyumba zetu kwa 300k tumekuja kuwa wapangaji Dar kwa 350k.
☺️
Hi kweli nakaa kwa Mtogole ndani kabisa kule mvua zikinyesha usalama mdogo halafu unatembelewa na mgeni utampelekajeWatu wa mikoani, hivi ulishawahi kujiuliza kwanini ndugu yako wa Dar anapiga chenga kila ukitaka kumtembelea? Ukiachana na chakula na gharama za Maisha, watu wengi wanaishi makazi duni sana hapa jijini.
Dar Unaweza hata kuishi kwenye nyumba ya 2M lakini ukitoka nje unakutana na frem za waucha chips au mkaa na madimbwi kama yote. Viongozi na wananchi we are all selfish.Upo sahihi kabisa, kuna nyumba nzuri sana ukiwa na bajeti nzuri.
Sinza kuna nyumba nzuriSisi wa mikoan Tutulize makomwe yetu hizo hekaheka bakini nazo watu wa daslam