Watu wote duniani wangekuwa hivi, dunia ingekuwa na amani na furaha kuu

Watu wote duniani wangekuwa hivi, dunia ingekuwa na amani na furaha kuu

Setfree

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2024
Posts
6,238
Reaction score
8,194
Watu wote duniani wangekuwa wanaishi maisha haya wanayoishi Wakristo wa kweli, dunia ingekuwa na amani na furaha kuu. Wakristo wa kweli:
  1. Hawalipi kisasi – badala yake huacha Mungu mwenyewe alipe (Warumi 12:19).
  2. Hawaibi – wanaishi kwa uaminifu na kuridhika na walicho nacho (Waefeso 4:28).
  3. Hawatukani – maneno yao ni ya neema, ya kujenga, si ya kuumiza (Waefeso 4:29).
  4. Wanaheshimu kila mamlaka iliyowekwa na Mungu – huwaombea viongozi (Warumi 13:1-2).
  5. Hawapigani katika ndoa – wanafanya bidii kupendana, kuvumiliana na kusameheana (Wakolosai 3:13-14).
  6. Hawaui binadamu wenzao – wanaheshimu uhai kwa kuwa ni zawadi kutoka kwa Mungu (Kutoka 20:13).
  7. Hawavuti bange wala kunywa vileo vinavyosababisha ugomvi – hujiepusha na chochote kinachoharibu afya ya akili (Methali 20:1).
  8. Hawadhulumu mtu – wakiajiri wafanyakazi hawawanyanyasi wala kuwanyima stahiki zao. Wanapendezwa na haki (Mika 6:8).
  9. Wakikopa, wanalipa deni – kwa sababu wanajua kutokulipa deni ni kuvunja maagano - ni dhambi (Zaburi 37:21).
  10. Wana moyo wa msamaha – hawatunzi kinyongo wala chuki (Mathayo 6:14-15).
  11. Huishi kwa amani na kila mtu kadiri wawezavyo (Warumi 12:18).
  12. Hutoa msaada kwa wahitaji – hujitolea kwa upendo na huruma (Matendo 20:35).
  13. Wanakataa rushwa na vitendo vya kifisadi – huishi kwa uadilifu (Kutoka 23:8).
  14. Huomba kwa ajili ya maadui zao – hawawatakii mabaya adui zao, badala yake wanawaombea wapate wokovu (Mathayo 5:44).
  15. Wanaishi maisha ya kiasi – hawafuati tamaa za dunia hii (Tito 2:12).
  16. Huulizana hali na kujali wengine – wanapenda kuwa na umoja (Wagalatia 6:2).
  17. Wanaheshimu ndoa na kujiepusha na uzinzi – wanatosheka na mme mmoja na mke mmoja, mambo ya nyumba ndogo hawana (Waebrania 13:4).
  18. Hawatelekezi watoto, bali wanawalea katika hali ya kumcha Mungu (Mithali 22:6).
  19. Wanajitahidi kuwa mfano mzuri mahali pa kazi, nyumbani na mitaani (1 Timotheo 4:12).
  20. Wakikosewa, wako tayari kusamehe hata saba mara sabini – hawana la kuwakwaza (Mathayo 18:21-22
  21. Hawabagui watu kwa rangi, kabila, au hali yao ya maisha, kwa kuwa katika Kristo, hakuna Myahudi wala Myunani, mtumwa wala aliye huru (Wagalatia 3:28).
  22. Hawana tamaa ya kujilimbikizia mali wala faida binafsi. Ni wakarimu. Wanapenda kuwasaidia yatima na wajane, kwakuwa wanajua tamaa ya mali ndiyo chanzo cha migogoro mingi duniani (1 Timotheo 6:10).
  23. Wanawaombea wagonjwa, na kuwatia moyo waliokata tamaa. Mioyo yao inapenda kuwasaidia wenye mahitaji (Yakobo 1:27; Mathayo 25:35-36).
  24. Hawajishughulishi na uchawi, ushirikina wala kulogana, kwakuwa Biblia inawakataza kujihusisha na matendo ya giza (Kumbukumbu la Torati 18:10-12; Wagalatia 5:19-21).
  25. Wakristo wa kweli, kabla hawajaoa au kuolewa hujiepusha na uasherati na mambo machafu; wanatambua kwamba miili yao ni hekalu la Roho Mtakatifu, haipaswi kuchafuliwa (1 Wakorintho 6:18-20).
Maadili hayo mema yanatoka kwenye Biblia. Hakika Biblia ina hazina zilizositirika. Ndio sababu shetani anaipiga vita Biblia na kuwazuia watu wasiisome. Shetani hapendi tuwe na amani wala furaha.

Tuwahimize watu wasome Biblia na kuyafanyia kazi maagizo yote ya Yesu, tutaona furaha, amani na utulivu vikishamiri katika maeneo mbalimbali ya maisha yetu.
 
