- Nina kiasi flani naombeni ushauri nifanye biashara gani
- Kwa kiasi flani naweza kufanya biashara gani
- Nimeachiwa urithi kiasi kadhaa nifanye biasara ipi
Sababu kuu ni kwamba hawana uzoefu, hiki ni kitu muhimu sana kwenye biashara sio cha kuchukulia poa, mtu mzoefu anazijua changamoto, ngozi yake imekomaa dhidi ya matatizo ya biashara, anajua vitu gani vinauzika vipi haviuziki, anajua soko lilivyo, n.k.
Kwa upande mwengine pia wanakosa connection za machimbo, siri za biashara, vishoka, n.k. connection sio za kubeza.
wanaofanikiwa ni wale wenye mioyo ya chuma kurudi upya kufanya biashara inayofanana maana mara ya pili hawaanzi kutoka sifuri, tayari wana kauzoefu na vi connection. wanaofeli ni wale walioanguka kisha wanaenda kufanya biashara tofauti kabisa ambayo hawana chembe ya uzoefu nayo wala connection, hawa ndio hupanga foleni kwa waganga wakihisi wamerogwa utawasikia "kila biashara mpya nafanya inafeli"