Hawa wenye haka kamtindo ni washamba sana eti mtu anaandika xaxa badala ya sasa........ Akinijibu mtu hivo namfutilia mbalimtu kujibu text kwa vifupi , unakuta umetuma text ndefu mtu anajibu p,k, pp, kuandika texts za msingi kwa vifupi ani dah me mtu akiniandikia p,k,pp simjibu hadi akili imkae sawa
Du..[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]kuna x wangu mmoja nilimtumia sms kumjulisha kuwa wale wadogo zake walio kuwa wana tafuta kazi,awajulishe wanitafute niweze kuwapa maelekezo juu ya nafasi za kazi,mara paa mwanaume ananipigia simu na kunitumia sms kuwa mke wa mtu anauma...nikaishia kucheka na kumjibu kuwa ..unaumia nini wakati kitumbua unacho karibu..si utafune ,,unakaa muda wote umeangalia simu ya demu wako.badala ya kushughulika.
Hiyo tabia ya kupiga calls kumi inakera, piga mara moja then tuma sms kama unadhani ujumbe ni wa muhimu sana.
Kukata simu katikati ya maongezi (hii mara nyingi ni kwa wapendanao), watu mkipishana kauli kidogo tu mtu anakata simu, sijui anataka abembelezwe au vipi. Ukinikatia simu katikati ya maongezi hakika hutaona call yangu.
Kupiga simu then mtu haweki sikioni, ukipokea haongei, yupo zake anapiga story, unasema "vipi upo?" Ongea basi...nakereka balaa!!
Michepuko: unaweza kukupigia na kukuta upo kwenye kwenye mazingira hatarishi (upo na waziri mkuu kwa mfano) na inabidi uikate ile simu. Badala ya mtu kujiongeza, unashangaa anapiga tena na tena na tenaaa😀
Nikitoka kama hautaki kukasirika niulize umechukua simu?Nitakunyoosha
Ukinitext naweza kukuchanganya na mtu mwingine....unakasirika kesho tena vile vile.Hili hata mimi ninalo aisee japo sidhani kama hali ni mbaya kama yako
kuna x wangu mmoja nilimtumia sms kumjulisha kuwa wale wadogo zake walio kuwa wana tafuta kazi,awajulishe wanitafute niweze kuwapa maelekezo juu ya nafasi za kazi,mara paa mwanaume ananipigia simu na kunitumia sms kuwa mke wa mtu anauma...nikaishia kucheka na kumjibu kuwa ..unaumia nini wakati kitumbua unacho karibu..si utafune ,,unakaa muda wote umeangalia simu ya demu wako.badala ya kushughulika.
Unatumia hela demu wako mpaka tena umpigie kujua kama kaiona ndipo atajibu nimeiona Asante.
Mama nikimtumia hela muda huohuo anaunga bando la mia 500,anakupigia utasikia "Asante mwanangu nimeiona ubarikiwe sana baba yangu, Mungu abariki za mikono yako najivunia kukuzaa wewe na wadogo zako wamefurahi sana.
Nakupenda mama,wadogo zangu wa kike wafundishe huo ukarimu kwa wanaume zao .
MDAU😱y niaje
WEWE:shwari vipi hali
MDAU:safi habari za huko?
WEWE:nzuri tunamshukuru Mungu
MDAU:vipi shemeji na watoto
WEWE:hawajambo kabisa.
MDAU:mambo yanakwendaje huko?
WEWE:tupo tunakomaa
MDAU:mmetunyima nini huko?
WEWE:hamna ndg jus tu
MDAU:wanasemaje huko?
Huwa nachoka kabisa maana ni kama sms kumi zote za aina moja tu.
Ni kweli japo siyo wote mwingine wala shida yeyote zaidi ya salamu tu.Haha ukiona hivyo anakupanga kuna shida anataka kukwambia
a) Umenipigia simu sijapokea, Baada ya muda kukuta call zako, nakupigia "Unaanza lawama" hawa naona nachoka kuwavumilia sasa.
b) Mtu kaanzisha mada mwenyewe kwa sms! Unamjibu kwa kutulia kabisa tena kwa ufafanuzi zaidi (kumbuka ni text) umeacha kufanya ulokuwa nalo. Kaipata kaisoma, Anauliza swali. Unacopy sehemu ya ile text uliomtumia, maana ndio jibu la swali lake lilipo! Anakuuliza tena, unacopy sehemu nyingine tena unamtumia! Baadae anakujibu 'Aaah' sawa.
c) Unachart na Mtu anatuma vitext vifupi, kukamilisha habari yake unajipata Haikuwa na haja ya text ziwe sita, kwa jambo lilelile moja, angelitumia tu sms moja, wala isingalikuwa refu ya kumaliza kurasa moja ya sms. Dah hivi Watu wa hivi huwa Mnaandika sms Miguu ikiwa wapi? Naona inapoteza muda aise!
Tuishi tu Tutaelewana.
Kama upo hivyo kwenye kuangalia blue tick na mie huwa nakereka mtu akikomaa nimekutumia msg nimeona blue tick ukauchuna (na mie huwa naamini mtu anaehitaji kitu cha muhimu lazima atapiga ama atatuma sms ya kawada ambayo uwe na kifurushi huna kifurushi itaingia (lazima nitamchimba mkwara wakati message inaingia nilikuwa na bundle yaani 4MB yaani muda ule ule nataka kujibu ikakata (maana kuna watu message za muhimu wanatuma kuitia whatsapp ambayo ni subject to bundle kwa mpokeaji hao mie ndo hinikera)Me katika yote ayo sina matatizo nayo lakini me ni lile swala la late replies na blue tick za whatsapp... fanya mambo yote lakin sio izo vitu mbili