Nilichoka kuzunguka mkuu,na katika zunguka yangu yote maduka yote nakutana
na router ambazo niliweza zitambua hazina uwezo bila hata kukuuliza,hizo ambazo
nimekuuliza ndio zilikua zinanichanganya na jinsi bei zake zinavyotofautiana kukawa
kunanipa wasi wasi,nikawa nakuuliza ila mwisho wa siku nimechukua hii
DWR M960
nimekuja ijaribu kazini nione,kwakweli Haijaniangusha "sijutiii pesa niliyotoa" napata nilicho hitaji
nimedumbukiza line ya halotel,nataka nione usiku huko nyumbani maana hii ni ya HOME
nione hali itavyokua,ila mpk sasa speed yake si ya kawaida,niki connect WIFI ne simu
hamna page inayo load yani ni Tip Tap.Asante sana sana sana
Chief-Mkwawa you deserve being
Platinum Member asante tena na tena kwani kama si wewe leo ningeondoka na router zile
za mwanzo nilizokuuliza maana ndio zimejaa kila duka nililokua naingia nlikutana na zile
baada ya kuniambia SIO ndio nikapata nguvu ya kutafuta na hatimae nikakutana na kaduka kamoja
kana hyo M960 uliponiambia Hii ipo sawa kasoro haina Advance LTE nikasema naibeba hvyo hvyo.
nisipokushukuru nitakua mchoyo wa fadhila,Asante chief na Mungu akubariki.