Watu weusi watabaki masikini na duni milele

Watu weusi watabaki masikini na duni milele

Wenye mamlaka ya kufanya hayo mabadiliko kama hawafanyi unategemea wewe mwenyewe utaweza kufanya hayo mabadiliko kwa bara zima?

Kwamba, unadhani wewe binafsi unaweza kubadilisha mfumo wa Elimu wa nchi nzima ukiwa wewe kama wewe?

Mtu mmoja mmoja, Hawezi kubadilisha mfumo mzima wa nchi au bara.

Inatakiwa wahusika wenye mamlaka na viongozi wayafanye hayo.

Ndio maana watu wana lalamikia viongozi wenye mamlaka wafanye mabadiliko.

Sasa, Usipo lalamika hao viongozi wata fahamu vipi mifumo inahitaji mabadiliko?

Lazima walalamikiwe ili warekebishe.

As an individual you can't change the whole continent.

Huku kudanganyana na misemo uchwara kama huu wa "Changes begins with You" Halafu kuna viongozi wajinga wachache hawataki changes zifanyike Haisaidii kitu.

Lazima watu walalamike ikibidi hata kwa Vita na maandamano.
Kuna watu hata hawatambui maendeleo yanatakiwa yaanzaje broo
 
Ndo maana nakwambia mimi ningekuwa mkuu jeshini ningepindua nchi mchana wa saa nane kweupe.

Ukiruhusu sana demokrasia isiyo na mipaka utashindwa kufikia malengo ya msingi kwa wakati.

Gaddafi hakuifikisha libya pale ilipokuwa kwa kuruhusu demokrasia za kibepari
Kwa hiyo ukipindua serikali tu tayari thamani yako kama mtu mweusi itapanda?

Tupe ushahidi wa utofauti wa ukuaji wa kiuchumi wa nchi zinazoongozwa Kijeshi na hizi zinazoongozwa Kiraia.
 
Sisi tumewekeza kiroho na hicho ndio kitu chenye thamani.

Hizo anasa za kumiliki majumba na vitu vya kifahari inaonekana ni ujanja katika vision ya kibinadamu.

Sisi waafrika tuna hazina yetu mbinguni hakuna haja ya kuotesha uyoga ambao hautakusaidia kwenye future life.
Umeongea ujinga mkubwa sana, mbinguni Unapajua wewe? Uliendaga lini?
 
Kila tatizo lina chanzo chake ... wengi tunachukia waafrika kuwa masikini, kudharaulika,nk je wengi tunajua pamoja na sababu nyingine walizosema wengine sababu kubwa ni weupe wamehakikisha tunakuwa masikini, na tunaendelea kutojitambua ili waendele kututawala....kumbuka ukimwamsha aliyelala utalala wewe...
 
Km umekata tamaa ya masiha qwe jinyonge tu jiubge na mtetezi wa wanyonge, Nigeria ni pure blacks na ni nchi ya kwanza kwa uchumi Afrika, tajiri wa kwanza Afrika ni pure black Dangote, nchi km Botswana ni blacks na wana uchumi mzuri sana. We una inferiority complex na kweli kwa akili hiyo hutatoboa wakati wenzio wanapambana. Marekani tangia ipate uhuru ina miaka 247, sisi tuna miaka 60, kwa akil yako unafikiri miaka mingine 200 ijayo Afrika itakuwa wapi. Ndugu tuliza boli kila jambo lina pakuanzia, hayo maendeleo yameanza Ulaya yatafika hata Afrika. Hata Ulaya kulikuwa kuna rushwa sana, hayo mambo hayataisha, muhimu tupambane tuiunge serikali yetu mkono kwakufanya kazi kwa bidii na kulipa kodi stahiki.
Afrika hii ije iendelee wakati kila siku ni kurudi nyuma kama treni ya Godegode. Afrika nzima ilikuwa nzuri sana wakati wa ukoloni kuliko ilivyo leo.

Afrika bure kabisa. Watawala tulio nao leo ni mafisi watupu halafu eti ndio Afrika iendelee? Endelea kujitekenya na kucheka mwenyewe.
 
