Watu wote hapa ambao hawaamini kama Mungu yupo someni hapa

Watu wote hapa ambao hawaamini kama Mungu yupo someni hapa

Brojust

JF-Expert Member
Joined
Sep 17, 2016
Posts
349
Reaction score
1,024
Shalom watu wa Mungu.

Moja kwa moja kwenye mada, wanasayansi na wana imani watatusaidia.

Je, Uhai wako ulianza tu pale ambapo mbegu moja ya mzee wako ilipokutana na yai la mama yako ?

Je ulikuwa unajitambua kwamba tayari mimi ni binadamu na ile miezi tisa wakati uko tumboni ulikuwa unahisi nini (najua hisia zilikuwa kwa mbali sana) je, ulikuwa unahisi?

Je, Baada tu ya kuzaliwa ukirudisha memory zako nyuma utakumbuka siku yako ya kuzaliwa yaani kuingia kwenye ulimwengu?

Je ni katika nipindi cha miaka mingapi ulijitambua na kuanza kujielewa na kufanya matendo kama binadamu wa kawaida mpaka hii leo ni mtu mzima na umejiunga na JamiiForums na unasoma post hii.

Mimi binafsi kuna kumbukumbu huwa inakuja ila machoni mwangu nilikuwa naona rangi nyekundu tu. Lakini nahisi pale ndio uhai uliingia kwenye roho na nikatokea mimi ambaye sasahv nipo jamiiforum na naandika post hii.

NB; mnaopendaga kuweka vikombe vya chai kwenye comment piteni mbali kabisa na hii mada.

Nawasilisha.
 
Uzi tayari?, umetoa maelezo mengi pasipo ku-support point yako!
Una maelezo gani yanayotofautisha kuhusu kuku wa maabara(broiler) na kuku wa kienyeji kuhusu uhai?
 
Uzi tayari?, umetoa maelezo mengi pasipo ku-support point yako!
Una maelezo gani yanayotofautisha kuhusu kuku wa maabara(broiler) na kuku wa kienyeji kuhusu uhai?
Sijakuelewa mimi nataka kujua uhai wako wewe ulianzaje ? Au ulianzia wapi ?
 
Maswali yako yanaonesha ni maswali ambayo yanayohitajika kupatiwa majibu kwa njia za kiuchunguzi.

Lakini hayaoneshi kuwa jibu lake ni Mungu.

Wewe kutojua kilichojiri wakati ukiwa tumboni, inathibitisha kuwa hujui kilichoniri haithibitishi Mungu yupo.

Kweli Mungu anayetajwa kuwa ndiye muumba wa ulimwengu, binadamu na kila kitu kilichopo utumie mfano dhaifu kama huo kumthibitisha?
 
Imagine the pumping heart system , ni very complex and well structured 🙏, non stop till death no matter what!!!
-God is immanence
 
Hawaaminije kama yupo wakati wanasema hayupo?hayupo basi hayupo huna haja ya kuhoji unahoji wewe wa kazi gani wakati unaamini kabisa kwamba hayupo?

Kitendo cha kukanusha tu kwamba yupo ndani ya vichwa vyao kuna alarm inajaribu kuwaambia yupo lakini wana kiu ya kumjua tatizo namna wanayotumia kumjifunza ya ujuaji ndiyo imawefelisha.
 
Acha na wapinga MUNGU mkuu watakupasua kichwa tu

Endelea kumtumainia KRISTO na kuliombea kanisa lake lienende katika mafundisho na aman ya kweli
 
Mkuu kaza ubongo huo bado sana kwenye upande wa fikra!, hizo sio hoja zakutuita!.. inaonekana mwepesi kwenye hili jambo

Tumia fikra zako kwenye mambo unayoyaweza, nikushauri tu haya achana nayo!.
 
Mungu yupi huyo unamzungumzia wewe pamoja na wafia dini wenzako? Hapa ndipo mnaposhindwa kujitetea na kutetea hoja zenu.

Uislam una Mungu wake ambaye ni tofauti na Mungu wa ukristo, the same kwa wakristo Mungu wao ni tofauti na Mungu wa uhindu& Budha na dini nyinginezo.

Je huyo Mungu yupi mnaemuongelea? Na ukija ktk Afrika kila kabila lina tamaduni zake za upekee za kuabudu na kuamini mambo ambayo hayalingani na dini nyinginezo wala tamaduni zingine, na wamekuwa wakiomba na kupata majibu kutokana na wanachokiamini, je huyo Mungu ni yupi?

Majibu mnayo sema mlishaharibiwa akili na hizo dini zenu za kipuuzi.

Mungu ni jina tu la cheo cha kiumbe chenye nguvu dhidi ya viumbe wengine ktk kundi fulan.

Hata Simba/tembo wanaweza kuwa Miungu wa mbuga, mfalme/rais ni Mungu wa nchi, hili halina ubishi kama alivyo tajiri wa mtaa wako na kijiji chako huyo mtu mwenye pesa na heshima ndiye Mungu wa mtaa wenu utake ama usitaku ukweli haubadiriki.