HAKIKA MKUU

Ukristo umechangia pakubwa katika amani kwa maana ukristo haukufundiishi kuipenda au kuipiganua dini bali kuipigani nafsi yako katika wokovu wa bwana.

KAMA WEWE NI MKRISTO BASI HONGERA SANAAA🎉🎉🎉🎉🎉🎉
 
Ungesema hivi watu wote wangefuata mafundisho ya biblia hapo ingeleta maana,maana wakristo wapo lkn hawayaishi hayo

usikurupuke
 
Nimeipenda sana hiyo point: Ukristo haukufundishi kuipigania dini. Asante mkuu kwa kuchangia
 
Mbna kabla hatujaletewa dini tuliishi kwa amani na maadili yetu yalikua mazuri tu, ila walipokuja waleta dini wakatufanya watumwa kabisa na kututendea ukatili?
Walioleta dini walitukatili na bado wanaendelea kutukatili.... Utu wa mtu upo ndani yake na si kwenye dini kama unavyotufundisha Madame
 
Ungesema hivi watu wote wangefuata mafundisho ya biblia hapo ingeleta maana,maana wakristo wapo lkn hawayaishi hayo

usikurupuke
Soma kwa utulivu, mkuu. Nimesema Wakristo wa kweli.
Au kama kimombo unakipenda zaidi...Genuine Christians/Faithful Christians/Committed Christians/Practicing Christians/Biblical Christians
Hao unaosema hawayaishi hayo, ni Wakristo wa jina tu.
 
mental health is real
You're already a senior member — impressive. But unless you make the leap to JF-expert member status, some of these higher-order arguments might remain just slightly out of reach. Press on — understanding grows with elevation😎
 
Mbna kabla hatujaletewa dini tuliishi kwa amani na maadili yetu yalikua mazuri tu, ila walipokuja waleta dini wakatufanya watumwa kabisa na kututendea ukatili?
Walioleta dini walitukatili na bado wanaendelea kutukatili.... Utu wa mtu upo ndani yake na si kwenye dini kama unavyotufundisha Madame
Kama ulikwepa kusoma somo la Historia, ngoja nikumegee:

David Livingstone (mpelelezi Mkristo wa karne ya 19), alishuhudia ukatili mkubwa wa utumwa uliokuwa ukifanywa na Waafrika kwa Waafrika hata kabla ya biashara ya watumwa kuimarishwa na Waarabu au Wazungu.

Watafiti wa Historia kama John Iliffe wameandika kuwa jamii nyingi za Kiafrika zilikuwa na mifumo ya kifalme na vita vya mara kwa mara kati ya makabila ili kushindania ardhi na mali. Na kuna makabila yalikuwa yanajimwambafy kuwa ni mashujaa wa kuiba ng'ombe za watu wa makabila mengine.

Kabla ya dini, kulikuwa na tohara za kikatili, ndoa za kulazimishwa, na kafara za binadamu katika baadhi ya maeneo.

Kabla ya dini kuna maeneo watu walikuwa wakiishi kwa hofu ya uchawi na ushirikina. Mtu akijenga nyumba nzuri analogwa.

Hayo ndiyo maadili mema unayodai yalikuwepo kabla ya Ukristo kuingia?
 
Hawabagui watu kwa rangi, kabila, au hali yao ya maisha, kwa kuwa katika Kristo, hakuna Myahudi wala Myunani, mtumwa wala aliye huru (Wagalatia 3:28).
Hapa ungeongezea hawabagui watu kutokana na imani na misimamo yao ingekuwa bora zaidi
 
Kama ulikwepa kusoma somo la Historia, ngoja nikumegee:

David Livingstone (mpelelezi Mkristo wa karne ya 19), alishuhudia ukatili mkubwa wa utumwa uliokuwa ukifanywa na Waafrika kwa Waafrika hata kabla ya biashara ya watumwa kuimarishwa na Waarabu au Wazungu.

Watafiti wa Historia kama John Iliffe wameandika kuwa jamii nyingi za Kiafrika zilikuwa na mifumo ya kifalme na vita vya mara kwa mara kati ya makabila ili kushindania ardhi na mali. Na kuna makabila yalikuwa yanajimwambafy kuwa ni mashujaa wa kuiba ng'ombe za watu wa makabila mengine.

Kabla ya dini, kulikuwa na tohara za kikatili, ndoa za kulazimishwa, na kafara za binadamu katika baadhi ya maeneo.

Kabla ya dini kuna maeneo watu walikuwa wakiishi kwa hofu ya uchawi na ushirikina. Mtu akijenga nyumba nzuri analogwa.

Hayo ndiyo maadili mema unayodai yalikuwepo kabla ya Ukristo kuingia?
Kama ni kweli basi naungana na wewe
 
Kama ni kweli basi naungana na wewe
Vipi lakini umeishaacha kulewa? Kama bado, jikumbushe tena huu uzi:
 
Vipi lakini umeishaacha kulewa? Kama bado, jikumbushe tena huu uzi:
Naelekea kuacha
 
Back
Top Bottom