SI KWELI Watu wenye Damu kundi B hawatakiwi kula kuku

SI KWELI Watu wenye Damu kundi B hawatakiwi kula kuku

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
<div class="bbWrapper"></div>
 
Tunachokijua
Makundi ya damu ni uainishaji wa damu kwa kuzingatia kuwepo au kutokuwepo kwa dutu za antijeni za kurithiwa kwenye uso wa chembechembe nyekundu za damu (RBCs).

Antijeni hizo zinaweza kuwa protini, kabohaidreti, glikoprotini au glikolipidi, kutegemeana na mfumo wa aina ya damu.

Kuna makundi makuu manne ya damu ambayo ni A, B, AB, O na kila kundi lina aina yake ya razazi ambazo ni (+) na (-).
1712219889216-jpeg.2953585
Je, ni kweli watu wenye kundi "B" hawatakiwi kula kuku?

Kumekuwepo na madai kuwa watu wenye damu kundi B wasile baadhi ya vyakula ikiwemo Kuku huku wakielezwa kuwa chakula hicho si salama kwa afya zao.

Ukweli ni kwamba hakuna ushahidi wowote wa kisayansi unaothibitisha kuwa kuku si salama kwa watu wenye kundi B la damu, watu wenye kundi hilo la damu wanaruhusiwa kula vyakula yote kama yalivyo makundi mengine.

Madai hayo yanakanushwa zaidi na Wizara ya afya, kupitia mtandao wa X imekanusha kuwa watu wenye kundi B la damu hawana sababu yoyote ya kuepuka kula kuku, kanusho hilo limefafanua kuwa si kweli kuwa watu wenye kundi B la damu hawaruhusiwi kula kuku kwani hakuna ushahidi wowote wa kisayansi unaothibitisha madai hayo.

GKTdK6CXQAAuZG_
Kufuatia kanusho la Wizara ya Afya, Jamiicheck imethibisha kuwa taarifa zinazodai watu wenye kundi B la damu wasile kuku ni taarifa za Uzushi.
Back
Top Bottom