Watuma salamu maarufu waliotamba kwenye vipindi mbalimbali vya Redio

Watuma salamu maarufu waliotamba kwenye vipindi mbalimbali vya Redio

Kuna mmoja wa chunya makongolosi namsikiaga sana R.F.A anajiita LAWENA NSONDA
 
Huyo wajadi fundi wajadi binadamu mashaka nakumbuka RTD enzi hizo
 
Father nagunwa nakomolwa aka (fanana)...singida,huyu yupo,anayetaka mawasiliano naye ani-dm
 
Ima Kulaya...

Jamaa wanapiga simu kipindi cha kuamshana asubuh na mim najiandaa kwenda shule nmewasha redio mkulima ya baba sebulen 😂😂😂
 
Walikuwa wanajitolea kweli kweli kwa vocha zao....

Ova
 
Pale pale mjini na ndio maana ikawa ni rahisi kumpata.....ni watu maarufu kwenye mji ule,tena kwasasa huyo Paul ana duka la jumla la retail shop

Nitarudi tena kwenye ule mji muda si mrefu nimepakumbuka ni almost miaka 2 sijafika
Aise namm nimepamiss San sumbawanga
 
Miaka imesonga sana, maisha yamebadilika Kwa kiasi kikubwa.Tofauti na sasa ambapo ukiwa na simu janja au tarakirishi unapata taarifa zote zilizotokea na zilizovunjika 'breaking news', Zamani redio ilikuwa chombo muhimu ktk kupata taarifa na burudani.

Leo nimewakumbuka wale watuma salamu maarufu enzi zile,ingawa hata sasa wapo baadhi ya watu ambao ni maarufu ktk vipindi mbalimbali ukisikiliza redio km Clouds mfano kuna heri dereva babaji, shangwe dereva babaji, Daudi wakota n.k

Enzi hizo ukisikiliza kipindi cha mirindimo asilia na Malima Nderema au salamu Kwa wagonjwa, kuna majina maarufu huwezi kuacha kuyasikia wakati wa kutuma salamu.

Kuna huyu jamaa wa kuitwa Wajadi fundi Wajadi binadamu mashaka, yeye kila siku yupo safarini kuelekea mahuta shimoni, fundi Khamisi full migebuka wa mwandiga fashion sokoni Kigoma.

Lawena Msonda Baba mzazi kutoka chunya Mbeya.

Ally Mrangi Gigiri Mresa yeye mar kila siku yupo safarini kuelekea mabibo Dar es Salaam.

Zakaria Ndemfoo, Issa Mzee wa urembo kutoka Moshi. Lupa tingatinga "mdau asiyechuja" ndiyo ilikuwa slogan yake bila kumsahau Chesko Mzee wa matunda kutoka Africa Sana.

Kuna mdau akiitwa Limonga Justine Limonga na kuna huyu mama Abuu wa majani mapana. Kuna jamaa aliitwa Fikiri Dario Gakala wa GGM Geita na Filbert Kyenshambi kutoka Muleba-Nshambi, wapo wengi sn na tulikuwa tunaenjoy sana Enzi hizo

Unawakumbuka baadhi? Unazikumbuka kauli mbiu zao maarufu zilizotamba?
Umesahau Matumla s Matumla wa kirombero kidatu Morogoro
 
Back
Top Bottom