Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,681
- 8,887
Bajeti ya Mwigulu Nchemba inayosomwa leo imependekeza tozo ya Tshs 382 kwa kila kilo ya gesi asilia inayotumika kwenye magari ikiwa na lengo la kuchangia mfuko wa kutengeneza barabara na kuleta usawa kwa magari yanayotumia mafuta.
Swali langu kwa Mwigulu, kwanini ahangaike na kuleta usawa na kitu ambacho hakizalishwi nchini? Wewe unazalisha gesi halafu unataka iwe sawa na mafuta usiyozalisha, hadi baba wa demokrasia Marekani kila siku anadhibiti bidhaa asizolisha kutoka China japo kinyume na sera ya biashara huru!
Haitapunguza morali ya kuhamia kwenye gesi na ambayo inapunguza matumizi ya fedha za kigeni kuagizia mafuta ambazo sasa zinatafutwa kwa tochi! Hata watu binafsi wanaoanza kuwekeza kwenye vituo vya kujazia gesi vilivyo haba wataanza kutafuta biashara nyingine kwani huku hakuna ishara njema tena.
Napendekeza waache watumiaji waongezeke, wakiwa wengi waweke tozo ndogo isiyo na athari ya chini ya tshs 100, kwasababu watakuwa wengi wakati ujao wakiichangia kidogo kidogo itakuwa kubwa kuliko kuharibu sasa na kuendelea kuhangaika na uhaba wa dola.
Pia, soma=> Dkt. Mwigulu: Tusamehe ushuru wa magari ya umeme na Gesi