Kiufupi huyo Mungu mnaetaka kutuaminisha kupitia vitabu vyenu vya kidini, hayupo na hajawai kuwepo na hatowai kuwepo, maana kaundwa na watu kulingana na fikra zao, mawazo yao na tamaduni zao, ndiomaana kila tamaduni inavutia upande wake kuwa Mungu wao ndie sahihi kuliko Mungu wa tamaduni zingine.

Mungu(nadharia) angekuwepo angejidhihirisha kwa njia anayojua yeye ili kuondoa hii mikanganyiko.

Note; Kuna Muumbaji wa Ulimwengu& Asili kiujumla ambaye si Mungu, na wala hana sifa za Uungu, huyu ndiye chanzo cha Ulimwengu, huyu hana sifa za viumbe maana yeye si kiumbe,

huyu huwezi kumuona maana hana sifa za viumbe(kuonekana),

huyu hana haja ya sadaka wala ibada zako maana yeye hanasifa za uhitaji

Huyu hapatikani sehemu yoyote ile iwe duniani, huko mbinguni mnakosema kupo, ama rohoni maana yeye ndie Muanzilishi wa mambo itawezekana vipi awe ndani ya ulimwengu? Kiufupi hapatikani ktk nadharia yoyote ile isipokuwa hisia tu za uwepo wa Nguvu zake(NATURE)

huyu hausiki na majanga ya dunia maana alishaumba sheria za kiasili za ulimwengu, ambapo kiumbe chochote kikienda kinyume na hizo asili lazima kipate matatizo(majanga, njaa, ukame, vita, vifo)

huyu pia hana haja sana na wewe binadamu, wewe ndiye unamuhitaji kwa uhuru wako na maamuzi yako, tofauti na hiyo Miungu ya dini zenu ambayo ukienda kinyume na dini eti utachomwa moto.

Sheria na hukumu za Huyu Muumba ziko wazi, ukienda sambamba na sheria zake za Asili utalipwa sambamba na hizo sheria, ukiua, ukiharibu maisha ya viumbe wengine, ukitesa maisha ya viumbe wengine adhabu ipo ambayo utaipata hata ukifa ambayo ni tofauti na hizo adhabu za Miungu yenu ya dini eti kuchomwa moto milele😀😀

Kiufupi nisiwachoshe, Dunia ina misingi yake ya asili ambayo watu wameiharibu kwa kwenda kinyume nayo, watu waliaharibu sheria za uumbaji wa dunia na kuunda sheria mpya za kishenzi ambazo baadhi ni DINI, SIASA, ELIMU inayopingana na asili, Kiufupi tunaishi ktk Uongo 100%, tunazaliwa ktk uongo, tunakuzwa uongo, tunalishwa uongo na tunakufa ktk uongo, hapa ndipo matatizo yanapotuandama.

Achaneni na hizo stories za wazungu&waarabu, Mungu wa hizo dini zenu hayupo mnapoteza muda, mnaabudu mizimu ya hao watu weupe ambayo wameipa majina ya kuwavutia, amkeni enyi wapumbavu
 
Hata
Imagine the pumping heart system , ni very complex and well structured 🙏, non stop till death no matter what!!!
-God is immanence
Hata wanasayansi wanaunda Non stop artificial heart inayopiga kaz zaidi ya hiyo natura heart ambayo ikipata tatizo kidogo tu mtu amekiwisha, kiufupi mkishindwa kutetea hoja za uwepo wa kitu fulani, msilete mambo ambayo mnaamini hayana ufumbuzi ili muyatumie kuaminisha watu kuwa kuna supernatural imeunda.

Amkeni enyi vilaza
 
Mkiambiwa prove uwepo wa Mungu mnaanza vitisho na storie za kusadikika.

Nikikwambia weka bible/quran pemben na umuelezee huyo mungu bila nukuu ya kitabu utaweza? Hapa ndipo wafia dini mnaonekana brainwashed kwa kushindwa kumuelezea huyo mnaeaminishana na Mungu.

Mungu ni nadharia ya wazungu&waarabu kuelezea chanzo cha uumbaji ambapo walishindwa kujua mambo yametokea vipi, wakaamua kumsusia huyo Kiumbe wa nadharia kuwa katenda, hawakuishia hapo wakatuaminisha na sisi kupitia mauaji, utumwa, ubakaji, vita na mambo mengi machafu.

Rudishen akili enyi watumwa wa wazungu

Hawaaminije kama yupo wakati wanasema hayupo?hayupo basi hayupo huna haja ya kuhoji unahoji wewe wa kazi gani wakati unaamini kabisa kwamba hayupo?

Kitendo cha kukanusha tu kwamba yupo ndani ya vichwa vyao kuna alarm inajaribu kuwaambia yupo lakini wana kiu ya kumjua tatizo namna wanayotumia kumjifunza ya ujuaji ndiyo imawefelisha.
 
Back
Top Bottom