mtwa mkulu
JF-Expert Member
- Sep 11, 2013
- 8,586
- 11,227
Natamanigi sana kumsikia mogile machuki kutoka kisii kenya bila mafanikio
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Chivalavala S. ChivalavslaMiaka imesonga sana, maisha yamebadilika Kwa kiasi kikubwa.Tofauti na sasa ambapo ukiwa na simu janja au tarakirishi unapata taarifa zote zilizotokea na zilizovunjika 'breaking news', Zamani redio ilikuwa chombo muhimu ktk kupata taarifa na burudani.
Leo nimewakumbuka wale watuma salamu maarufu enzi zile,ingawa hata sasa wapo baadhi ya watu ambao ni maarufu ktk vipindi mbalimbali ukisikiliza redio km Clouds mfano kuna heri dereva babaji, shangwe dereva babaji, Daudi wakota n.k
Enzi hizo ukisikiliza kipindi cha mirindimo asilia na Malima Nderema au salamu Kwa wagonjwa, kuna majina maarufu huwezi kuacha kuyasikia wakati wa kutuma salamu.
Kuna huyu jamaa wa kuitwa Wajadi fundi Wajadi binadamu mashaka, yeye kila siku yupo safarini kuelekea mahuta shimoni, fundi Khamisi full migebuka wa mwandiga fashion sokoni Kigoma.
Lawena Msonda Baba mzazi kutoka chunya Mbeya.
Ally Mrangi Gigiri Mresa yeye mar kila siku yupo safarini kuelekea mabibo Dar es Salaam.
Zakaria Ndemfoo, Issa Mzee wa urembo kutoka Moshi. Lupa tingatinga "mdau asiyechuja" ndiyo ilikuwa slogan yake bila kumsahau Chesko Mzee wa matunda kutoka Africa Sana.
Kuna mdau akiitwa Limonga Justine Limonga na kuna huyu mama Abuu wa majani mapana. Kuna jamaa aliitwa Fikiri Dario Gakala wa GGM Geita na Filbert Kyenshambi kutoka Muleba-Nshambi, wapo wengi sn na tulikuwa tunaenjoy sana Enzi hizo
Unawakumbuka baadhi? Unazikumbuka kauli mbiu zao maarufu zilizotamba?
Hao wengi walitoka ukanda wa pwani kuanzia tanga, dar, lindi na mtwara yani pwani yote
Huyu alishaingiaga mjengoni enzi izo akivaa full nguo nyekunduKuwaya Waya wa Kuwaya Waya kutoka Lizaboni Nyumbi hii bombi hii!
Huyu mwamba alikuwa comedian balaa
thomas mushi kimbokaThomas Kimboka aliwakilisha sana miaka ya 90
🤣🤣🤣ilikuwa burdan sana kuwaskiza hawa jamaaWajadi binadamu mashaka, yeye kila siku yupo safarini kuelekea mahuta shimoni