Watu wengi wanapitia changamoto kwasababu ya vifungo vya kiroho

Watu wengi wanapitia changamoto kwasababu ya vifungo vya kiroho

Samia atosha tukutane2030

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
17,728
Reaction score
49,762
November 15 mwaka huu nafunga miaka 39.

Kwa mazingira niliyozaliwa, kukua na sasa nilipo nathibitisha pasi na shaka kuwa matatizo yanayowapata watu 98% ni vifungo vya kiroho ambavyo watu hufungwa na mapepo, wachawi au shetani mwenyewe.

Hii 2% ndio matokeo ya ujinga. Mtu anapokosa maarifa juu ya jambo fulani lazima akwame mbele.
Turudi kwenye hii 98%

Watu wengi huku Afrika ni wachawi. Kuna wachawi ambao wanajijua na ofisi yao kuu au kazi yao kuu ni kuroga.
Kuna wachawi ambao hawajijui. Hawa ndio wengi zaidi. Hawa ndio marafiki, ndugu, workmates n.k
Mtu wa karibu au ndugu anapoona kuna mafanikio mbele yako anaposikia wivu, uchungu au hasira juu yako shetani huigeuza nafsi yake na kuwa nafsi ya kichawi.

Pale anapotakani ufeli, ushindwe au jambo lako likwame ndipo witchcraft mechanism inafanya kazi.
Huu uchawi ni ngumu sana kuuzhinda hasa ndugu mliyeshare damu. Kwasababu hauonekani mbele ya watumishi wa Mungu wa tia maji tia maji.
Kumbuka jambo hili👇👇👇

Ni mara ngapi ulipomsimulia ndugu yako wa karibu jambo lako lililoiva kabisa hilo jambo likafanikiwa kwa 100%?

Ukiona una ndugu au marafiki wachawi njia za kuwashinda ni mbili tu;
1. Kuwa msiri sana.
waone jambo lako likiwa tayari limekamilika kwa 100%.

Waone tu umeshamia nyumba mpya, umeshamia kwenye nyumba yako mpya. Wasikie tu ushaenda ng'ambo na sasa unataka kurudi.

2. Tembea katika roho.
Kutembea katika roho ni hali ya kuwa spiritual aware 24 hrs.
Macho yako na masikio yako ya rohoni yawe active.

Ukiwa active rohoni hata mtu anapokuambia hongera huku anakuroga moyoni kwa kutema witchcraft spells unajua. Hata zawadi zenye mambo meusi utaziona kwa uhakika.

Ndoa nyingi ziliharibika siku ya harusi. Zawadi zenye uchawi, vigelrgele vyenye uchawi vimeharibu ndoa.

Mzee mmoja, tena Askofu kuna jambo tulikwazana kidogo, Mzee akaniambia ubarikiwe. Rohoni nikapata signal kuwa hii si baraka ni uchawi kwahiyo ninatakiwa niushughulikie chap.

Ukiwa upo tu na unawamini watu sana utakuja kupokea baraka mfu.

Yaani zawadi yenye kifungashio kizuri kumbe ndani ni mavi.
 
Nna Baadhi ya Rafiki zangu nikiwaambia mipango yangu aisee inakwama kabisa hasa mmoja hivi ni Mwl.

Hivi mchawi akiwa Africa anaweza mroga mtu yupo europe? Uchawi siuamini sana ila upo.
 
Kuna uzi nilichangia humu siku chache nyuma, nilisema njia ya kujua mtu mwema kwako kwa usahihi kabisa, nj ya kiroho, kupitia hisia na ndoto/maono tu. Hata mtu ajifanye mwema vipi katika Ulimwwngu wa Kimwili, Ulimwengu wa roho utakuambia tu.

Ni kweli kukwama kwingi ni mambo ya kiroho kwa asilinia kubwa.
 
Back
Top Bottom