Chief Wingia
JF-Expert Member
- Jul 12, 2013
- 2,653
- 4,744
Kwahiyo huu uvumi kuwa watarudishwa kazini ni wakupuuza
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Inaumiza, inauma sana, imetugharimu sana tuliokutwa au ndugu zetu kukutwa na janga hili lakini ni muhimu kufanya mambo sahihi kadri inavyotakiwa
Mimi binafsi watu wangu wa karibu sana wamepigwa na hili janga na familia zimeyumba na imetugharimu lakini kamwe siwezi kuilaumu serikali na kumtetea mtu aliyenunua au kughushi vyeti. Kamwe!!!!
Kosa ni kosa tuu haijalishi linakufaidisha au kukubeba kwa kiasi gani
Seems una huruma sana? Nitakaribia PM kwako.Roho mbaya inakutesa ka jiwe kukomoa komoa
Usiangalie kosa katika kughushi tu, angalia kosa katika kumwajiri, kosa katika kukubali utumishi wake kwa miaka mingi, kosa katika kuikubali kodi yake kwa miaka mingi.
Pamoja na kosa walilofanya, zile 10% zao za mafao walizokatwa wakipewa huo ni ubinadamu lakini wengi wao wameshakubali adhabu na pengine wana maisha yenye mwanga kuliko waliochukua hayo maamuzi. Siwatetei, mm ni muumini wa utu.
Umesoma ukaelewa?Kosa la kumwajiri lingetokea wapi kama asingefanya kosa la kughushi na kumuongopea mwajiri?
Kuhalalisha haramu nalo ni kosa lingine. Haramu haijawahi kuwa halali hata ukaitetea vipi
Kuumizwa tumeumizwa, kuumia tumeumia lakini tusijibebmbeleze ati tumeonewa. Kukubali kosa ni jambo jema
Lini bajeti yetu ilianyiwa kazi 100%?Bajeti ya 21\22 ni kama 33t, ya mwaka 22/23 ni kama 39t. Kutakuwa na bonge la ongezeko la mshara. Hakuna atapungukiwa take home ya 50,000 kwa kima cha chini. Mama oyee
Yani kulipa watu walioiba na kughushi vyeti ni sawa? Hii nchi haitakaa ifike mahali kwa mentality hizi wallah! Kama mnawekwa kwenye decision making na mentality hizi unadhani tutafika kweli?Roho mbaya inakutesa ka jiwe kukomoa komoa
Kuna waliondolewa Kwa makosa wamerudishwa. Cha ajabu kuna wenye vyeti feki mpaka Leo wanadunda makazini.Kwahiyo huu uvumi kuwa watarudishwa kazini ni wakupuuza
Umesoma ukaelewa?
Sijasema kaonewa mtu. Wanastahili yaliyowapata ila kama watapewa zile 10% walizokatwa kwenye miahahara still bado huo utakuwa ni utu tu.
Ni Sawa na kumtupa mhalifu jangwani na ukampa chupa ya maji ya kunywa.
Halafu wewe hujaumizwa ila ni tetea tetea wa serikali, usitumie nguvu sana kutetea maana hata hao yaliowakuta wamekubali makosa na wanaendelea na maisha.
Yaani akili zimgine!Hivi aliyugushi cheti si ndiye mwenye roho mbaya kwa kuwa ameziba nafasi ya mtu aliyestahili kupata hiyo ajira.Acha roho mbaya
Hatuelewani. Haya mafunzo unayotoa unajiweka kwenye utakatifu fulani. Mm sijaongelea utakatifu. Nimeongelea kuwa hakuna ubaya wakipewa ile michango na sijasema wizi ni jambo sahihi. Wasipopewa pia hawatakuwa wameonewa. Usihubiri.Hilo la mimi kuumizwa au kutoumizwa sijakulazimisha kuniamini. Nikiamini mimi mwenyewe inatosha
Kikubwa Tujifunze kuacha udanganyifu, tujifunze kukubali makosa yetu na kuyabeba! Udanganyifu wa vyeti ni wizi kama wizi mwingine
Hatuelewani. Haya mafunzo unayotoa unajiweka kwenye utakatifu fulani. Mm sijaongelea utakatifu. Nimeongelea kuwa hakuna ubaya wakipewa ile michango na sijasema wizi ni jambo sahihi. Wasipopewa pia hawatakuwa wameonewa. Usihubiri.
Kuiba na kutokujulikana hakuhalalishi wizi......Usiangalie kosa katika kughushi tu, angalia kosa katika kumwajiri, kosa katika kukubali utumishi wake kwa miaka mingi, kosa katika kuikubali kodi yake kwa miaka mingi.
Pamoja na kosa walilofanya, zile 10% zao za mafao walizokatwa wakipewa huo ni ubinadamu lakini wengi wao wameshakubali adhabu na pengine wana maisha yenye mwanga kuliko waliochukua hayo maamuzi. Siwatetei, mm ni muumini wa utu.
Sawa. Ni kosa hilo linajulikana.Mimi sijasema kuwa ni mtakatifu, wala kujiweka kwenye utakatifu, wewe ndio umeniwazia hayo.
Nilichokisema ni kwamba kughushi au kuiba vyeti ni kosa. Na siwezi kusema ni sawa ili kukuridhisha wewe
Kuhusu kupewa hiyo michango sijasema kwamba kuna ubaya. Ila kabla hatujadai hiyo michango kwa kulalamika na kulazimisha wataalamu wa sheria watuambie pia kuna adhabu au gharama gani kwenye kosa la kughushi kwa kukusudia
Narudia kusema tusiangalie tulipoumizwa au kuumia, tujiulize nani amepelekea sisi kuumizwa. Na nani aliyeghushi?
Kabisa. Upo sahihi.Kuiba na kutokujulikana hakuhalalishi wizi......
Ccm yenyewe huiba kura sembuse waliofoji vyeti?Yani kulipa watu walioiba na kughushi vyeti ni sawa? Hii nchi haitakaa ifike mahali kwa mentality hizi wallah! Kama mnawekwa kwenye decision making na mentality hizi unadhani tutafika kweli?