Ukitaka ndoa ya utamaduni wa kizungu utaipata, yaani ile ya kushikana mikono, mabusu kila wakati, kila kitu ndani ya nyumba ni 50-50 (kama mwanamke atakubali), kubembelezwa na mwanaume kuwa emotional na nini na nini..(a fair tale one), zipo, ila huwa zina expire baada ya miezi 3, 6 mpaka mwaka...
Ila ukitaka ile ya utamadini wa Kitanzania, yaani ya makubaliano, majukumu pande zote 2, kwamba mwanaume ndio kiongozi wa nyumba, kwamba wewe mwanamke jukumu lako ni kwa mwanaume kwanza, halafu watoto, na kwamba final say iko mwanaume basi ndoa yaweza dumu miaka na miaka mpaka kifo kwaachanishe, hii ndoa ya Kitanzania furaha siyo swala muhimu, muhimu ni heshima na kila mwanadoa ajuwe nafasi yake, hii ndoa ya ki Tanzania kama ya mababu na mabibi zetu ndiyo ilikuwa nguzo kuu kuwalea, kuwakuza na kuwapa baraka wazee wetu,ila kama ujuavyo, mambo ya internet ndiyo mambo siku hizi, Watanzania hatujuwi tufuate ya EU, USA, Scandinavia, Australia au New Zealand! Tupo tupo tu, kuiga kucha, tunahangaika tu..