Kama budget yako ni nzuri chukua kama Aliyochukua mkuu
CONTROLA maana ni 4g router utaweza kutumia line ya simu na pia ina function kama router ya kawaida kama una vifaa vingine vya ethernet ama wifi nyumbani itaviunganisha.
Router kubwa kama hio inauwezo wa kuunganisha vifaa vyote (bila internet) na kuifanya nyumba iwe connected. Mfano una desktop ama laptop, na smart tv, kupitia tv unaweza ukaangalia movie za kwenye desktop/laptop sababu tayari vipo connected kwenye same network. Unaweza hamisha mafile kwa haraka baina ya simu na simu, kuunganisha remote na tv (inasaidia sana remote og inapopotea ama kuharibika), kustream games toka kwenye pc ama console kama ps3 na ps4 kwenda kwenye vifaa vidogo kama simu, psp etc.
Hivyo ni vyema kwa matumizi ya kifamilia kuwa na router kubwa kama hio hata kama huungi bundle.
Ila kama budget ni ndogo hivi vi mobile wifi vipo vingi sana kuanzia 50,000 unapata mpaka laki 1. Havina functions kama hizo router kubwa ila vinaweza kutengeneza hotspot vizuri tu.