Jamal Akbar
JF-Expert Member
- Oct 9, 2014
- 413
- 471
Kama unadhani ugoro hutumika mdomoni na puani pekee kama sehemu ya kilevi, basi fahamu umeongezewa matumizi mengine kwa wanawake, wanautumia kukata hamu ya tendo la ndoa.
Iwapo utapewa kiburudisho hicho kwa mara ya kwanza, hakika hutothubutu kukigusa kutokana na ukali wake, lakini hivi sasa baadhi ya wanawake mkoani Tabora wanauweka sehemu zao za siri kukata kiu ya tendo la ndoa.
Mwanaidi Nyagumbi, mkazi wa Kijiji cha Kadata wilayani Nzega ni mmoja wa waliohamisha penzi kutoka kwa mumewe kwenda kwenye ugoro.
Mwanaidi alichukua uamuzi huo baada ya kukimbiwa na mumewe na amedumu kwenye kiburudisho hicho kwa takriban miaka nane sasa anayosema hajawahi kushiriki tendo la ndoa.
“Nimekaa miaka nane bila kushiriki tendo la ndoa, faraja yangu ni ugoro. Umekuwa ukinisaidia kumaliza shida zangu. Kwa mwezi naweza kuweka mara mbili, muwasho ninaoupata kisha nanawa na maji ya baridi ndio hunisaidia kukata hamu ya tendo la ndoa,” anaeleza mwanamke huyo.
Mwanamke mwingine ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini anakiri kuutumia ugoro kama kimbilio kutokana na kumkosa mtu wa kuwa baba watoto wake baada ya wazazi wake kuweka pingamizi kwa mwanamume aliyebahatika kuzaa naye mtoto.
“Ugoro ni kitu pekee ambacho siwezi kuacha kukitumia maana ndio mbadala wa mwanamume. Nikiutumia, hamu zote zinaisha na ni miaka mingi nimekuwa nautumia,’’ anasema.
Halima Abbasi anatumia ugoro kama njia ya kujikinga na magonjwa ya zinaa yanayosababishwa na muingiliano wa mwanamume na mwanamke kutokana na baadhi ya wanaume kutotaka kutumia kinga.
“Magonjwa yamekuwa mengi miaka hii, kuliko kuwa na mwanamume ni bora kutumia ugoro ambao ukiuweka sehemu za siri unapata ladha nzuri na tofauti kuliko hata kulala na mwanamume,” anasema Halima.
Halima anasema mwanamke akishatumia ugoro hana haja ya kukutana na mwanamume kwa sababu hamu ya tendo inakata kabisa
Chanzo: Mwananchi