Watu weusi watabaki masikini na duni milele

Ecowas yuko tayari kushirikiana weupe kumtwanga Niger wakati wananchi wameyaunga mkono mapinduzi,Afrika bara lililoacha utamaduni wake na kufata tamaduni za weupe[emoji24][emoji24]
Si ndio hapo,eti ECOWAS, Nigeria, ufaransa na USA ndio wanaumia kupinduliwa kwa kibaraka wao badala ya wananchi ndio waumie
 
Hata hao wazungu katka swala la imani shetani wanamfananisha na mtu mweusi ...... sisi tunamfananisha yesu na mzungu [emoji125][emoji125]
 
Sisi hatujikubali na hiyo ndio shida inapoanza.
Ni wepesi wa kupuuza asili yetu na kucopy ya wengine.

Kingine tunasema tunabaguliwa wakati ubaguzi tunauanza sisi kwa kubaguana sisi kwa sisi.

Kuna mdau hapo kasema USA ilipata uhuru wake miaka 200+ iliyopita huko so na sisi twende taratibu, mimi sikubaliani na hoja ya jamaa kwasababu hizi..

Kipindi hao watu wanajijenga kwa kupitia vita, maandamano ya ndani, kupishana mawazo na mitazamo hakukua na msukumo sana toka nchi kubwa za wakati huo na ukizingatia USA ilikua na watu wa mataifa tofauti duniani.
Leo hii uanze kujitafuta mabeberu watakutupia jicho, mrusi atakutupia jicho, mchina atakutupia jicho, mwarabu atakutupia jicho wote hao watataka ukaribu nawe ili wakupige kwa kujifanya ni rafiki yao mpya.
Ukikaidi wataungana na hutafika popote tena.

Naweza kusema nadhani nchi nyingi za Africa ni kama tumechelewa, kipindi cha kukua kilikua kile tulichotawaliwa, kilikua kile ambacho tumepata uhuru(walau tungejipigapiga) ila kwa sasa mikono ni mingi mno.

Tutajifariji tu ila kupiga hatua kua kama wao sio leo.
 
Wao wakiwa na miaka 60 ya uhuru,hali ya uchumi ilikuwa sawa na hii ya kwetu?
 
Kama Burkina Faso kaamua kusimama na Niger ni jambo zuri sana,ni wakati wa Afrika kusimama na kuwa kitu kimoja ni kheri tuwe masikini tukiwa na mali zetu kuliko kuwa masikini uku tukiachiwa mashimo tupu
Unazungumziaje kuhusu bandari yetu!
 
Hata ulipokea Imani yao ya Kikristu, una uhakika na Yesu wao. Kwa wenye Imani Kali mtanipinga, leteni mapovu.
 
Changes start with you. By JKN.
Ukibadirika wewe waafrika watakuwa wamebadirika.
Wanao ibadili marekani sio wengi ni wacgache kabda 10% tu.
Wengine ni mkumbo ndio unaowabeba.
 
Kitu kikubwa ambacho kilifanyika ni kuumaliza utamaduni wetu na hii ilifanyika kupitia dini. Dini ni sehemu ya utamaduni. Huwezi kuendelea katika nyanja zozote ikiwa huna utamaduni wako unaokuongoza.


Mwarabu, mzungu,myahudi,mchina,mhindi, mjapani n.k wote hawa wana utamaduni wao ambao wameamrishwa waufuate na kuutekeleza mpaka kwenye vitabu vyao vya dini.Hali hii imewapelekea kujikubali,kujiamini,kujithamini,kujiheshimu, kujipenda n.k!!!!!!!!!


Ustaarabu ni hatua ya juu ya maendeleo iliyopigwa na jamii fulani katika nyanja zote. Ustaarabu huigwa, hakuna jamii isiyoiga utamaduni wa jamii fulani kwa lengo la kuboresha bila kuharibu msingi mzima wa utamaduni husika.


Leo hii jambo lolote linatazamwa kwa kutumia picha ya mwarabu (uislamu), mzungu (ukristo) na kwa mbali uyahudi!!!!!!!!! Siyo kwa mtazamo wa kiafrika tena!!!!!!
Naamini hiki ndiyo kifungo kikuu na kibaya kuliko vyote ambavyo mwafrika amefungwa!!!!!!!!!

Naomba kuwasilisha!!!!!!!!!!!!


How culture is related to development?



Culture influences development from the moment we're born, making an impact on us as we grow. For instance, culture can affect how children build values, language, belief systems, and an understanding of themselves as individuals and as members of society.


Cultural Influences on Child Development | Maryville Online


https://online.maryville.edu
 
Tatizo linaanzia Kwa watu weusi wenyewe Kwa wenyewe wanabaguana, wachache wakipata hawataki wengine wapate (Ubinafsi)
Ushirikiano kwenye mambo ya maana ni wakinafki Tu .

Viongozi wanaongoza kusema watu walipe Kodi wkt wao wanongoza Kwa kughushi na kuiba hizo Kodi 🥴

Kuanzia viongozi WA juu mpka Kwa Mwenyekiti wa mtaa asilimia kubwa Wana mitazamo ya kibinafsi na kilafi .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…