Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Jumla ya watuhumiwa saba wamekamatwa na Jeshi la Polisi mkoani Iringa kwa kuhusishwa na mauaji ya kijana aliyedaiwa kuiba parachichi. Jeshi la Polisi limesema watuhumiwa hao wanashikiliwa kwa mahojiano na mara baada ya taratibu kukamilika watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma za mauaji zinazowakabili.
Kufuatia tukio hilo lililonaswa kwenye picha mjongeo na kusambaa mitandaoni, Serikali ya mkoa wa Iringa ikiongozwa na Mkuu wa mkoa Kheri James imechukua hatua za haraka kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha wahusika wanakamatwa. Aidha, RC Kheri James ametembelea eneo la tukio na nyumbani kwa marehemu katika eneo la Don Bosco, Manispaa ya Iringa, kutoa pole kwa familia na kuzungumza na jamii kuhusu umuhimu wa kudumisha utu na kuheshimu utawala wa sheria.