byakunu
JF-Expert Member
- Sep 13, 2016
- 583
- 1,318
Sisi watu weusi sijui nani alituroga, mimi katika pita pita zangu hapa Tanzania sijawahi kukuta mlinzi wa kihindi au au wa kiarabu, mlizi wa kizungu au wa kichina, ila sisi ngozi nyeusi ndo tunapenda penda kazi za ulinzi, kushinda magetini na manguo ya dark blue, ukiona ndugu yako ana taka kazi za ulinzi kemea sana pepo hilo, mzabe vibao akatafute kazi nyingine, hii tumezidi.
Tunakua na maisha duni kwa sababu tunapenda kazi za chini chini, shule tunakimbia umande, hatutaki kujituma ndo tunaishia kushinda kufungua mageti maisha yetu yote. Kwanini sio wachina sio wahindi au wazungu wao wasiwe walinzi? tusome bas kama wao, tumejazana huko ma Gardaworld kama makenge yasio na mwelekeo.
Walinzi wa kizungu utawakuta kwenye embassy zao kama US Embasy , British council na balozi zingine, ila humu kwenye mastoo na magodauni ndo sisi tunazaliana humo, tunalinda na mapanga na masululu shwain kabisa sisi chakula maandazi na mihogo.