Watu weusi wana uwezo mdogo wa kiakili na ndio maana nchi nyingi za kiafrica bado kuna umaskini wa kutupwa.

Hatuna uwezo wa kutatua changamoto zetu.

Barabara tunajengewa, madaraja tunajengewa, tunaagiza asilimia kubwa ya vitu tunavyotumia.

Ni nadra sana kusikia kampuni ya kitanzania imepata tenda ya kufanya kazi fulani kwenye nchi nyingine.
 
Kila tatizo lina chanzo chake ... wengi tunachukia waafrika kuwa masikini, kudharaulika,nk je wengi tunajua pamoja na sababu nyingine walizosema wengine sababu kubwa ni weupe wamehakikisha tunakuwa masikini, na tunaendelea kutojitambua ili waendele kututawala....kumbuka ukimwamsha aliyelala utalala wewe...
Tatizo kubwa linaanza kwetu wala si kwa weupe
 
Kwa hiyo ukipindua serikali tu tayari thamani yako kama mtu mweusi itapanda?

Tupe ushahidi wa utofauti wa ukuaji wa kiuchumi wa nchi zinazoongozwa Kijeshi na hizi zinazoongozwa Kiraia.
Kwani ukiipindua nchi ndiyo lazima uingoze kijeshi ?

Gaddafi ile ya Libya ilikuwaje ?

Ukiruhusu demokrasia itumike kwenye kila kitu hautoendelea.

Weka demokrasia baada ya kuwa umeshaendelea tayari
 
Kiongozi wa nchi ya fulani ya Kiafrika aliulizwa kwanini nchi yako masikini ilihali ina kila kitu jibu alilotoa ni kwamba hajui[emoji24]
 
Nashangaa sana NIGERIA na ukubwa wake eti ndiyo ya kwanza kuishawishi ECOWAS nzima waingie NIGER kijeshi, ni ujinga mtu kuhangaika na mataifa mengine wakati kwake tu pale boko haramu wamemshinda, magenge ya wahalifu yanateka na kuua watu kila kukicha na wameshindwa kudhibiti hiyo hali alafu leo wapeleke jeshi NIGER kwenda kumrudisha madarakani kibaraka wa weupe.

Au kwa sababu wanajua wakiingia kijeshi NIGER weupe watawaunga mkono ndo maana wanaji-aminisha hivo.

Bora Burkina faso ilisema wazi kuwa, ecowas ikiingia NIGER kijeshi itakuwa pia imetangaza vita na sisi.

Na leo naona NIGER wamefunga anga yao hakuna ndege kupaa, maana yake ndege itakayoonekana angani ni halali yao mpaka pale watakapoifungua anga tena.
Mapinduzi ya kijeshi hayajawahi kuwakomboa wananch kiuchumi.
 
Sana.

Kwa kiasi kikubwa umaskini na uduni wetu unasababishwa na sisi wenyewe wala siyo wazungu.

Hasa uongozi mbovu (hili ndiyo tatizo cronic) na pili sisi waafrica hatujafunzwa kujikubali na kujipenda wenyewe, kuyapenda mataifa yetu, kwa kifupi uzalendo hatuja funzwa
Hawa wazungu baada ya kuondoka tunawatumia kama kisingizio.
Hatupaswi kusahau ukatili wao na ukoloni.
Lakini kwa suala la maendeleo, ni suala la nchi husika.
Hata Tanzania 80 ya uchumi inashikiliwa na Asians.

Huku wazawa wakibanwa vilivyo, hususan kama hautokei katika familia au koo zenye reputation nzuri ya wakina Oyee...Oyeee.

Hakuna mipango thabiti ya maendeleo kwa kweli.
 
Alhamdulillah, Sipo kwenye list ya mleta mada.mi mweusi na nikmesafiri nchi kadhaa, nimewazidi weupe mambo kadhaa na wao wamenizidi kadhaa.
 
Story fupi ya kuchekesha na kusikitisha ni kwamba watu weusi wao kwa wao hawapendani na wanafitinishana na wako radhi kuchomeana utambi kwa maboss zao weupe, ili mmoja aharibikiwe mmoja akidhani atakuwa juu na atapendwa.

Mawazo ya maji machafu! 😂
 
Back
Top Bottom